Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g97 12/8 uku. 31
  • Ni Wakati Gani Nyuki Si Nyuki?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Ni Wakati Gani Nyuki Si Nyuki?
  • Amkeni!—1997
  • Habari Zinazolingana
  • Fahari ya Okidi
    Amkeni!—2003
  • Kukuza Okidi—Jinsi Subira Huvuta Heri
    Amkeni!—2010
  • Kutafuta Okidi Katika Ulaya
    Amkeni!—1995
  • Kwa Nini Mungu Amekuwa Mwenye Saburi Sana?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1991
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1997
g97 12/8 uku. 31

Ni Wakati Gani Nyuki Si Nyuki?

Nyuki huishi maisha yenye shughuli nyingi, wakitembelea mamia ya maua kila siku na kusafirisha nekta hadi kwenye mzinga tena. Wakati majira ya kuchipua yanapokuja, nyuki wa kiume hutafuta mwenzi. Ili kutafuta, wanategemea kuona na kunusa. Hata hivyo, uangalifu wa nyuki asiyeweza kuona mbali, hunaswa na mchumba asiye wa kawaida—okidi.

Katika kusini mwa Ulaya, kuna okidi kadhaa wa mwituni ambao urutubisho wao hutegemea kuigiza kwao nyuki wa kike. Okidi hawa huhitaji kutuma “vifurushi” vya chavua kwa okidi wenzao. Nyuki ndio wachukuzi walio bora. Lakini kwa kuwa okidi hawana nekta yoyote tamu ya kuwavutia nyuki, wanalazimika kutumia ujanja. Na kengo ni kwamba ua huonekana na kunukia sana kama nyuki wa kike hivi kwamba nyuki wa kiume hujaribu kujamiiana nalo! Kila moja ya spishi hizi za okidi ina namna yake yenyewe ya kujigeuza umbo na manukato.

Kufikia wakati nyuki anapotambua kosa lake, okidi huwa ameweka pakiti yenye gundi ya chavua kwenye mwili wake. Ndipo nyuki huenda zake, na kudanganywa tena na okidi nyingine, ambayo hupokea hiyo chavua. Baada ya kupumbazwa namna hiyo mara kadhaa, nyuki hutambua ya kwamba okidi hawa si wa kuaminiwa. Kufikia wakati huu, yaelekea atakuwa amechavusha baadhi ya maua.

Ni jinsi gani okidi hizi zisizofikiri zilivyopata harufu na sura inayofaa ili kupumbaza nyuki? Namna za utaratibu huu wa kufanya mambo ulio wa ajabu zashuhudia Mbuni mwenye akili, ambaye uumbaji wake haukosi kamwe kushangaza na kuvutia.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki