Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g94 8/8 kur. 19-21
  • Maradhi ya Kifumbo ya Guam

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Maradhi ya Kifumbo ya Guam
  • Amkeni!—1994
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Litiko na Bodigi Ni Nini?
  • Fumbo Laongezeka
  • Kujaribu Kulifumbua Fumbo
  • Mambo ya Kutarajia na Jinsi ya Kukabili
  • Imani Yangu Yaniimarisha—Kuishi na Ugonjwa wa ALS
    Amkeni!—2006
  • Yaliyomo
    Amkeni!—2006
  • Mambo Ambayo Watunzaji Waweza Kufanya
    Amkeni!—1998
  • Pigano Dhidi Ya Ugonjwa Na Kifo Je! Linashindwa?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1991
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1994
g94 8/8 kur. 19-21

Maradhi ya Kifumbo ya Guam

NA MLETA-HABARI ZA AMKENI! KATIKA GUAM

MWANAMKE huyo alishuku ana maradhi hayo. Na bado, maneno ya daktari yalimshtua sana. “Machunguzo yetu yote yaonekana kuhakikisha kwamba baba yako ana litiko na bodigi.” Mwanamke huyo alijua kwamba maradhi yote mawili huishia kifoni.[1]

Guam ndiyo yenye visa vingi zaidi ulimwenguni vya maradhi haya, mara nyingi kuliko Marekani.[3] Lakini maradhi haya yatakayoondoa uhai wa baba ya mwanamke huyu ni nini? Ni nini huyasababisha? Naye aweza kufanya nini kumvumilisha muda uliomsalia?

Litiko na Bodigi Ni Nini?

Litiko na bodigi ni magonjwa ya kuzorotesha mfumo wa misuli ya mishipa ya fahamu.[4] Litiko yajulikana katika ulimwengu wa tiba kuwa amyotrophic lateral sclerosis (ALS, kushupaa kwa tishu kwa kukosa lishe izifaazo), au maradhi ya Lou Gehrig. Yule mcheza-besiboli Lou Gehrig wa kikoa cha Mayankii wa New York alipokufa kwa ugonjwa huu 1941, ulikuja kujulikana kwa jina lake. Litiko ndilo jina litumiwalo hapa kwa ALS.[5]

ALS huathiri chembe za mishipa ya kuendesha mwili na neva zilizo katika uti wa mgongo. Misuli ya mikono, miguu, na koo hupooza polepole bila kuacha.[6] Hata hivyo, uwezo wa kuhisi, na pia uwezo wa kuzaa na kudhibiti mkojo na kinyesi, hufanya kazi vizuri kwa muda.[7] Kwa kweli, watoto kadhaa wamezaliwa na wazazi wenye ALS.[8] Mwanamke mmoja alizaa watoto sita wazima katika ile miaka 14 aliyokuwa na ALS kabla hajafa akiwa na miaka 43.[9] Hata hivyo, wakati wa hatua za baadaye za ALS, maambukizo ya njia ya mkojo, baridi ya mapafu, au kutopumua vya kutosha yataleta kifo.[10] ALS hutokea mara nyingi katika watu wazima wenye miaka kati ya 35 na 60.[11] Katika Guam mtu aliyekufa kijana zaidi alikuwa mwanamke wa miaka 19.[12]

Bodigi ndio mtajo utumiwao hapa kwa kufinyaa ubongo. Huitwa kichaa cha Parkinson (PD),[13] na huelezwa kuwa mchanganyiko wa dalili za maradhi ya Parkinson na maradhi ya Alzheimer.[12][14] Ama dalili za Parkinson (miendo ya polepole, ukakamavu wa misuli, mitetemo) ama mabadiliko ya kiakili (kupoteza kumbukumbu, kurukwa na mawazo, mabadiliko ya utu) huenda yakaanza kwanza. Nyakati fulani, dalili za maradhi yote mawili hutokea pamoja.[15][16] Katika hatua za baadaye, mgonjwa huwa na vidonda vya kulala sana kitandani, kutokwatokwa na mkojo na kinyesi, kusinyaa mifupa, mivunjiko ya mifupa, na kupungukiwa na damu na mwishowe hufa kwa maambukizo.[17]

Litiko na bodigi huonwa kuwa maradhi mawili. Hata hivyo, utafiti umefanya wengine waamini kwamba ni maradhi mamoja yaonyeshayo dalili tofauti.[18]

Fumbo Laongezeka

Kati ya maswali makubwa yanayofanyiwa utafiti kuna yafuatayo: (1) Kwa nini asilimia 98 ya wenye ALS na PD katika Visiwa vya Mariana ni wenyeji asilia wa Chamorro na wachache waliobaki ni Wafilipino waliokaa huko sana? (2) Kwa nini maeneo mengineyo yenye maradhi hayo ni yale tu ya longitudo ileile? (3) Kwa nini watu kadhaa katika Visiwa vya Mariana wawe na maradhi yote mawili ya ALS na PD, hali wagonjwa kwingineko wana maradhi mamojapo tu? (4) Alumini iliyokolea huingiaje mfumo wa mishipa mikuu ya fahamu ya watu hawa? (5) Kwa nini zinki chache hupatikana katika chembe za ubongo palipo na alumini nyingi?[19] Machunguzo ya mazingira katika maeneo ya magharibi mwa Pasifiki yenye visa vingi yalionyesha wingi wa alumini, manganisi, na chuma lakini uchache wa kalsiamu, magnesi, na zinki katika udongo na maji.[20]

Kujaribu Kulifumbua Fumbo

Kwa miaka mingi watafiti katika Guam, Japani, na Kanada wamejaribu kuyafumbua mambo ya hakika juu ya maradhi haya ya kifumbo.[21] Katika nadharia kadhaa zidokezwazo na vikoa hivi vya utafiti, visababishi tofauti hutajwa: kurithi kasoro fulani isiyo ya kawaida,[22] kuambukizwa virusi ya polepole,[23] na kuingiwa daima na vijisumu vya madini.[24]

Mjuzi mmoja wa dawa amedai kwamba hata uchache wa kufikia miligramu mbili hadi tatu za alumini katika chembe za ubongo waweza kuvuruga utendaji wa kawaida wa ubongo.[25] Mbali na udongo na maji, vitu vyenye alumini vimeongezwa kwenye hamira za unga, michanganyo ya keki na magole, unga wa kujiumusha, kiyunga kilichogandishwa, vikabili-asidi fulani, diodoranti, na dawa za kikundu. Zichangiazo ni karatasi za kufungia za alumini na masufuria pia, maana alumini hulika, hasa vyakula vya asidi au alkalini vipikiwapo katika vitu hivyo.[26]

Dakt. Kwang-Ming Chen, mjuzi wa mishipa ya fahamu na wa maradhi haya yaliyo haba, ataarifu: “Machunguzo mapana yaliyofanywa na Taasisi ya Kitaifa ya Maradhi ya Mishipa ya Fahamu na Uambukizaji na Pigo la Fahamu (NINCDS) muda wa miaka 30 iliyopita hayajalifumbua kabisa fumbo la visa vingi ajabu na kisababishi cha maradhi haya ya mfumo mkuu wa mishipa ya fahamu (CNS) yadhoofishayo na kutibika kwa shida kuliko mengine yajulikanayo na wanadamu.”[28] Hata hivyo, alionyesha kwamba vijisumu vya daima kutokana na vijipande vya madini vyaweza kuwa ndivyo huyasababisha kuliko kasoro ya kurithi au kuambukizwa na virusi polepole.[29] Bado utafiti unaendelea.[30] Hadi jawabu lipatikane, hakuna la kufanya ila kujaribu kukabiliana na matatizo hayo na kuwasaidia wagonjwa kadiri iwezekanavyo.

Mambo ya Kutarajia na Jinsi ya Kukabili

Ingawa familia zilizohojiwa Guam ziliogopa sana na kuhuzunika zilipoujua ugonjwa, zilisema mtazamo wazo ulikuwa wa kuikubali hali.[31] Zilijua hakuna dawa.[32]

Mvurugiko mkubwa wa hisia na mtamauko hupata mgonjwa na familia yake pia.[33] Alipoulizwa ni nini kilichomsononesha zaidi, mgonjwa mmoja wa PD alisema: “Kutoweza kusema wazi na kutembea-tembea nyumbani hunivuruga hisia.”[34] Mabadiliko ya utu na kupoteza kumbukumbu hutatiza familia kukabili hali.[35] Vidonda vitokanavyo na kulala sana kitandani na kutokwa-tokwa na mkojo na kinyesi hutatiza zaidi utunzaji.[36] Kwa sababu mgonjwa wa ALS yuko chonjo akilini, kwa ujumla mtazamo wake huwa wa ushirikiano zaidi, lakini yeye huwa hoi katika hatua za baadaye za maradhi hayo.[37]

Mara nyingi bomba la kuvuta kohozi huhitajiwa kusafisha koo la mgonjwa wa ALS au PD.[38] Lazima chakula kiwe chororo, na lazima vijiko vyenye chakula viingizwe ndani sana kooni kuzuia kukabwa koo.[39] Oksijeni huhitajiwa kuwapo na shida ya kupumua.[40]

Matibabu ya kuzoeza mwili, kudhibiti ambukizo, na kutegemezwa kihisiamoyo huandaliwa yote na Shirika la Huduma ya Utunzaji wa Nyumbani.[41] Kati ya mahitaji mengineyo, Shirika la Guam la Litiko na Bodigi huandaa mikanda, mikongojo, vitanda vya mpandisho na mshusho na magodoro, viti-magurudumu, na vinyeo vya kitandani. [42] Tangu 1970, wagonjwa wa PD wametibiwa kwa L-dopa, ambayo hulegeza ukakamavu wa misuli na kuboresha miendo ya polepole.[43] Kwa kusikitisha, hakuna dawa ya kuuondoa udhoofu wa akili wala ya wagonjwa wa ALS.[44]

Ushirikiano wa karibu wa familia kwa kawaida umesaidia sana magonjwa haya yakumbapo. Mwanamke mmoja aliyefiwa na baba, dada, na washiriki wengine sita wa familia yake kutokana na ama ALS ama PD alipongeza familia yake, akisema: “Wote walisaidia sana.” Na akisema kwa ukumbuko wa kupendezwa na msaada uliotoka kwa mume wa dada yake mgonjwa, alisema: “Alionyesha upendo mwingi sana! Kila siku alimweka katika kiti-magurudumu na kumtembeza.”[45]

Mwanamke mmoja alichagua kubaki mseja miaka mingi amtunze mama yake. Familia yake ilikuwa tayari imefiwa na washiriki watatu kwa sababu ya ALS, na wengine walianza kudhihirisha dalili.[46] Mwanamke mwingine, aliyepooza kabisa kwa zaidi ya miaka 24, alikuwa na binti watatu, na wawili wa hao waliacha shule wamtunze sana mama yao. Aligeuzwa upande hadi upande kila dakika 30 mchana na usiku.[47] Kwa sababu ya madai ya utunzaji wa daima, familia fulani zimeona ni lazima kuweka wagonjwa hospitalini ambapo wafanyakazi waliozoezwa waweza kuwapa mahitaji yao.[48]

Familia ambazo zimekabiliana na ALS na PD kwa mafanikio zatoa madokezo haya: Uwe na upendo lakini thabiti. Usionyeshe kukosa subira wala kutarajia mengi mno kwa mgonjwa. Uwe na imani katika Mungu. Sali mara nyingi. Wapangie vipindi fulani vya faragha washiriki wa familia wakaao muda mwingi zaidi na mgonjwa. Mpeleke mgonjwa matembezi nyakati fulani na umsaidie kuhudhuria starehe za kijiji au mtaa. Usiaibikie kuwa na mgonjwa katika familia. Na watie moyo watoto, wajukuu, na marafiki kuzuru, maana wagonjwa huwa wapweke mara nyingi.[49]

Ingawa sayansi ya tiba haijapata elezo la wazi kwa maradhi haya, kuna tumaini kwa waliokumbwa na kwa familia zao pia. Biblia huonyesha kwamba karibuni, katika ulimwengu mpya wa Mungu, maradhi yote, maumivu, na kifo yataondolewa milele. Badala yayo, kutakuwako ukamilifu wa akili na mwili, kwa tazamio la uhai wa milele. Hata wafu watafufuliwa kwenye uhai duniani. Tafadhali msomee Neno la Mungu, Biblia, mpendwa anayeugua aweze kujifunza juu ya tumaini la ajabu lililo mbele.—Zaburi 37:11, 29; Isaya 33:24; 35:5-7; Matendo 24:15; Ufunuo 21:3-5.

[Picha katika ukurasa wa 20]

Washiriki wa familia hutatizika kukabiliana na magonjwa yaishiayo kifoni kama haya

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki