Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g95 1/22 kur. 8-10
  • Kutafuta Okidi Katika Ulaya

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kutafuta Okidi Katika Ulaya
  • Amkeni!—1995
  • Habari Zinazolingana
  • Fahari ya Okidi
    Amkeni!—2003
  • Kukuza Okidi—Jinsi Subira Huvuta Heri
    Amkeni!—2010
  • Je, Okidi Imo Hatarini?
    Amkeni!—1998
  • Ni Wakati Gani Nyuki Si Nyuki?
    Amkeni!—1997
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1995
g95 1/22 kur. 8-10

Kutafuta Okidi Katika Ulaya

NA MLETA-HABARI WA AMKENI! KATIKA UHOLANZI

OKIDI zavutia watu kila mahali. Mimea hii yafanana na urembo mgeni na mng’ao wenye urangi. Utukiaji wazo katika pori za ndani za kitropiki zisizopenyeka huongeza ule unukato usioelezeka uyazungukayo maua haya. Ni watu wachache hung’amua kwamba okidi hazipatikani katika maeneo ya kitropiki tu, bali zapatikana pia katika maeneo yenye ujoto wa kiasi zaidi ya sayari yetu, kama vile Ulaya.

Spishi za okidi zaweza kupatikana katika maeneo mbalimbali, kutoka Iceland ya aktiki hadi Ugiriki yenye tropiki ya kadiri. Karibu jumla ya spishi 350 zajulikana katika Ulaya. Tofauti na spishi nyingi za kitropiki, spishi za Kiulaya zakua kutoka ardhini, zikipata uhimili wa mizizi udongoni. Katika Tropiki okidi kwa msingi ni vimelea, zikipata uhimili wa mizizi mitini. Spishi nyingi za kitropiki hutoa maua manene, murua, ilhali maua ya okidi za Kiulaya ni ya kiasi kwa saizi.

Uvinjari wa kutafuta okidi katika Ulaya ni upitishaji wakati wenye kupendeza, kwa sababu spishi nyingi hukua katika mazingira yenye kupendeza. Okidi kwa kawaida ni viashiria, vikiashiria kuwapo kwa hali mbalimbali za kimazingira. Spishi nyingi huwa hususi kuhusu mfumo wa mazingira ambamo zinakuwa na huwa katika maeneo ambayo hutimiza matakwa yazo yote. Kwa kielelezo, okidi za viziwa kama vile Dactylorhiza incarnata, hukua katika maeneo ambapo maji ya tabaka ya chini ya udongo yana chokaa ya kutosha. Hili laeleza sababu ya spishi fulani kuwa haba kuliko nyingine. Spishi fulani ya okidi itakayo hali hususa sana itatokea katika maeneo machache zaidi kuliko moja inayoweza kukua katika hali zenye uzuivu mchache zaidi.

Tukisafiri kimawazo kupitia Ulaya, kutoka Uholanzi kuelekea kusini mwa Italia, maeneo yaliyo mengi tuyasafiriyo yana okidi. Tuanze safari yetu na Uholanzi. Katika nchi hii iliyo chini katika Ulaya Magharibi, bado twapata maziwa yaliyo mapana, vibonde vyenye unyevunyevu, na nyanda zenye nyasi. Katika Mei na Juni, hali-nchi fulani ina urangi wa waridi na urujuani wa okidi ya jenasi Dactylorhiza. Ya kupendeza na yenye fahari ni ile spishi Dactylorhiza praetermissa. Mmea huu waweza kufikia kimo cha meta moja na waweza kuwa na vichanuo kufikia 60. Mabaki ya mboji za nyika na pori za vichaka vidogo, hukuza okidi. Kwa msingi katika nyanja za pori zenye unyevu, idadi kubwa ya Dactylorhiza maculata wakati fulani yaweza kupatikana. Katika mboji za nyika tungehitaji kufanya utafutaji wenye umakini kabla ya kupata vichanuo vidogo vya kijani vya Hammarbya paludosa. Okidi hii ndogo hukua katika maeneo yasiyofikilika kabisa.

Twasafiri mbali zaidi, ndani ya safu za katikati za milima ya Ujerumani. Hapa, katikati ya miti yenye kupukutika, miwakilishi kadhaa ya jenasi Epipactis yapatikana. Ingawa baadhi ya hii hukua ndani ya vivuli vizito, mingine, kama vile Epipactis muelleri, hupendelea pembe za pori. Kule kuchanuka kwa zile spishi za Epipactis mwisho-mwisho mwa kiangazi na masika humalizia msimu wa okidi katika Ulaya. Ikiwa katika miinamo ya vilima vilivyo na chokaa nyingi ni aina hususa ya eneo kame la nyasi, eneo la nyasi lenye chokaa, ambalo limejaa okidi. Wakati wa Mei na Juni, huenda tukapata dazani za spishi hapa, miongoni mwazo zikiwamo Orchis militaris na Orchis ustulata zenye kupendeza.

Katika sehemu ya kusini mwa Ujerumani, tunafikia milima ya Alps. Makonde ya majani ya milimani yajulikana kwa ule wingi wawo wa vichanuo. Kwa kawaida okidi huchangia mazingira haya. Makonde hayo ya majani ya milimani, kama yale ya Dolomites katika Italia, huvikwa na okidi urangi wa zambarau katika mwezi wa Julai. Uvuvumukaji wa Nigritella nigra hutokea hapa katika unamna-namna wa marangi. Nigritella hutoa uturi mzito wa vanila, watukumbusha kwamba vanila hutwaliwa kutoka kwa tunda la okidi ya kitropiki.

Okidi zaweza kupatikana kwenye vimo vya zaidi ya meta elfu tatu. Yawezekana kwenye vimo hivyo kupata ile ambayo huenda ikawa ndiyo okidi ndogo zaidi ulimwenguni, Chamorchis alpina. Machanuo ya spishi hii huwa na nusu-kipenyo iliyopungua milimeta tano. Kwa sababu ni za rangi ya kijani, chanuo hizi hazivuti uangalifu mwingi. Hata hivyo, spishi hii ina mahali payo hususa katika mfumo wa mazingira wa milimani.

Tukiwa tumesafiri kupita Alps, twafika eneo la Mediterania la Ulaya. Hapa twapata spishi zaidi za okidi kuliko mahali kwingineko katika Ulaya, na unamna-namna wazo wamakisha. Spishi zenye kupenda ujoto zinazokua hapa huchanua mwanzoni mwa masika tu. Wakati wa kiangazi kisicho na mvua, majani yote, kutia ndani okidi, manyauko, na kwa hakika hakuna mmea wowote wenye kuchanuka unaopatikana. Ni baada tu ya mvua za kwanza za vuli kwamba mimea mibichi hutokea tena.

Okidi huitikia mvua hii. Wakati huo spishi nyingi hufanyiza majani na kuokoka kipupwe zikiwa vitita vya ujani. Ni hadi mwanzo wa masika ndipo huonyesha maua yazo murua. Spishi za jenasi ya Ophrys ni za kawaida katika ujani wa Mediterania. Kwa uchavushaji nyingi za spishi hizi hutegemea wadudu wa kiume ambao huchanganyikiwa na maua yanayofanana na mdudu mwenzi anayetaka kujamiiana. Spishi kadhaa hupata jina kutokana na wadudu zifananao nao, kama vile okidi-buibui, okidi-nzi, na okidi-nyuki-rafiki (Ophrys sphegodes, insectifera, na bombyliflora). Baada ya kujamiiana huko bandia mdudu huyo hubeba ugavi wa chavuo hizo na kuzisafirisha bila kujua kwenye ua jingine la spishi hiyohiyo. Uchavushaji hutukia, na ufanyizi wa mbegu waweza kuanza. Mbinu hii ya uchavushaji ni sahihi kwa njia ya kustaajabisha.

Miongoni mwa spishi fulani za Ophrys, jamii mbalimbali zinajulikana. Kila moja huchavushwa na spishi hususa ya mdudu. Wadudu wachavushaji wa aina moja wapatwapo na maua tofauti lakini yanayofanana na jamii ile, wao hukataa kuyachavusha. Wakati fulani “hitilafu” hutokea, na spishi nyingine kwa kukosea zinachavushwa, ikitokeza mivyauso. Mara kwa mara, mivyauso hii yaweza kutokeza mbegu nzuri na kutokeza upya idadi kubwa ya zao.

Jenasi nyingine ya kawaida katika Mediterania ni okidi-ulimi (Serapias). Spishi hizi huchavushwa na wadudu ambao hulala usiku katika shimo la neli ndani ya chanuo hilo. Kufikia wakati mdudu huyo ataamka, tungamo la chavuo litakuwa limejishikisha kwenye mwili wa mdudu huyo, hivi kwamba ua jingine litachavushwa usiku unaofuata.

Kadiri tulivyosafiri kupitia Ulaya, tuliona maeneo mengi ya kiasili yenye kupendeza yaliyojaa okidi. Hata hivyo, nyingi zimetoweka. Katika maeneo yenye viwanda, yaliyo na idadi kubwa ya watu, na yaliyoendelea kikilimo katika Ulaya, karibu kila eneo lililotengwa la mbuga ya kiasili lahatarishwa na idadi kubwa ya hali zenye kuhatarisha. Mvua ya asidi, ukame, ulimaji upeo wa maeneo ya kilimo, utalii, ukuzi wa majiji, zote zaathiri okidi. Spishi nyingi zimekuwa haba. Katika nchi kadhaa spishi fulani zimelindwa kisheria.

Hata hivyo, kutangaza tu kwamba kitu fulani kimekatazwa kisheria hakusaidii sana. Mwanadamu apaswa kutendea uumbaji kwa staha. Katika mfumo huu wa mambo uliopo usiokamilika, ambapo staha kwa Muumba na uumbaji wake inakosekana, hatutazamii kwamba asili itasitawi. Ni mpaka kwenye mfumo mpya wa Mungu itakapowezekana watu waadilifu kufurahia upatano wa asili. (Isaya 35:1) Ndipo zile aina nyingi za okidi zitathaminiwa ifaavyo kwa jinsi zilivyo.

[Picha katika kurasa za 8 and 9]

Kwenye kurasa mbili hizi kuna okidi kutoka (1) Italia, (2) Uholanzi, (3) makonde ya majani ya milimani, (4) maeneo ya nyasi yenye chokaa, na (5) maeneo ya pori za vichaka vidogo. (6) Okidi kipepeo

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki