Kizungumzio Uwezacho Kula
ETI KITINDAMLO? . . . Naam, KITINDAMLO! . . . Je, umewahi kupangia wageni mlomkuu kisha ukajiuliza, ‘Nitaandaa kitindamlo gani?’ Labda tatizo hili la kuchagua limefanya upekue vitabu vyako vyote vya mapishi kutafuta kitindamlo bora kwa kikusanyiko chako cha kirafiki.
Ungependa kujaribu fondue? Si kwamba ni kizungumzio safi tu uwezacho kula [1] bali pia ni cha haraka na rahisi kutayarisha. Fondue ni nini? Kwa urahisi, ni mchanganyiko wa vichanganyio fulani viyeyushwavyo katika chungu. Halafu, vyakula vingine, tutakavyoviita “vichovyo,” huchovywa ndani ya mchanganyiko huo na kuliwa. Neno fondue hutokana na neno la Kifaransa fondre limaanishalo “kuyeyusha.”[2] Kwa kielelezo, katika fondue ya kitindamlo cha chokoleti, ule mchanganyo huwa hasa ni chokoleti iliyoyeyushwa, na vichovyo ni kinyunga na matunda mapya.
Fondue ya Kitindamlo cha Chokoleti
Upande wa kushoto kuna mapishi ya fondue iliyo kitindamlo cha chokoleti. Ikiwa hujawahi kuijaribu, utashangaa!
Yeyusha chokoleti katika kisufuria. Ongeza vichanganyio vilivyobaki. Koroga mpaka mchanganyiko uwe mzito. Hamisha mchanganyiko uutie katika chungu cha fondue, na uuweke ukiwa na joto juu ya jiko la moto mchache.
Kabla hujaanza kuchovya ndani ya fondue, huenda ukataka kukoroga ndani kahawa ya vijiko viwili vya chai au mdalasini ulio robo ya kijiko kimoja cha chai. Kuzuia vichovyo vya matunda visiwe vyeusi, vinyunyizie umajimaji wa limau ukiwa umechangamana na maji.[6] Ikiwa mchanganyo wa chokoleti ni mwepesi mno, ongeza chokoleti zaidi. Ikiwa ni mzito mno, utohoe kwa maziwa.
Ikiwa unatumia chungu cha umeme cha fondue au chungu cha fondue kilichoinuka juu ya jiko, waweza kutayarisha na kupakua katika chungu kilekile. Weka chungu cha fondue katikati ya meza mahali pa kufikiwa rahisi na kila mtu. Chungu kimoja hutumikia watu sita hadi wanane.
Ikiwa mchuzi fulani umebaki, huhifadhika vizuri katika friji na kuwa kipakwa bora juu ya aisikrimu.[7]
Fondue ya Jibini-Uswisi
Je, ungependa kujaribu fondue ya jibini? Upande wa kulia kuna mapishi ama ya kionjesha-tumbo ama chakula kikuu.
Sugua ndani ya kisufuria kwa upande uliokatwa wa kitunguu-saumu kimoja, halafu tupa kitunguu-saumu hicho. Mwaga divai na umajimaji wa limau ndani ya kile kisufuria, na ukiweke juu ya joto la kiasi. Mapovu yatazuka na kufunika usoni. Usiiruhusu divai kuchemka.
Unganisha wanga-mahindi au wa ngano na jibini iliyokatwa kinyuzinyuzi, na ukoroge.
Unapokoroga ule mchanganyo wa divai daima, ongeza konzi la jibini. Jibini iishapo kuyeyuka, ongeza konzi jingine la jibini, na ukoroge mpaka iyeyuke. Endelea hivyo hadi jibini yote iyeyuke. Ukitaka, koleza kwa pilipili nyeupe na kungumanga au pilipili-mboga na karafuu iliyosagwa.
Hamisha mchanganyo huo wa jibini uutie katika chungu cha fondue, na uuweke juu ya joto la chini hadi la kadiri. Kila mtu ana uma-mpini-mrefu wake mwenyewe wa kulia fondue, ana sahani ya mlomkuu, na uma wa mlomkuu.[10] Dunga tu kimojapo vichovyo na ukizungushe-zungushe kama kwamba unachora 8 katika ile fondue. Weka kile kichovyo juu ya sahani yako ya mlomkuu, na ukile kwa uma wako wa mlomkuu.
Ikiwa fondue ni nyepesi mno, ongeza jibini zaidi.[11] Ikiwa nzito mno, koroga ndani kiasi fulani cha divai iliyopashwa joto.[12] Ule mchanganyo ukitengana, upashe joto jingi, upigepige kwa kipigio, kisha punguza joto.[13] Mchanganyo huo haupasi kutengana ukiukoroga kwa kichovyo kila mara uchovyapo.[14]
Ukipendelea msingi usio na alkoholi katika fondue yako, tayarisha mapishi ya msingi ya mchuzi wa jibini.[15] Changanya vijiko vikubwa vinne vya siagi na vya unga-ngano pia. Pika mchanganyo huo juu ya joto kidogo. Ongeza vikombe viwili vya maziwa baridi, chemsha polepole, na upike mchanganyo huo kwa dakika mbili. Ongeza polepole kikombe kimoja na nusu cha jibini kali na ukoroge mpaka iyeyuke. Koleza kwa chumvi na pilipili. Chovya kama ilivyoelezwa juu.
Kimalizio Kitamu
Mara ile nyingine ukabilipo tatizo la kuchagua kitindamlo, waweza kuchagua kukoroga fondue ya chokoleti. Au labda kwa mlomkuu utapakua fondue ya nyama.
Bila shaka mchanganyo huu wa mionjo mizuri utakuwa kipendezi cha muda mrefu kwako na rafiki zako. Uvutio wacho watokana na kutumia chungu cha ushirika. Kila mtu huchovya ndani, ikifanyiza urafiki wenye shauku, na hicho ndicho kichanganyio kikuu cha kizungumzio uwezacho kula![40]—Imechangwa.
[Sanduku katika ukurasa wa 22]
Mapishi ya Fondue ya Kitindamlo cha Chokoleti[4]
Gramu 170 (aunzi 6) za chokoleti isiyotiwa usukari
Desilita 3.6 (kikombe-na-nusu) za sukari
Desilita 2.4 (kikombe 1) za krimu nyepesi
Desilita 1.2 (nusu-kikombe) za majarini au siagi
Thumni (1/8) ya chumvi ya kijiko kimoja cha chai au tu:
Gramu 340 (aunzi 12) za chokoleti iliyotiwa usukari kidogo[5]
Vijipande vya chokoleti au chokoleti-mapishi yenye usukari
Desilita 1.2 (nusu-kikombe) ya unusunusu (wa krimu na maziwa yasiyoondolewa mafuta)
Vichovyo vya kinyunga:
Keki ya chakula-malaika, keki-vidole (ladyfingers), vitumbua, keki ya kawaida, kyubu (vipande) za paundi-keki (ya wingi wa mayai na siagi)
Vichovyo vya Matunda, Chochote Ukitakacho:
Matufaa, ndizi, cheri, tende, zabibu, machungwa, matikiti, mapapai, mafyulisi (pichi), pea, vipande vya nanasi, stroberi
[Sanduku katika ukurasa wa 23]
Mapishi ya Fondue ya Jibini-Uswisi
Kitunguu-saumu 1, kimekatwa nusu
Desilita 3.6 (kikombe-na-nusu) za divai nyeupe iliondolewa sukari
Kijiko kikubwa cha umajimaji wa limau
Kijiko 1 1/2 hadi 2 vikubwa vya wanga-mahindi au unga-ngano
Gramu 435 (aunzi 16) za jibini-Uswisi, imekatwa kinyuzinyuzi (au muunganisho wa jibini-Uswisi na Gruyère)
Vijiko 2 hadi 3 vikubwa vya divai kirsch (hiari yako)
Pilipili nyeupe na kungumanga au pilipili-mboga na karafuu, ukitaka
Vichovyo:
Mikate 2 mikavu ya Kifaransa (au mkate wa Kiitalia au mikate-viringwa migumu) iliyokatwa kyubu (vipande) za sentimeta 3, kila mmoja ukiwa na upande mgumu
Kuku aliyepikwa, paja la nguruwe, uduvi
Mboga mbichi au zilizopikwa
[Sanduku katika ukurasa wa 24]
Michuzi ya kuchovya:
Mchuzi wa Mronge[22]
ijiko vikubwa 3 vya mronge uliotayarishwa
Desilita 2.4 (kikombe 1) cha krimu ya maziwa-mgando
Kijiko 1 cha chai cha umajimaji wa limau
Thumni (1/8) ya kijiko cha chai cha pilipili-mboga
Changanya vichanganyio
Mayonesi na Mchuzi wa Bizari
Desilita 1.2 (nusu-kikombe) za mayonesi
Desilita 1.2 (nusu-kikombe) ya krimu ya maziwa-mgando
Kijiko 1 cha chai cha umajimaji wa limau
Kijiko 1 cha chai cha bizari
Changanya vichanganyio
Chumvi na pilipili kulingana na upendezi
Mchuzi wa Haradali
Vijiko 3 vya chai vya haradali iliyotayarishwa
Vijiko vikubwa 2 vya kitunguu kilichokatwakatwa
Desilita 2.4 (kikombe 1) cha krimu ya maziwa-mgando
Changanya vichanganyio
Chumvi na pilipili kulingana na upendezi
Mapishi ya Fondue ya Nyama[16]
Kilo 1 ya nyama isiyo na mafuta, mnofu wa kando ya kiuno, au tako la kiuno bila mfupa
Mafuta ya mboga
Angalia: Chungu cha fondue ni lazima [17] kiwe cha chuma kilichoyeyushwa, shaba-nyekundu, au chuma-cha-pua. Vyungu vya kufinyangwa si salama kwa fondue ya mafuta. Mafuta ni moto mno, na chungu kitavunjika[17]
[Picha katika ukurasa wa 23]
“Fondue” ya kitindamlo cha chokoleti
[Picha katika ukurasa wa 24]
“Fondue” ya jibini-Uswisi