Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g94 5/22 uku. 31
  • Damu Yenye Viini Vibaya Hupewa Wasioganda Damu

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Damu Yenye Viini Vibaya Hupewa Wasioganda Damu
  • Amkeni!—1994
  • Habari Zinazolingana
  • Uchunguzi wa “Damu Yenye Dosari” ya Kanada
    Amkeni!—1995
  • Zawadi ya Uhai au Busu la Kifo?
    Amkeni!—1991
  • Kuokoa Uhai kwa Damu—Jinsi Gani?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1991
  • Utiaji-damu Mishipani—Ni Salama Kadiri Gani?
    Damu Yaweza Kuokoaje Uhai Wako?
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1994
g94 5/22 uku. 31

Damu Yenye Viini Vibaya Hupewa Wasioganda Damu

DAMU imekuwa shughuli yenye kuingiza dola bilioni mbili kwa mwaka. Utafutaji wa faida kutokana nayo umetokeza msiba mkubwa sana katika Ufaransa. Damu yenye viini vibaya vya HIV ilisababisha vifo vya watu 250 wasioganda damu katika magonjwa yenye kuhusiana na UKIMWI, kukiwa na mamia zaidi wenye kuambukizwa.[1]—The Boston Globe, Oktoba 28, 1992, ukurasa 4.

“Upatano wa kugutusha” wa wanatiba wasiojali na wanabiashara wenye pupa ulisababisha vifo vya Wajerumani wasioganda damu wapatao 400, kukiwa na angalau 2,000 zaidi walioambukizwa na damu yenye viini vibaya vya HIV.[2]—Guardian Weekly, Agosti 22, 1993, ukurasa 7.

Kanada ilikuwa na kashfa yayo yenyewe kuhusu damu. Yakadiriwa kwamba zaidi ya Wakanada 700 wasioganda damu walitibiwa kwa damu iliyoambukizwa na viini vya HIV. Serikali ilionywa katika Julai 1984 kwamba Shirika la Msalaba Mwekundu lilikuwa likigawa damu yenye viini vibaya vya UKIMWI kwa Wakanada wasioganda damu, lakini vile vifanyizo vyenye damu ya viini vibaya havikuondolewa sokoni mpaka mwaka mmoja baadaye, Agosti 1985.[3]—The Globe and Mail, Julai 22, 1993, ukurasa A21, na The Medical Post, Machi 30, 1993, ukurasa 26.

Ripoti moja iliyotoka kwenye shirika la habari la Reuters kutoka Madrid, Hispania, Aprili 21, 1993, ilisema kwamba Hispania ingewalipa ridhaa watu 1,147 wasioganda damu ambao waliambukizwa na virusi ya UKIMWI kupitia mitio ya damu na plazima mishipani katika miaka ya 1980, kulingana na Wizara ya Afya. Zaidi ya watu 400 tayari wamepata UKIMWI wakafa.[4]—The New York Times, Aprili 22, 1993, ukurasa A13.

Kuelekea mwisho wa 1982, Vituo vya Kudhibiti Magonjwa vilianza kuonya Shirika la Kitaifa kwa Wasioganda Damu (NHF) juu ya hatari za kugandisha damu kwa kutumia kigandishi Namba 8—kutiwa mishipani kwa kigandishi hicho mara moja kungeweza kuwa ni jumliko la damu iliyotoka kwa wachangaji 20,000, na ni damu ya mchangaji mmoja tu yatosha kuingiza viini vibaya vya UKIMWI katika sindano.[5] Onyo kali zaidi lilitolewa katika Machi 1983,[6] lakini katika Mei mwaka huo, NHF lilipeleka taarifa ya habari yenye kichwa “NHF Lahimiza Kigandishi Kiendelee Kutumiwa.” Kufikia wakati huo hesabu ya vifo ilikuwa ikiongezeka, na maelfu walikuwa wangali wakihatarishwa. Kigandishi hicho hakikuhitajika kabisa ili wasioganda damu waendelee kuwa hai; kulikuwa na namna nyingine za tiba.[7] Maelfu ya maisha zingaliweza kuokolewa.[8] Kufikia 1985, mashirika ya dawa yalikuwa yamegundua kwamba kwa kupasha moto kigandishi hicho, kilifanywa salama.[9] Hata hivyo, akiba zilizoorodheshwa za kigandishi kisichopashwa moto zilikuwa bado zikipelekwa sokoni.—Dateline NBC, Desemba 14, 1993.

[Hisani ya Picha katika ukurasa wa 31]

CDC, Atlanta, Ga.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki