Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g94 1/8 kur. 3-4
  • “Na Tujijengee Jiji”

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • “Na Tujijengee Jiji”
  • Amkeni!—1994
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Jiji Liitwalo Henoko
  • Tofauti na Bado Yenye Kufanana
  • Majiji Mbona Yamo Taabani?
    Amkeni!—2001
  • “Jiji Limejaa Uonevu”
    Amkeni!—1994
  • “Majiji Yanafurika Watu”
    Amkeni!—2001
  • Ugumu wa Kulisha Majiji
    Amkeni!—2005
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1994
g94 1/8 kur. 3-4

“Na Tujijengee Jiji”

Na mleta habari za Amkeni! katika Ujerumani

YAELEKEA kwamba wewe waishi jijini. Kulingana na makadirio fulani, karibu nusu ya wakazi wa ulimwengu huishi humo. Chanzo kimoja chasema kwamba “katika mwendo wa sasa, kufikia mwaka 2000, itabidi majiji yatoshee zaidi ya asilimia 75 ya watu wote wa Amerika Kusini.” Pia chatuambia kwamba katika kipindi icho hicho cha wakati, idadi ya watu waishio katika majiji ya Afrika itaongezeka zaidi ya maradufu.

Hata ikiwa huishi jijini, yaelekea kwamba ama wewe hufanya kazi jijini, ama husafiri kufanya ununuzi wako humo, ama angalau mara kwa mara wewe hufaidika kwa mafaa na mapendezi yapatikanayo jijini pekee. Kila mtu huathiriwa na majiji. Maisha zetu zingalikuwa tofauti kama nini bila hayo!

Jiji Liitwalo Henoko

Ujenzi wa majiji ulianza zamani sana, sana. Kuhusu Kaini, mtoto wa kwanza kupata kuzaliwa, twasoma kwamba ‘alijenga jiji akaliita Henoko, kwa jina la mwanawe.’ (Mwanzo 4:17) Kwa kujenga jiji, labda likiwa dogo kwa kulinganisha na viwango vya kisasa, Kaini aliwekea kiolezo vizazi vya wakati ujao.

Hali ya asili ya wanadamu kutaka kuishi pamoja imefanya watu watake kuwa pamoja. Ni hivyo, si kwa ajili ya urafiki tu bali pia ili kuhisi usalama na ulinzi, hasa katika karne zilizopita ambapo mara nyingi jumuiya zilishambuliwa. Hata hivyo, si hayo pekee yamefanya wanadamu waanze kujenga majiji.

The World Book Encyclopedia chasema kwamba kuna mambo manne makuu ambayo yamechochea kujengwa kwa majiji. Hayo ni “(1) maendeleo katika teknolojia [mashine ziendeshwazo kwa mvuke, nguvu za umeme, mawasiliano], (2) mazingira yafaayo [kama vile mahali, hali-anga, mito na hivyo ugavi wa maji], (3) utaratibu wa kijamii [mamlaka, serikali], na (4) ongezeko la idadi ya watu.”

Majiji yamefanya biashara na idadi kubwa ya wafanyakazi kuwa mahali pamoja. Kwa hiyo, katika majiji mengi twaona ujenzi wa nyumba za gharama ya chini kwa ajili ya wafanyakazi na familia zao. Leo, kwa kuwa usafiri wa umma na wa kibinafsi wapatikana kwa urahisi, umbali hauzuii usimamizi wa kibiashara na wa kisiasa wenye mafanikio. Kwa sababu hiyo, majiji yaweza kuwa na uvutano katika sehemu za viunga.

Baadhi ya majiji ya kale yalifungamana pia kwa ukaribu na sherehe za kidini. Mwanzo 11:4 lasema: “Wakasema [yaani watu walioishi muda mfupi baada ya Furiko la siku za Noa], Haya, na tujijengee [jiji], na mnara, na kilele chake kifike mbinguni [utumike kwa ajili ya ibada ya kidini], tujifanyie jina; ili tusipate kutawanyika usoni pa nchi yote.”

Mambo ya kijamii, kidini, kiuchumi, na kijiografia na pia ya kisiasa yamehusika katika ujenzi wa majiji. Wakati uo huo, kwa karne nyingi majiji yamekuwa kani kuu katika kuongoza jamii ya kisasa kama tuijuavyo na yametuathiri sisi sote.

Tofauti na Bado Yenye Kufanana

The New Encyclopædia Britannica chasema kwamba “makazi ya kudumu ya mwanadamu ya mapema zaidi yapatikana katika nyanda zenye rutuba zilizo karibu na tropiki za mito Naili, Tigris, Frati, Indus, na Yellow.” Bila shaka, yale majiji yaliyotangulia majiji ya karne ya 20 yalikuwa tofauti sana na yale ya kisasa ya kando ya mito.

Katika karne zilizopita watu wengi zaidi waliishi katika maeneo ya mashambani. Kwa kielelezo, jiji kuu pekee katika Uingereza katika mwaka 1300, lilikuwa London, na idadi ya watu walo iliyo chini ya elfu 40 ilikuwa chini sana ya asilimia 1 ya jumla ya idadi ya watu wa nchi hiyo. Kufikia 1650 karibu asilimia 7 ya Waingereza wote waliishi London. Kufikia mwanzo wa karne ya 19, jiji hilo lilikaribia kuwa na watu milioni moja. Leo, wakazi wa Uingereza wanaopungua asilimia 9 huishi katika maeneo ya mashambani. Wengine wote husongamana majijini, karibu milioni saba katika jiji kuu la London na viunga vyalo pekee.

Ili kuonyesha kadiri ambayo majiji yamekua na kuongezeka, katika 1900, London lilikuwa jiji pekee ulimwenguni pote lenye idadi ya watu milioni moja. Sasa kuna majiji zaidi ya 200 yenye wakazi zaidi ya milioni moja. Wanajiografia husema juu ya sehemu zenye idadi kubwa sana ya watu, kukiwa msururu wa majiji yaliyoungana kama ule upatikanao katika sehemu ya Ruhr katika Ujerumani, ambako eneo lililo kando-kando ya Mto Ruhr, kutoka Duisburg hadi Dortmund, hufanyiza jumuiya moja kubwa.

Kujapokuwa tofauti mbalimbali, majiji ya kale na ya kisasa yashiriki jambo moja—matatizo. Na matatizo hayajapata kuwa mengi sana au makubwa sana kama yalivyo leo. Majiji yamo katika taabu kubwa. Ikiwa ‘kujijengea wenyewe jiji’ kumefundisha ainabinadamu jambo lolote, angalau kungetufundisha kwamba, chini ya hali zisizo kamilifu na kama kufanywavyo na wanadamu wenye kukosea, kujenga majiji si njia ifaayo ya kutosheleza mahitaji yetu.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki