Kutoka kwa Wasomaji Wetu
Sikukuu Nilipomaliza kusoma ule mfululizo “Sikukuu—Sababu Inayofanya Watoto Fulani Wasizisherehekee” katika Amkeni! la Novemba 22, 1993, nilijikuta nikitiririkwa na machozi ya shangwe kwenye uso wangu. Mimi nililelewa nikiwa mmoja wa Mashahidi wa Yehova na nilikuwa na hisia zilezile kama wengi wa watoto walionukuliwa. Nilitaka kupongeza wachanga wetu kwa kuwa vielelezo vizuri jinsi hiyo! Nikiwa mzazi, natiwa moyo kujua kwamba watoto wengi wataka kumpendeza Yehova wakiwa na umri mdogo hivyo.
T. K., United States
Mimi nina miaka tisa, na sikujua kamwe kwamba Halowini ni sikukuu mbaya na ya kuchukiza jinsi hiyo. Sihisi kwamba ninakosa faida yoyote.
A. C., United States
Nilipokuwa mtoto, nilikuwa nikitazamia sana Krismasi na Ista. Lakini sasa naelewa kwamba hiyo ni misherehekeo ya kipagani na kwamba ingekuwa kazi-bure kufuata mapokeo tu. Maelezo yaliyotolewa yalikuwa kamili na yenye habari nyingi.
S. L. P., Ujerumani
Mimi nililelewa nikiwa Shahidi tangu nilipokuwa na miaka 6, na sasa nimo mwanzoni mwa miaka yangu ya 30. Watu wengi walifikiri kwamba ndugu yangu, dada zangu, na mimi tulinyimwa raha. Nikawaeleza kwamba sisi tulipokea zawadi muda wote mwakani na kwamba wazazi wetu walitupa wakati wao na nafasi zao wenyewe kwa hiari nyingi. Tulifanya mambo mengi pamoja. Baba yangu alikuwa pia mwaminifu katika kufanya funzo la Biblia la familia yetu kila juma. Hiyo ilikuwa ndiyo zawadi bora zaidi ya kiroho! Mimi sikuudhika kamwe kutoadhimisha zile sikukuu.
D. Y., United States
Mimi nina miaka 14 nami naweza kukubaliana na yaliyosemwa. Nilitiwa nguvu kujua kwamba vijana wengine wanachukua msimamo upande wa ile kweli.
C. A., United States
Mimi sihisi nakosa kitu chochote kwa kutoadhimisha sikukuu. Familia yetu hunipa mimi zawadi na kunipa fedha kadiri nizihitajivyo. Nina baadhi ya vitu vya kuchezea ambavyo watoto wengine wa umri wangu [12] hufurahia.
L. C., United States
Makala hiyo ilikuwa jibu kwa sala nyingi. Ni vigumu kuelewa kikweli shangwe na hofu za kulea mtoto mpaka uonapo kisichana kilichojawa na machozi kikikukodolea macho kana kwamba kikuulize ni kwa nini mtu fulani alikifanyia mzaha. Binti yetu alianza shule ya watoto wachanga sana mwaka huu, na ingawa tulitafuta habari juu ya sikukuu, bado ilikuwa vigumu kwake. Tulisali kila usiku ili awe imara na mwenye moyo mkuu shuleni. Halafu zile makala za Amkeni! zikaja. Yeye aweza kusoma mambo ya kiwango cha darasa la saba, kwa hiyo langu lilikuwa kumpa tu gazeti hilo alisome. Akawa mwenye moyo mkuu alipokuwa akisoma maelezo ya watoto wengine na kuona picha zao. Siku ileile iliyofuata aliangushia mwalimu wake nakala moja.
G. M., United States
Baadhi ya watoto shuleni walikuwa wakinifanyia mzaha wa uchokozi kwa sababu sikuadhimisha zile sikukuu, kwa hiyo nikafanya nakala za lile gazeti nikawapa baadhi yazo. Nina hakika ule mzaha wa uchokozi utakoma kwa sababu sasa wao wajua kwamba sinyimwi raha yoyote.
K. H., United States
Safari ya Basi Wakati ninapohisi nimekosa uchangamfu, nyakati fulani mimi hushona na kusikiliza kaseti zangu za Amkeni! Nilistaajabu kwelikweli juu ya jinsi ile makala “Safari ya Basi ya Kwenda Katikati ya Australia” ilivyonichangamsha. (Juni 8, 1993) Ilionekana ni kama mimi nilikuwa huko, nikishiriki zile shangwe na furaha nyingi ambayo wasafiri hao walikuwa wakipata. Asante sana sana.
A. W., United States