Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g94 12/8 kur. 18-19
  • Je, Mungu Hutoa Thawabu?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Je, Mungu Hutoa Thawabu?
  • Amkeni!—1994
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Thawabu Ni Matendo ya Upendo
  • Thawabu za Sasa na za Wakati Ujao
  • Ona Thawabu Akilini
  • Yehova Huwathawabisha Wale Wanaomtafuta kwa Bidii
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova (Funzo)—2016
  • “Mthawabishaji wa Wale Wanaomtafuta kwa Bidii”
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2013
  • Muumba Wako Anakupenda Sana Wewe
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1978
  • Kujipatia Faraja Kutokana na Neno la Mungu
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1985
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1994
g94 12/8 kur. 18-19

Maoni ya Biblia

Je, Mungu Hutoa Thawabu?

NDIYO, yeye hutoa. Kwa sababu hiyo, je! ni ubinafsi kutumikia Mungu ukiwa na mtazamo wa kupokea thawabu? La, kwa kuwa yeye mwenyewe huweka thawabu mbele ya watumishi wake waaminifu. Kwa uhakika, akiwa Mungu wa haki na upendo, Yehova hujiwajibisha kuthawabisha wale wanaomtumikia. Neno lake, kwenye Waebrania 11:6, husema kwa sehemu: “Ni lazima mtu amkaribiaye Mungu awe na imani katika mambo mawili, kwanza kwamba Mungu yuko na pili kwamba Mungu huthawabisha wale wamtafutao.”—Phillips.

Kuonyesha imani ya kweli katika Mungu hutokeza kupata urafiki wake, na urafiki huu huongoza kwenye thawabu. Mungu hubariki wale wanaotafuta kwa bidii upendeleo wake.

Thawabu Ni Matendo ya Upendo

Yehova hututaka tujue kwamba yeye ni aina ya Mungu ambaye huthawabisha wale wanaompenda. Kwa kielelezo, wazazi wenye ufikirio hutafuta njia za kuthawabisha mtoto wao ambaye hufanya kwa hiari kazi ndogo-ndogo za nyumbani akichochewa na upendo kwa wazazi. Huenda wazazi hao wakaandaa zaidi ya mahitaji yaliyo ya lazima tu ya maisha, wakithawabisha mtoto huyo kwa zawadi ya kipekee. Nyakati nyingine zawadi hiyo huenda hata ikawa fedha za kuweka katika benki ili kuandaa usalama wa wakati ujao wa mtoto huyo. Hivyo basi, Mungu si kama watu ambao hawana uthamini au ufikirio kwa wale wafanyao mambo wakichochewa na upendo au uaminifu. Yehova ni mchangamfu na hukaribia rafiki zake. Ikiwa utashikamana na imani katika yeye, ‘hatakupungukia kabisa, wala hatakuacha kabisa.’—Waebrania 13:5.

Mungu huthamini na kupendelea wote wanaofanya hata utumishi wa kiasi kidogo zaidi kwake, akiwapa fursa zaidi za kumjua yeye. Maneno ya Yesu kwenye Mathayo 10:40-42 huelezea hoja hiyo: “Awapokeaye ninyi, anipokea mimi; naye anipokeaye mimi, ampokea yeye aliyenituma. Ampokeaye nabii kwa kuwa ni nabii, atapata thawabu ya nabii; naye ampokeaye [“mtu mwadilifu,” NW] kwa kuwa ni [“mtu mwadilifu,” NW] atapata thawabu ya [“mtu mwadilifu,” NW]. Na mtu awaye yote atakayemnywesha mmojawapo wa wadogo hawa ngaa kikombe cha maji ya baridi, kwa kuwa ni mwanafunzi, amin, nawaambia, haitampotea kamwe thawabu yake.”

Yesu alitumwa na Baba yake, Yehova. Hivyo, mtu awapokeaye ifaavyo wanafunzi wa Kristo—iwe ni manabii, watu waadilifu, au wadogo—anampokea Kristo na vilevile Mungu, aliyemtuma Kristo. Kwa kweli mtu huyo atabarikiwa; hatakosa kuthawabishwa. Kasha lake la hazina ya mali za kiroho litajaa zaidi. Kwa nini? Kwa sababu Yehova hukumbuka hata tendo dogo sana la utumishi lililotolewa kwa kutegemeza Ufalme wake, na tendo hilo halitakosa kuthawabishwa.—Waebrania 6:10.

Kwa kupendeza, Petro, mwanafunzi wa Yesu, aliuliza Yesu waziwazi kama kungekuwa na thawabu kwa yeye na kwa mitume wenzake: “Tazama, sisi tumeacha vyote tukakufuata; tutapata nini basi?” (Mathayo 19:27) Yesu hakuona swali hilo kuwa lisilofaa bali alitoa jibu chanya, akisema: “Kila mtu aliyeacha nyumba, au ndugu wa kiume au wa kike, au baba, au mama, au watoto, au mashamba, kwa ajili ya jina langu, atapokea mara mia, na kuurithi uzima wa milele.”—Mathayo 19:29.

Thawabu za Sasa na za Wakati Ujao

Jibu alilotoa Yesu linaonyesha kwamba wafuasi wake wanathawabishwa sasa na katika wakati ujao pia. Thawabu moja ya sasa ni kuwa sehemu ya familia ya kimataifa inayopanuka ya ndugu na dada wa kiroho. Wakati ambapo makanisa ya Jumuiya ya Wakristo yanaugua kuhusiana na kupunguka kwa washiriki na ukosefu wa utegemezo, majumba ya kukutania ya Mashahidi wa Yehova yanajaa hata kufikia kufurika kitamathali. Mamia ya maelfu ya Mashahidi wapya wanabatizwa kila mwaka.

Thawabu nyingine zaidi ni amani ya akili pamoja na uradhi na furaha ambayo urafiki pamoja na Mungu na ujuzi kuhusu yeye huleta. Ndiyo, “utauwa [“ujitoaji kimungu,” NW] pamoja na kuridhika” ni faida kubwa. (1 Timotheo 6:6) Huonyesha hali tulivu ya akili kwelikweli wakati mmoja anapoweza kusema, kama alivyosema mtume Paulo: “Nimejifunza kuwa radhi na hali yo yote niliyo nayo,” yaani, kuridhika.—Wafilipi 4:11.

Muda mfupi kabla ya kifo chake, Paulo aliandika kuhusu thawabu ya wakati ujao kwa lile “kundi dogo” la wafuasi watiwa-mafuta wa Yesu—ile thawabu ya ufufuo wa uhai wa kimbingu: “Baada ya hayo nimewekewa taji ya haki, ambayo Bwana, mhukumu mwenye haki, atanipa siku ile; wala si mimi tu, bali na watu wote pia waliopenda kufunuliwa kwake.”—Luka 12:32; 2 Timotheo 4:7, 8.

Mamilioni ya wafuasi wa Yesu ambao ni “kondoo wengine” wake wanatazamia thawabu ya wakati ujao ya uhai wa milele katika dunia iliyogeuzwa kuwa paradiso. (Yohana 10:16) Na Yesu alihakikisha kuwa wafuasi wake wanaokufa ‘watalipwa katika ufufuo wa wenye haki.’—Luka 14:14.

Ona Thawabu Akilini

Inafaa kujaribu kuona akilini baraka hizo, ingawa hakuna ajuaye kwa ukamili jinsi zitakavyokuwa. Je! huwezi kuhisi furaha inayoelezwa kwenye Isaya 25:8: “Amemeza mauti hata milele; na Bwana MUNGU atafuta machozi katika nyuso zote”? Jaribu kuwazia maneno ya Isaya 32:17: “Kazi ya haki itakuwa amani; na mazao ya haki yatakuwa ni utulivu na matumaini daima.” Ndiyo, wanadamu wote watakuwa wakifanya kazi pamoja katika urafiki wa kweli. (Isaya 65:21-25) Hata leo, kazi yenye bidii nyendelevu hutokeza makao mazuri na matokeo yenye thamani bora zaidi. Basi, katika dunia mpya ya Mungu, watu wenye afya chini ya hali kamilifu wataweza kutokeza chochote kihitajikacho kufanya maisha yafurahishe.—Zaburi 37:4.

Thawabu ambazo Mungu hutoa si za kupewa kwa utumishi wowote wenye ustahili kwa upande wetu bali hutoka katika upendo wake kama zawadi japo hali yetu ya dhambi iliyorithiwa. (Warumi 5:8-10) Hata hivyo, kuna uhusiano kati ya thawabu inayotazamiwa na mwenendo wetu. Ni lazima tumtafute Yehova kwa bidii tukiwa na imani jasiri na uvumilivu. (Waebrania 10:35-39) Kwa maneno mengine, “lo lote mfanyalo, lifanyeni kwa moyo, kama kwa Bwana, wala si kwa wanadamu, mkijua ya kuwa mtapokea kwa Bwana ujira wa urithi.” Ndiyo, yeye hutoa thawabu.—Wakolosai 3:23, 24.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki