Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g94 12/8 uku. 3
  • Ufuatiaji wa Ufanisi wa Vitu vya Kimwili

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Ufuatiaji wa Ufanisi wa Vitu vya Kimwili
  • Amkeni!—1994
  • Habari Zinazolingana
  • Je, Ufanisi wa Vitu vya Kimwili Hutoa Uhakikisho Kamili wa Furaha?
    Amkeni!—1994
  • Je! Wewe Unaridhika na Kile Ulicho Nacho?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1981
  • Maisha Yenye Kuridhisha Katika Ulimwengu Mpya wa Mungu
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2006
  • Je, Mungu Hutubariki kwa Kutupa Utajiri?
    Amkeni!—2003
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1994
g94 12/8 uku. 3

Ufuatiaji wa Ufanisi wa Vitu vya Kimwili

NA MLETA-HABARI ZA AMKENI! KATIKA TAIWAN

‘FEDHA haziwezi kununua furaha!’ Hata ingawa watu walio wengi hukubaliana kwa kadiri fulani na taarifa hiyo, wengi wao bado wanazidi tu kufuatia mali za vitu vya kimwili kama njia ya kupata maisha yenye furaha zaidi. Na kwani wasifanye hivyo? Ingawaje, yaonekana kwamba suluhisho la mengi sana ya matatizo ya wanadamu hutegemea mafanikio ya vitu vya kimwili na ufanisi.

Ebu wazia ulimwengu ungekuwa tofauti kama nini kama kila mwanamume, mwanamke, na mtoto angefurahia maisha yenye ufanisi wa vitu vya kimwili! Ingekuwa imetoweka ile mivunjio ya heshima na mitaabiko ya mamilioni waishio katika vitongoji na mitaa michafu ya ulimwengu. Pia, lingekuwa limetoweka lile tatizo la kukosa makao linalokumba sasa kila taifa, lenye utajiri na kadhalika lenye umaskini.

Namna gani afya njema, iliyo muhimu sana kwa furaha? Ingawa sayansi ya kitiba inachapusha mwendo, watu zaidi na zaidi wanapata kwamba ni shida kupata huduma zayo. Kwa upande ule mwingine, njaa na utapiamlo bado vyapata mamilioni ya watu. Kama ufanisi ungekuwapo ulimwenguni pote, kila mtu angepata fursa ya kuishi maisha yenye afya zaidi, na hivyo maisha yenye furaha zaidi—sivyo?

Hata dunia yenyewe ingenufaika. Jinsi gani? Sasa mazingira ya dunia yanaharibiwa na vichafuzi vyenye kuua, visababishwavyo kwa sehemu fulani na uchomaji wa fueli za visukuku. Hata hivyo, sababu moja iliyotajwa ya kutofuatia tekinolojia ihitajiwayo ili kutumia namna safi zaidi za nishati ni kwamba i ghali mno. Uharibifu wa misitu ya mvua, ambalo ni tisho jingine zito la mfumo wa kimazingira, pia kwalaumiwa sana kuwa kumesababisha matatizo ya kiuchumi.

Kwa kuwa ufanisi wa vitu vya kimwili waonekana ni kama ungeweza kutatua mengi ya matatizo yetu na kupunguza kutaabika kwingi sana, si ajabu kwamba watu kwa muda mrefu wameshirikisha utajiri na furaha. Kwa kielelezo, ijapokuwa Wanamagharibi kwa desturi husalimiana kwa salamu ya “Furahia Mwaka Mpya!” katika Siku ya Mwaka Mpya, Wachina, wakati wa Mwaka Mpya wa kalenda-mwezi, kulingana na mapokeo huambiana “Kung hsi fa tsai,” wakitumainia ‘kujiambulia utajiri!’ Ndiyo, ni wazi kwamba twaishi katika ulimwengu ambamo watu hutanguliza ufanisi wa vitu vya kimwili katika nafasi ya juu sana, ikiwa si iliyo ya juu kupita zote. Kufanikiwa au kushindwa hupimwa mara nyingi kulingana na vitu vya kimwili.

Ingawa kupata na kufurahia vitu vya kimwili si kubaya kwenyewe, je, kwaweza kutoa uhakikisho kamili wa furaha? Ni umaana wa kadiri gani upasao kushikamanishwa na vitu hivyo? Je, kweli ufanisi wa vitu vya kimwili ndio ufunguo wa kupata ulimwengu mzuri zaidi?

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki