Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g94 5/22 kur. 25-26
  • Ingiza Ucheshi Katika Maisha Yako

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Ingiza Ucheshi Katika Maisha Yako
  • Amkeni!—1994
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Kucheka au Kutocheka
  • Ucheshi na Afya Yako
  • Ndani ya Familia
  • Kukabili Ugonjwa kwa Ucheshi
    Amkeni!—2005
  • Tiba ya Akili na Mwili
    Amkeni!—1993
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
    Amkeni!—1995
  • Je, Macho Yako Yana Madoa?
    Amkeni!—2000
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1994
g94 5/22 kur. 25-26

Ingiza Ucheshi Katika Maisha Yako

Ilikuwa siku moja ya majira yenye baridi nyingi, na ngazi zilikuwa zimefunikwa na barafu. Wa kwanza kujaribu kushuka karibu aanguke. Aliyefuata alitangaza hivi: “Mambo hufanywa jinsi hii!” Punde tu baada ya maneno hayo kumtoka kinywani, ndiye huyo chini—katandazika chini barabara kwa mgongo wake. Kukawa na kimya cha kugutuka kwa muda, kisha vicheko vikaanguliwa na wasimama-kando walipoona kwamba hakuumia.[1a]

KUNA “wakati wa kucheka.” Ndivyo alivyoona Sulemani mwanamume mwenye hekima karibu miaka elfu tatu iliyopita. (Mhubiri 3:4) Hiyo ni kweli hata leo. Uwezo wa kucheka ni tabia ya kupewa na Mungu, zawadi kutoka kwa Yule aelezwaye katika Biblia kuwa “Mungu mwenye furaha.”—1 Timotheo 1:11, NW.

Basi, haishangazi kwamba uumbaji umejawa na vitu vyenye ucheshi—watoto wa paka na wa mbwa wenye vichekesho vya upuuzi, mwana-simba akitafuna mkia wa mama yake mpaka anafyatwa kwa mkia huo, watoto wa nyani wakifukuzana na kuangukiana kwa kupita katika matawi. Ucheshi umetuzunguka kotekote, ukingojea kuonwa na kuthaminiwa.

Hiyo si kusema kwamba watu wote huchekea mambo yaleyale. Bali, mara nyingi kichekesho hutegemea utamaduni wa mtu, utu, malezi, na hali ya moyo, na mambo mengine pia. Ingawa hivyo, karibu kila mtu atachekeshwa na kitu fulani—hadithi ya kuchekesha, furahisho ambalo hakutarajia, mzaha, mgongano wa lugha ulioundwa kwa ustadi.

Ucheshi hutimiza kusudi gani? Angalau huo ni njia ya kuwa na uhusiano mzuri zaidi na wengine. Elezo moja liliita kicheko “mwendo ulio mfupi zaidi kati ya watu wawili.”[3] Kwa kweli, watu fulani huamini kwamba ucheshi waweza kutumiwa kama kipimo cha upatano wa ndoa. Uchunguzi mmoja juu ya ucheshi ulipata kwamba wenzi ambao hukubaliana juu ya mambo yaliyo ya kuchekesha huelekea zaidi kupendezwa mtu na mwenzake, kupendana, na kutaka kuoana kuliko wale ambao mapendezi yao ya ucheshi hayafanani sana. Kwa nini? Kwa sababu ucheshi ni kionyeshi cha mambo mengi: viwango, mapendezi, mashughulikio, uelewevu, uwazio, na mahitaji.[4] Uchunguzi mmoja wa 1985 wa mashirika elfu moja ya Marekani ulifunua kwamba “watu wenye hali ya ucheshi huelekea kuwa wabuni zaidi, wasioshikilia kauli kwa ukakamavu sana na wenye nia nyingi zaidi ya kufikiria na kukubali mawazo na mbinu mpya.”[5]

Kucheka au Kutocheka

Kwa kweli hakuna ajuaye ni nini hasa hufanya kitu fulani kichekeshe. Watu fulani huamini kwamba kiini cha ucheshi ni kusawazisha hali ya kukosa upatani—kule kuleta pamoja vitu viwili vinavyoonekana kuwa visivyopatana.[6] Mtu mzima aliyevalia kama mfanya-upuuzi wa kuchekesha katika sarakasi huenda akamtia mtoto mdogo katika kishindo cha kicheko. Hata hivyo, mtu mzima ambaye amejionea mengi zaidi maishani na mwenye ustadi bora wa kutambua mambo huenda asizione tena mbinu hizo za kipuuzi kuwa za kuchekesha. Huenda akaona raha katika namna za ucheshi wa kutumia akili zaidi—ufundi wa kugonganisha maneno yenye maana mbili, mbinu ya kucheza na lugha, au mizaha—ambayo husawazisha hali za kukosa upatani kwa ucheshi wa kutumia maneno, badala ya kutumia mwili.

Watafiti fulani huamini kwamba huenda ucheshi ukatokana na kufunguliwa kwa nishati za hisiamoyo zilizokazika ndani. Huenda ucheshi ukatumika kuficha wasiwasi na maumivu. “Hata wakati wa kucheka moyo huwa na huzuni; na mwisho wa furaha ni uzito wa moyo.”—Mithali 14:13.

Namna nyingi za ucheshi zatia ndani kile kiitwacho kicheko cha kubandika tu. Mtu ajikwaa au amwagikiwa na maji. Hiyo yachekesha, sivyo? Labda ndivyo, ikiwa hakuna mwenye kuumia kikweli.

Mkristo hujiangalia sana asisitawishe hamu ya ucheshi usiofaa au wa kufurahia kuteseka kwa watu. Ingawaje, upendo “haufurahii udhalimu.” (1 Wakorintho 13:6) Pia Mkristo huepuka mizaha ya kuudhi iliyo na madharau kwa taifa au jamii yoyote. Yeye husawazisha hali yake ya ucheshi na “huruma.” (1 Petro 3:8, Zaire Swahili Bible) Kwa kielelezo, huenda ikawa yafurahisha kutazama kitoto kikitembea de-de-de kwa hatua za kukisia kisha kuanguka pu. Lakini mtu mzee-mzee au asiyejiweza akianguka, itikio lifaalo ni kufanya haraka kwenda kumsaidia, si kucheka.

Ucheshi na Afya Yako

Ucheshi utumiwapo ifaavyo una thamani nyingi. Kwa kweli, uthibitisho unaendelea kuongezeka polepole kuonyesha kwamba kicheko huenda hata kikatumika kama dawa.[10] Yajulikana kwamba kitendo cha kucheka hukanda viungo vya ndani vya mtu kwa njia yenye afya. [11] Zaidi ya hilo, kulingana na gazeti American Health, “watafiti [fulani] hufikiri kicheko chaweza kuutia nguvu mfumo wa kinga za mwili.” Halafu gazeti hilo lanukuu mtaalamu wa kinga za mwili Lee S. Berk kuwa akisema: “Hisiamoyo zisizofaa zaweza kuuongoza vibaya mfumo wa kinga za mwili, na sasa yaonekana zile zifaazo zaweza kufanya jambo kama hilo.”[12] Hiyo yakazia hekima ya maneno ya Biblia: “Moyo uliochangamka ni dawa nzuri.”—Mithali 17:22.

Kwa matumaini ya kuitumia nguvu ya kuponya ya ucheshi, hospitali fulani zimeanzisha vile viitwavyo vyumba vya kuchekea ambamo wagonjwa waweza kucheza michezo, kutazama sinema za kuchekesha, kusikiliza mizaha, au kutembelewa tu na watu wa ukoo katika hali yenye uchangamshi zaidi.[13] Je! wewe mwenyewe waweza kutokeza ucheshi? Tuseme una rafiki au mtu wa ukoo aliye mgonjwa hospitalini. Kwa nini usimchangamshe kwa kumpa kitabu chenye ucheshi au kadi ya kuchekesha ambayo ingekuwa yenye kufaa?[14]

Pia kicheko chaweza kupunguza hasira. Dakt. R. B. Williams Jr., asema hivi: “Kuwa na hasira ni jambo baya kwa afya yako.”[16] Vivyohivyo, Biblia husema: “Moyo ulio mzima ni uhai wa mwili; bali husuda ni ubovu wa mifupa.” (Mithali 14:30) Dakt. Williams asema hivi: “Ni vigumu kukaa umekasirika unapocheka.”[17] Ndiyo, kuuona ucheshi ulio katika hali fulani ni mojapo njia zenye kujenga zaidi za kushughulika na hasira.

Ndani ya Familia

Ucheshi waweza kutumiwa nyumbani.[17a] Mume mmoja alisema hivi: “Huo ni wenye mafaa kwangu kama vile chombo cha matumizi mengi kilivyo kwa fundi wa magari kwa sababu huo hufanya mambo mengi sana. Hulinda, hutia moyo, huanzisha mazungumzo yenye matokeo mazuri, hubomoa dhana mbaya zilizotangulia kutungwa mapema, na hugeuza maneno yenye kuanzisha matata yawe ya kiasi na ya ufikirio.”[18]

Hali ya ucheshi husaidia hasa wakati tabia za kuudhi zitishapo kuvuruga mahusiano. Mwana wako asahau kuondoa vichezeo vyake ujapomwonyaonya kwa upole afanye hivyo. Mume wako aacha nguo zake chafu juu ya sakafu ya bafu. Mke wako aunguza chakula cha jioni. Kutafuta makosa, kuaibisha, kulaumu, kupiga mayowe, au kupiga makelele huzidi tu kuharibu mambo. Mtafiti mmoja wa afya, aliyenukuliwa katika gazeti Redbook, aliona hivi: “Ukikabiliana na mtu kwa pambano au kumdhihaki, atajitetea. Ucheshi huvuta watu watazame mwenendo wao kwa mbali—na kuubadili.”[19]

Hiyo haimaanishi kumcheka mtu aliye na hatia ya kile kitendo cha kukosa utambuzi. Kwa kawaida hiyo huleta maumivu, si kicheko. Jaribu kuelekeza ucheshi wako kwenye hali yenyewe. Kuwa na kicheko kizuri kwaweza kusaidia sana kupunguza wasiwasi. Asema hivi mke mmoja: “Kuna nyakati ambazo mume wangu huona nikiwa karibu kukasirika, naye hupoesha mambo kwa neno au tendo la ucheshi. Mimi kuja kushtuka, najikuta nikicheka. Halafu mimi hung’amua kwamba kumbe jambo lile halikuwa zito sana.”[20]

Ingawa hivyo, hapa pana tahadhari kidogo. Epuka kujaribu kuchekesha wakati hali itakapo uzito au sikitikio. Angalia Mithali 25:20: “Amwimbiaye nyimbo mtu mwenye moyo mzito, ni kama yeye avuaye nguo wakati wa baridi; ni kama siki juu ya magadi.” Ucheshi wapasa kutumiwa kwa utambuzi ufaao tu, usije ukadhuru kihisiamoyo au kimwili. Usiruhusu ucheshi kamwe uwe wa kishenzi wala wa kimadharau. Hiyo ingeondolea mbali kuruhusu watoto wenye umri mkubwa zaidi kuwafanyiafanyia wadogo wao mizaha ya daima. Uchokozi mwanana huenda ukafaa, lakini maelezo ya kuchokorachokora hayafai kabisa. Wenzi wa ndoa ni lazima pia wajitahidi kuzuia ucheshi usiruke mipaka, kutoutumia kama silaha ya uchambuzi au njia ya kufanya madharau.

Mshairi Langston Hughes aliandika hivi wakati mmoja: “Kama vile mvua ya kupendeza wakati wa kiangazi, ndivyo ucheshi huenda ukasafisha na kupoza ardhi, hewa, na wewe.”[21] Kwa kweli, ucheshi waweza kutimiza sehemu ya maana katika maisha zetu. Waweza kutuzuia tusijichukue kwa uzito mno. Waweza kutusaidia tubaki wachangamfu na wenye kustarehe. Waweza kulainisha mahusiano pamoja na wengine. Waweza kutusaidia kukabili shida kubwa. Waweza hata kuboresha afya yetu.

Kwa hiyo ingiza ucheshi katika maisha yako. Ugundue. Ukuze. Usitawishe. Bila shaka huo utafanya maajabu kwa ajili yako na wale walio karibu nawe!

[Picha katika ukurasa wa 26]

Ucheshi waweza kusaidia kulainisha vituko vya nyumbani

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki