Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g98 10/8 uku. 31
  • Je, Okidi Imo Hatarini?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Je, Okidi Imo Hatarini?
  • Amkeni!—1998
  • Habari Zinazolingana
  • Fahari ya Okidi
    Amkeni!—2003
  • Kutafuta Okidi Katika Ulaya
    Amkeni!—1995
  • Kukuza Okidi—Jinsi Subira Huvuta Heri
    Amkeni!—2010
  • Ni Wakati Gani Nyuki Si Nyuki?
    Amkeni!—1997
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1998
g98 10/8 uku. 31

Je, Okidi Imo Hatarini?

Okidi hubadilikana kulingana na hali. Okidi yaweza kukua katika udongo, kwenye miti, hata kwenye mawe. Lakini shirika la Muungano wa Kimataifa wa Kuhifadhi Asili na Mali za Asili (IUCN) laonya kwamba aina nyingi za mimea hii yenye fahari zaweza kushindwa kuokoka porini ikiwa mazingira yao yataendelea kuvurugwa. “Mazingira yanapofanyiwa marekebisho, hii humaanisha kwamba wadudu walio muhimu kwa mchavusho hutoweka kabisa au huhamia mahali penginepo,” asema Wendi Strahm wa shirika la IUCN. Yeye aongezea kwamba “jambo hili litokeapo,” “okidi haiwezi kuzaana.”

Inakadiriwa kuwa asilimia 20 ya okidi milioni tano zinazouzwa ulimwenguni pote kila mwaka hutolewa porini. Shirika la IUCN lasema kwamba jambo hili huhitilafiana na hifadhi ya mmea huu maridadi. Hivyo, shirika la IUCN lapendekeza kwamba wale wanaotaka kujipatia okidi wapaswa kununua ile inayokuzwa katika vibanda vya kukuzia mimea badala ya kuing’oa kutoka kwenye mazingira yake ya asili.

Kuna angalau aina 20,000 za okidi zinazojulikana na mwanadamu. Nyingine zina urefu wa sentimeta 0.6; nyingine hutambaa kufikia urefu wa meta 30. Aina nyingi za okidi husitawi katika maeneo ya kitropiki yaliyo na joto na mvua nyingi. Lakini zinategemea usawaziko wa kiasili ulio wa maana sana ili ziendelee kuishi.

Kwa kusikitisha, kutojua na kutojali kwa binadamu kwaendelea kuharibu mazingira, kukitisha mimea mingi, kutia ndani okidi. Lakini karibuni jambo hili litakoma. Katika ulimwengu mpya ambao Mungu ameahidi, mwanadamu ataishi kwa upatano pamoja na viumbe vya asili. Wakati huo maneno ya mtunga-zaburi yatatimizwa: “Mashamba na yashangilie, na vyote vilivyomo. Ndipo miti yote ya mwituni iimbe kwa furaha.”—Zaburi 96:12.

[Hisani ya Picha katika ukurasa wa 31]

Jardinería Juan Bourguignon

[Hisani ya Picha katika ukurasa wa 31]

Jardinería Juan Bourguignon

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki