Maswali Kutoka kwa Wasomaji
● Je! Mkristo aweza kupandisha au kushusha bendera kazini?
Ikiwa mgawo huo wa kazi si sehemu ya sherehe ya bendera, Mkristo aweza kujiamulia atakalofanya, akifikiria hali za kwao na dhamiri yake.
Inajulikana sana kwamba watu wengi wanaona bendera ya taifa lao yapaswa kuheshimiwa sana. The Encyclopedia Americana chasema: “Bendera, kama msalaba, ni takatifu. . . . Wanadamu wanatumia sheria na kanuni zenye maneno makali kuhusu bendera za mataifa, kama ‘Utumishi kwa Bendera,’ . . . ‘Bendera Iheshimiwe Sana,’ ‘Kujitoa kwa ajili ya Bendera.’” Mara nyingi kunakuwa na sherehe za pekee, nao watu ‘wanajitoa’ kwa njia ya pekee kwa ajili ya bendera.
Kila mtu yu huru kuamua kama atashiriki katika sherehe hizo. Hata hivyo, Mashahidi wa Yehova wanasadiki kwamba, yanayosemwa na Biblia juu ya kujiepusha kutumikia vitu vionekanavyo visivyo na uhai, yanapaswa kufikiriwa. (Kut. 20:4, 5; 1 Yohana 5:21) Kwa hiyo, ingawa Mashahidi wa Yehova wanaheshimu haki za wengine za kufanya watakavyo, wao hawashiriki katika sherehe za bendera. Hata hivyo, wao ni raia wanaowekea wengine mfano mwema kwa kuunga mkono sheria za nchi kila siku.—Rum. 13:1.
Mara nyingi bendera ya taifa huwekwa katika majengo ya shughuli za watu wote na mahali pa watu kukutania, kama katika nyumba za wazima moto, afisi za baraza ya mji na shuleni. Kwa sababu Mashahidi wa Yehova wanaheshimu serikali pamoja na vitu vinavyotumiwa kuiwakilisha, hawakatai kuingia au kufanya kazi katika majengo ambamo bendera ya taifa imewekwa. Vivyo hivyo, huenda bendera ikawa katika stampu, katika mabati yanayoonyesha namba ya motokaa au katika vitu vingine vinavyotengenezwa na serikali. Lakini hiyo haimaanishi mtu wa serikali anayetumia vitu vya namna hiyo bila shaka anashiriki katika matendo ya kutumikia bendera. Jambo la maana si kuwapo kwa bendera, bali jinsi mtu anavyotenda.
Nyakati nyingine mfanya kazi katika jengo la serikali hupewa kazi ya kupandisha bendera asubuhi na kuishusha mwishoni mwa siku. Huenda hiyo ikawa sehemu ya sherehe ya pekee, na huenda watu wakawa wakati huo wanasimama wima kabisa au wanaisalimu bendera. Inapokuwa hivyo, mtu asiyeshiriki katika sherehe za kusalimu bendera angekuwa na sababu za dhamiri za kutopandisha wala kushusha bendera, kwa maana kufanya hivyo kungekuwa ni kushiriki katika sherehe hiyo. Kungekuwa ni kuunga mkono sherehe hiyo, kama vile ambavyo wana-muziki wanaweza kutazamiwa kuunga mkono sherehe hiyo kwa muziki wa kutukuza nchi yao.
Lakini, mara nyingi hakuwi na sherehe wakati wa kupandisha au kushusha bendera kila siku katika jengo la serikali. Kwa mfano, huenda ikapandishwa ili kutayarisha jumba litumiwe, kama vile kufungua milango ya jengo hilo, kufungua madirisha, na kadhalika. Inapokuwa hivyo bendera inachukuliwa kama mfano unaowakilisha serikali yenye nchi ambamo jengo limejengwa.
Inapokuwa hivyo, mfanya kazi Mkristo anayeagizwa kufanya kazi hiyo pamoja na nyingine yu huru kuamua atakalofanya. Huenda mtu mmoja akaongozwa na dhamiri yake kumwomba msimamizi wake aagize mfanya kazi mwingine aipandishe na kuishusha bendera. Lakini huenda Mkristo mwingine akaona dhamiri yake itamruhusu ashughulike na bendera maadamu hakuna sherehe. Kila mtu anayeagizwa kufanya hivyo kazini pake apaswa kufikiria hali za kwao na vilevile vionyo vya dhamiri yake iliyozoezwa na Biblia. Halafu atafanya uamuzi utakaomwacha akiwa na dhamiri safi.—1 Pet. 3:16.