Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w91 10/1 kur. 2-4
  • Kwa Nini Mungu Amekuwa Mwenye Saburi Sana?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kwa Nini Mungu Amekuwa Mwenye Saburi Sana?
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1991
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Mungu Hujali!
  • Ni Wakati Gani Nyuki Si Nyuki?
    Amkeni!—1997
  • Ufugaji wa Nyuki—Hadithi “Tamu”
    Amkeni!—1997
  • Chavua Vumbi Linaloendeleza Uhai
    Amkeni!—2007
  • Nyuki Dhidi ya Kompyuta
    Amkeni!—1995
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1991
w91 10/1 kur. 2-4

Kwa Nini Mungu Amekuwa Mwenye Saburi Sana?

TAZAMA uso wenye huzuni wa mtoto mwenye njaa. Ona mwili wake uliokonda na tumbo lake lililofura. Fikiria uhitaji wake mkubwa wa chakula, na kuangalia bakuli tupu analobeba. Labda mama yake hutazama kupitia macho yaliyotota, uso wake mwenyewe ukionyesha hali ya kukata tamaa. Halafu jaribu kuzuia huzuni yako—naam, na kujizuia usilie.

Tukio hilo larudiwa mara nyingi mno katika eneo la kilometa milioni 6 za mraba lenye kupatwa na njaa liitwalo Saheli. Linaenea kilometa zaidi ya 4,800 kutoka upande mmoja wa Afrika hadi mwingine kusini mwa jangwa la Sahara, kutoka Senegali kwenye pwani ya Atlantiki hadi Ethiopia kwenye Bahari Nyekundu (Shamu). Bila shaka, njaa inatisha pia watu wengi sana katika nchi nyinginezo. Shirika la Afya Ulimwenguni laripoti kwamba karibu watu elfu milioni 1.1 kuzunguka dunia ni wagonjwa sana au hukosa chakula kinachofaa.

Njaa, bila shaka, ni upande mmoja tu wa kuteseka kwa mwanadamu. Mwanadamu huchafua dunia, nasi sote twaathiriwa. Mifumo ya kisiasa huruhusu ukosefu wa haki na vita vinavyoletea wengi taabu na kifo. Kwa nini Mungu huruhusu mambo kama hayo? Je! yeye hutujali?

Mungu Hujali!

Muumba wetu hutujali. Kuna uthibitisho mwingi wa jambo hilo na wa uwezo wake wa kufanya mambo yafanye kazi pamoja kwa faida yetu na kwa ajili ya upatano katika uumbaji wake wote. Kwa mfano, tazama picha iliyomo ya nyuki akiendea ua kwenye mti wa matunda. Nyuki hutegemea ua kupata nektari (maji matamu yaliyo katika ua) anayohitaji kwa chakula. Kisha, mti hutegemea chavua (unga uliomo ndani ya ua) inayochukuliwa na mwili wa nyuki kutoka mti kama huo. Kwa njia hiyo, ua hilo lachavushwa ili kwamba matunda yakue. Si miti yote ya matunda inayochavushwa katika njia hiyo, lakini kwa uhakika Mungu amepanga ushirikiano usio wa kawaida katika jambo hilo. Na wema wake watokeza matunda ambayo twaweza kula kwa furaha na kwa faida.

Nyuki mwenyewe ni sehemu ya kundi lenye kupangwa vizuri kitengenezo lililo na nyuki zaidi ya 30,000. Wengine hulinda mzinga, hali wengine huusafisha au kuuingizia hewa safi. Wengine bado huweka akiba nektari na chavua, hulisha viluwiluwi, au kutafuta-tafuta vyanzo vipya vya nektari. Mungu mwenyewe amepanga mambo hivi kwamba twanufaika wakati nyuki hao wenye shughuli nyingi wanapotokeza asali tamu na yenye kulisha iliyo na ladha yenye kupendeza.

Muujiza wa ushirikiano kati ya nyuki na mimea na miongoni mwa wadudu wenyewe ni mojawapo ya uthibithisho mwingi kwamba Muumba anaweza kabisa kufanya vitu vyenye uhai vishirikiane. Kwa hiyo, “Mungu si Mungu wa machafuko, bali wa amani.” (1 Wakorintho 14:33) Basi, kwa nini ameruhusu ainabinadamu iwepo katika hali ya kutopatana hivyo, inayotokeza huzuni kwa wengi? Ikiwa Mungu anatujali, ni kwa nini amengoja kwa muda mrefu mno kabla ya kusahihisha hali hiyo? Kwa kweli, kwa nini Mungu amekuwa mwenye saburi sana?

Neno la Mungu, Biblia, lajibu maswali kama hayo. Kitabu hicho cha ajabu kinatuambia kwamba Yehova Mungu amekuwa mwenye saburi kwa sababu nzuri. Hiyo ni sababu gani? Na saburi ya Mungu itaendelea kwa muda gani?

[Hisani ya Picha katika ukurasa wa 2]

Foto ya Jalada: Frilet/Sipa

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki