Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g94 1/8 kur. 22-23
  • Mahakama Kuu Zaidi ya Ufilipino Yatetea Uhuru wa Ibada

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Mahakama Kuu Zaidi ya Ufilipino Yatetea Uhuru wa Ibada
  • Amkeni!—1994
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Sababu Inayofanya Mashahidi wa Yehova Wasiisalimu Bendera
  • Sababu za Uamuzi wa Mahakama Kuu Zaidi
  • Maana ya Wapendao Uhuru
  • Sikukuu na Maadhimisho
    Shule na Mashahidi wa Yehova
  • “Wokovu Una Bwana”
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2002
  • Maswali Kutoka kwa Wasomaji
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1977
  • Kanuni za Adili Zinazostahili Staha
    Mashahidi wa Yehova na Elimu
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1994
g94 1/8 kur. 22-23

Mahakama Kuu Zaidi ya Ufilipino Yatetea Uhuru wa Ibada

Na mleta habari za Amkeni! katika Ufilipino

MNAMO Juni 7, 1993, mamilioni ya watoto wa shule Wafilipino waliporudi kwenye madarasa yao, Mashahidi wa Yehova miongoni mwao ndio waliokuwa wenye furaha zaidi. Kwa nini? Kwa sababu mnamo Machi 1, 1993, kabla tu ya kufungwa kwa mwaka wa shule uliotangulia, Mahakama Kuu Zaidi ya Ufilipino ilibadili uamuzi wa Mahakama Kuu Zaidi wa 1959 na kutetea haki ya watoto wa Mashahidi wa Yehova wasiisalimu bendera, wasikariri kiapo cha uaminifu, na kuimba wimbo wa taifa.

Ni nini kilichoongoza kwenye hali hiyo iliyobadilika? Na kuna matokeo gani kwa wote wapendao uhuru katika Ufilipino kama tokeo la uamuzi huo?

Sababu Inayofanya Mashahidi wa Yehova Wasiisalimu Bendera

Mashahidi wa Yehova huamini kwamba kuisalimu bendera, kuimba wimbo wa taifa, na kukariri kiapo cha uaminifu ni matendo ya kidini. Dhamiri yao iliyozoezwa na Biblia haiwaruhusu kushiriki katika matendo kama hayo ya ibada. (Mathayo 4:10; Matendo 5:29) Haidhuru wao waishi katika nchi gani, huo ndio msimamo wao katika kumwiga Yesu Kristo, aliyesema kwamba wafuasi wake ‘hawangekuwa sehemu ya ulimwengu, kama vile yeye asivyo sehemu ya ulimwengu.’—Yohana 17:16.

Wakati uo huo, Mashahidi wa Yehova huonyesha staha kwa serikali wanazoishi chini yazo, na wanaamini kwamba hizo ni mpango ambao Mungu ameruhusu. Hivyo, wako chini ya jukumu la kutii sheria za nchi, kulipa kodi, na kutoa heshima ifaayo kwa maofisa wasimamizi. Wao hawawezi kushiriki wakati wowote katika uasi wowote dhidi ya serikali yoyote.a

Sababu za Uamuzi wa Mahakama Kuu Zaidi

Ni sababu zipi zilizotolewa na Mahakama Kuu ya sasa za kubadili uamuzi wa 1959 wa Gerona v. Secretary of Education? Uamuzi wa 1993 ulioandikwa na Hakimu Griño-Aquino ulisema: “Wazo la kwamba mtu aweza kushurutishwa kusalimu bendera, kuimba wimbo wa taifa, na kukariri kiapo cha uaminifu, wakati wa sherehe ya bendera au sivyo aadhibiwe kwa kufukuzwa kazini au shuleni, halipatani na dhamiri ya kizazi cha sasa cha Wafilipino ambao mawazo yacho yaliundwa na Haki za Kibinadamu zinazowahakikishia haki zao za usemi na za kufuatia dini na ibada kwa uhuru.”

Mahakama hiyo ilionelea kwamba ingawa Mashahidi wa Yehova “hawashiriki katika sherehe ya bendera iliyo ya lazima, wao hawashiriki katika ‘matendo yanayoweza kuonwa na wengine’ au tabia inayoweza kuwakosea wananchi wenzao wanaoamini katika kuonyesha upendo wao wa nchi kwa kufanya sherehe ya bendera.” Mahakama hiyo ilionelea zaidi hivi: “Wao husimama wima wakiwa kimya wakati wa sherehe ya bendera ili kuonyesha staha yao kwa ajili ya haki ya wale wanaochagua kushiriki katika sherehe hizo. . . . Kwa kuwa hawashiriki katika tabia yenye kuondoa amani, hakuna sababu yoyote ya kuwafukuza.”

Mahakama ya sasa pia ilishughulikia utabiri uliofanywa na uamuzi wa Gerona kwamba ikiwa Mashahidi wa Yehova wataruhusiwa wasishiriki katika takwa la kusalimu bendera, “sherehe ya bendera itasahauliwa au labda itafanywa kukiwa na washiriki wachache sana, na wakati utakuja ambapo tutakuwa na raia wasiofundishwa na wasiokaririwa na wasio na kicho kwa bendera, na upendo wa nchi, kupenda mashujaa wa kitaifa, na uzalendo—hali yenye kusikitisha, hata yenye msiba, na yote hayo kwa sababu sehemu ndogo ya idadi ya wote shuleni ilitaka nia yayo ifuatwe, ikadai na kukubaliwa isishiriki.”

Uamuzi wa Mahakama wa 1993 ulijibu hilo kwa kusema: “Ile hali mbaya ambayo Mahakama ilitabiri katika Gerona . . . haijatokea. Hatushawishwi kwamba kwa kuwaachilia Mashahidi wa Yehova wasiisalimu bendera, kuimba wimbo wa taifa na kukariri kiapo cha uzalendo, kikundi hiki cha kidini ambacho kwa wazi chafanyiza ‘sehemu ndogo ya idadi ya wote shuleni’ kutatokeza mvurugo katika sehemu yetu ya ulimwengu na kwa ghafula kutokeze taifa ‘lisilofundishwa na lisilokaririwa na lisilo na kicho kwa bendera, lisilo na uzalendo, upendo wa nchi na kuwapenda mashujaa wa taifa.’”

Hatimaye Mahakama ya sasa ilirejezea maelezo ya Bw. Justice Robert Jackson wa Mahakama Kuu Zaidi ya U.S. katika kesi ya 1943 ya Barnette ambayo alisema hivi: “Kuamini kwamba uzalendo hautasitawi ikiwa sherehe za kizalendo ni za hiari na za kujitolea badala ya utaratibu wa kulazimishwa ni kufanya kadirio lisilofaa juu ya upendelevu wa mambo tuzoeayo kwa akili zilizofunguka. . . . Uhuru wa kutofautiana hautumiki tu katika mambo madogo. Huo ungekuwa uhuru usio mkamilifu. Hali halisi ya uhuru huthibitishwa na haki ya kutofautiana kwa habari ya mambo yanayougusa moyo wa jamii iliyoko.”

Baada ya kutajwa kwa mambo hayo ya sheria yafaayo, uamuzi wa wote wa Mahakama ya Ufilipino ulikuwa: “Amri za kufukuza zilizotolewa na washtakiwa [waliokata rufani] dhidi ya washtaki [waliopinga rufani] ZIMEBATILISHWA NA HAZITUMIKI. Amri ya muda ya kuzuia [wenye mamlaka wa shule] iliyotolewa na Mahakama hii inafanywa iwe ya kudumu.”

Hakimu-Mshirika Isagani Cruz katika maoni ya kuunga mkono aliongeza maoneleo haya: “Kwa maoni yangu ya unyenyekevu, Gerona ilikuwa na msingi wa dhana yenye kosa. Yaonekana Mahakama ile iliyopitisha uamuzi huo ilitenda chini ya usadikisho kwamba Taifa lina haki ya kuamua yale yaliyo ya kidini na yale yasiyo ya kidini na kumwamrisha mtu kile ambacho angeweza na kile ambacho hangeweza kuabudu. . . . Katika kuwataka washtakiwa walio hapa washiriki katika sherehe ya bendera, Taifa limejulisha ex cathedra [kimamlaka] kwamba hawaendi kinyume cha Biblia kwa kusalimu bendera. Kwangu mimi huku ni kuingilia bila idhini itikadi zao za kidini zinazowaambia mambo yaliyo kinyume. Taifa haliwezi kuwafasilia Biblia. Hilo halina uwezo katika jambo hilo.”

Maana ya Wapendao Uhuru

Wote wapendao uhuru kwa kweli waonea shangwe uamuzi huo wa kutetea haki ya hiari ya kuchagua katika jambo la dini na kulingana na miongozo ya dhamiri ya mtu, na wakati uo huo kujitiisha chini ya mamlaka ya kadiri ya Taifa. (Warumi 13:1, 2) Katika kulinda haki za mtu mmoja-mmoja, Taifa halitokezi hali ya ukosefu wa kufuata sheria, ila latumikia jukumu lililotajwa na mtume Paulo kwenye Warumi 13:5, 6, ambapo asema: “Kwa hiyo ni lazima kutii, . . . kwa sababu ya dhamiri. Kwa sababu hiyo tena mwalipa kodi; kwa kuwa wao ni wahudumu wa Mungu, wakidumu katika kazi iyo hiyo.”

Mashahidi wa Yehova katika Ufilipino waheshimu mamlaka ya mahakimu wa Mahakama Kuu Zaidi na wang’amua kwamba sifa ya mwisho lazima ipewe kwa Muumba wetu, Yehova Mungu.

[Maelezo ya Chini]

a Kwa mazungumzo marefu juu ya sababu Mashahidi wa Yehova hawashiriki katika kuisalimu bendera, kuimba nyimbo za taifa, na kufanya kiapo cha uaminifu, tafadhali ona broshua Shule na Mashahidi wa Yehova, Kiingereza, iliyotangazwa na Watchtower Bible and Tract Society of New York, Inc., kurasa 12-16.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki