Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g94 3/8 uku. 31
  • “Kazi Nzuri!”

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • “Kazi Nzuri!”
  • Amkeni!—1994
  • Habari Zinazolingana
  • Kushangilia Katika Yehova Kujapokuwa Majaribu
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1999
  • Kujenga Pamoja Duniani Pote
    Mashahidi wa Yehova—Wapiga-Mbiu wa Ufalme wa Mungu
  • Mashahidi wa Yehova—Ripoti ya Kitabu-Mwaka 1994
    1994 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
  • Uharibifu wa Ghafula!—Wamekabilianaje?
    Amkeni!—1990
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1994
g94 3/8 uku. 31

“Kazi Nzuri!”

NDIVYO kilivyosema kichwa kimoja katika gazeti St. Helena News.[1] Mashahidi wa Yehova walikuwa wamefaulu tena. Walikuwa wamejenga Jumba la Ufalme la pili katika kile kisiwa kidogo cha St. Helena, zaidi ya kilometa 1,600 magharibi ya Afrika.[2] Jengo hilo liko kwenye uwanja ulioinuka katika eneo liitwalo Bonyeo la Nusu-Mti, mahali penye mtazamo mzuri ajabu wa Bahari Kuu ya Atlantiki.

Mkaguzi wa ujenzi na mkuu wa wazima-moto aliwapongeza Mashahidi. “Mmefanya maajabu,” akasema gavana mmoja aliyestaafu.[3] “Hiki ni kielelezo kizuri ajabu!” mkaguzi wa nguvu za umeme akaongezea.[5]

Siku ya wakfu iliwekwa iwe Jumamosi, Januari 9, 1993. Kwa kufanya matangazo katika radio, kisiwa kizima cha watu wapatao 6,000[7] kilialikwa kuhudhuria. Lakini je! kikundi kidogo hicho cha Mashahidi wa hapo, ambao ni karibu 150, kingeweza kukamilisha mradi huo kwa wakati? Sarel Hart, mwangalizi asafiriye wa Afrika Kusini, aeleza hivi: “Hangaiko lilijaa mioyoni mwetu wakati ambapo katika alasiri ya tarehe nane, njia ya kupitia magari ilikuwa bado ikihitaji kokoto nyingi ya kuitandaza.” Wangeweza kupataje malori, vifaa, na kokoto ya kujazia ili kuitandaza ardhi muda ukiwa umekwisha sana hivyo? Hart aendelea kusema: “Sala za kimyakimya zilisikiwa na Yehova. Yule mwanakandarasi aliyetoa kokoto ya kujazia aliwaambia ndugu hivi: ‘Mliomba magari matano yaliyojazwa. Mimi najua mwahitaji zaidi. Nimeacha kuhesabu—nyinyi acheni tu malori yaendelee kujazwa hadi mpate ya kutosha.’ Ilikuwa saa 10:00 alasiri wakati mwendeshaji wa tingatinga la uchotaji alipopita hapo akielekea nyumbani. Mmoja wa Mashahidi alimsimamisha akamweleza tatizo letu. ‘Nyinyi toeni tu malipo yangu ya kazi ya ziada mwone mambo,’ akasema, naye akaingiza tingatinga yake humo njiani akautandaza udongo mara tu ukiisha kumwagwa na yale malori. Katika muda wa saa tatu ile njia isiyo laini ya kwenda kwenye Jumba la Ufalme ikatandazika kwa ulaini.

Kesho yake jumla ya watu 328—zaidi ya asilimia 5 ya wakaaji wa kisiwa hicho—walihudhuria hotuba ya wakfu. Kati ya wasikilizaji walikuwako pia katibu wa serikali na mmoja wa washauri, na pia askofu Mwanglikana alipeleka ujumbe wa kuwatakia mema.

[Ramani katika ukurasa wa 31]

(Ona mpangilio kamili katika nakala iliyochapishwa)

Afrika

St. Helena

[Picha katika ukurasa wa 31]

Jumba la Ufalme Jipya

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki