Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g90 10/8 uku. 31
  • Mbuga ya Kitaifa ya Yosemite—Ina Miaka 100

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Mbuga ya Kitaifa ya Yosemite—Ina Miaka 100
  • Amkeni!—1990
  • Habari Zinazolingana
  • Umande-Barafu-Sakitu—
    Amkeni!—1994
  • Uhai Katika Bonde la Kifo
    Amkeni!—2006
  • Kaa Katika “Bonde la Milima”
    Daftari la Mkutano wa Huduma na Maisha Yetu ya Kikristo—2017
  • Paradiso ya Aina Tofauti
    Amkeni!—1998
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1990
g90 10/8 uku. 31

Mbuga ya Kitaifa ya Yosemite—Ina Miaka 100

KUENDESHA gari tu na kuingia milimani kutoka Merced, Kalifornia, U.S.A., huwa hakutoshi kukutayarisha kwa ajili ya mfululizo wa miono ikutanayo na macho yako wakati uibukapo kutoka kwenye handaki la chini katika barabara kuu. Mara ile ile wewe washangazwa sana na ukubwa na mapana ya Bonde la Yosemite, likiwa na matungamo makubwa ya miinuko na vilele vyenye kuchongoka-chongoka vikiwa vimeinuka juu ya sakafu ya bonde, ambayo yenyewe iko meta 1,200 juu ya usawa wa bahari. Kushoto, El Capitan huinuka wimawima kwa meta 1,100; kulia kuna poromoko la maji la Bridalveil, lenye anguko la meta 190; kule mbali kulia kuna tungamo kubwa la Nusu Kuba, lenye kuinuka hadi meta 2,698. Tamasha hii ni ya ghafula sana na yenye kushtusha. Maneno haya yaja akilini upesi: “Yeye Mwamba [Yehova], kazi yake ni kamilifu.”—Kumbukumbu 32:4.

Mamilioni ya watu kutoka sehemu zote za ulimwengu wameonea shangwe upendezi na fahari ya Mbuga ya Kitaifa ya Yosemite tangu ilipojulishwa kuwa hivyo na Kongresi ya United States katika 1890. Mapema kufikia 1864, Kongresi ikawa imeipa Kalifornia Bonde la Yosemite liwe mbuga ya umma. Siku hizi, Yosemite huvamiwa na umayamaya wa watu iwapo ni msimu mkubwa wa kwenda huko. Lakini ikiwa wewe wataka kuwa peke yako, waweza sikuzote kujasiria kwenda kwenye ile Sierra Iliyoinuka ukaone mandhari yote ukiwa kwenye mwinuko wa juu kama tai.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki