Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g95 2/8 kur. 24-25
  • Nyuki Dhidi ya Kompyuta

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Nyuki Dhidi ya Kompyuta
  • Amkeni!—1995
  • Habari Zinazolingana
  • Ufugaji wa Nyuki—Hadithi “Tamu”
    Amkeni!—1997
  • Ni Wakati Gani Nyuki Si Nyuki?
    Amkeni!—1997
  • Wajue Nyuki Wasiouma wa Australia
    Amkeni!—2000
  • Kwa Nini Mungu Amekuwa Mwenye Saburi Sana?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1991
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1995
g95 2/8 kur. 24-25

Nyuki Dhidi ya Kompyuta

NYUKI-ASALI wa kawaida ni mwerevu kadiri gani? Kwa wazi, ni mwerevu kuliko kompyuta zenye nguvu zaidi za leo ziwezazo mambo mengi zaidi. Na uwezo wao wa kufanya maajabu huwa katika nafasi ndogo sana.

Moja ya kompyuta zenye uwezo zaidi ulimwenguni yaweza kuchukua habari kwa mwendo wa kasi ajabu wa gigaflopu 16. Kwa usemi wa kawaida, kompyuta hiyo yaweza kufanya shughuli sahili za hesabu bilioni 16, kama vile kujumlisha tarakimu mbili, kila sekunde. Tofauti na hivyo, uhesabu wa kiasi wa matukio yote ya kiumeme na kikemikali yanayotendeka katika ubongo wa nyuki waonyesha kwamba nyuki-asali huyo wa hali ya chini hufanya shughuli mithili ya trilioni kumi kwa sekunde moja. Ajabu!

Nyuki hufanya yote hayo huku akitumia umeme kidogo sana kuliko kompyuta. Kulingana na gazeti Byte, “ubongo wa nyuki hutapanya mikrowati zinazopungua 10. . . . Yeye ana uwezo mwingi kwa karibu viwango saba vya ukubwa kuliko kompyuta zitengenezwazo leo zifanyazo kazi vizuri kupita zote.” Kwa hiyo, bongo zaidi ya milioni kumi za nyuki zaweza kufanya shughuli kwa kutumia kiasi cha umeme kihitajiwacho kwa balbu moja tu mwangaza wa wati 100. Kompyuta ifanyayo kazi vizuri kupita zote leo hutumia nishati izidiyo hiyo kwa mamia ya mamilioni ili kufanya idadi ya shughuli zilizo mithili ya hizo.

Hata hivyo, nyuki-asali hufanya mengi zaidi kuliko kompyuta. Wao waweza kuona rangi, kunusa, kuruka, kutembea, na kudumisha usawaziko wao. Wao waweza kusafiri hewani miendo mirefu wakatafute vyanzo vya mbochi na kisha warudi kwenye mzinga na kuwasilisha mielekezo kwa nyuki wenzao. Wao ni wanakemia hodari sana pia. Huongeza vimeng’enya maalumu kwenye mbochi ili kufanyiza asali. Wao hutengeneza nta ya nyuki kwa utumizi wa kujenga na kurekebisha mizinga yao. Wao hutayarisha vyakula maalumu, kama jeli bora na mkate wa nyuki, kwa ajili ya wachanga wao. Wao hulinda kao lao kwa kutambua na kufukuza wavamizi.

Wakiwa ni watunza-nyumba wazuri, kwa kawaida wao huondoa takataka na vichafu vinginevyo kutoka kwenye mzinga. Wao hudhibiti tabia-anga katika mzinga ama kwa kukusanyika pamoja kibumba ili wapate ujoto majira ya baridi ama kwa kupepea hewa safi iingie humo na kunyunyiza maji majira ya kiangazi. Kao lao liwapo limesongamana kupita kiasi, nyuki ni werevu vya kutosha kujua kwamba baadhi yao ni sharti waondoke. Kwa hiyo wao huchagua malkia mpya kwa ajili ya ule mzinga wa zamani, na yule malkia wa zamani na wengi wa wafanya-kazi huruka pamoja wakaanzishe jamii mpya. Ingawa hivyo, kwanza wapelelezi hutumwa nje wakachunguze maeneo mapya. Hawa wakiisha kurudi na kujadiliana maoni yao, kwa njia ya kitamathali, nyuki “wafyatukaji” huliongoza bumba kwenye kao lalo jipya.

Hao nyuki wa hali ya chini hufanya yote haya bila usaidizi wala mwelekezo wowote wa nje. Wao hutenda kazi kwa kujitegemea. Hata hivyo, kompyuta zilizo zenye nguvu zaidi hutaka vikoa vya watayarisha-programu, wahandisi, na mafundi wa mitambo. Hakuna kifani! Kwa kweli nyuki ni ajabu ibebayo mambo makubwa katika nafasi ndogo sana.

[Hisani ya Picha katika ukurasa wa 25]

L. Fritz/H. Armstrong Roberts

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki