Umande-Barafu-Sakitu—
Nani Msababishi wa Usanifu Wayo?
WAKATI hewa iliyoloweshwa na mvuke wa maji ipatapo baridi jioni, haiwezi tena kushikilia maji yote. Maji yale yazidiyo huanguka nje yakiwa umande. Lakini halijoto ya hewa hiyo ishukapo chini ya kiwango cha mgando wa baridi, yale maji mazidifu husablimika—yaani, huruka ile hatua ya kuwa umande wa maji yakaangushwa yakiwa barafu. Vipande vya fuwele za umande wa barafu vilivyofanyizwa kwa njia hiyo ni kama sahani na hufanana na fuwele za theluji. Zikiwa zimeangushwa juu ya madirisha ya nyumba, huvutia kwa maumbo yavyo yenye upatani sahihi sana na vigezo vyayo vya kanda zilizo maridadi. Ni ya usanifu sana.
Lakini kuna namna nyingine ya kutazamisha zaidi ya vipande vya fuwele za umande wa barafu ijulikanayo kama umande-barafu-sakitu. Hiyo ni mikuki-barafu yenye uwazi ndani ikiwa na pande sita zinazochomoza kuelekea juu, nayo ijazanapo katika fungu moja katika mazingira ya nje, huwa na sura nzuri na kwa kufaa huitwa maua ya barafu. Mapema asubuhi moja yenye jua katika Mbuga ya Kitaifa ya Yosemite, California, maua-barafu haya yalipatikana yakikua juu ya miamba katika maji ya Mto Merced utiririkao kupita katika Bonde la Yosemite. Hayo pia ni ya usanifu sana, nayo hutokezwa na zile sheria za kiasili zilizoanzishwa na Muumba wa ulimwengu wote mzima. “Umestahili wewe, Bwana [“Yehova,” NW] wetu na Mungu wetu, kuupokea utukufu na heshima na uweza; kwa kuwa wewe ndiwe uliyeviumba vitu vyote, na kwa sababu ya mapenzi yako vilikuwako, navyo vikaumbwa.”—Ufunuo 4:11.