Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g95 3/8 kur. 15-16
  • Kasuku Washaufu-Shaufu wa Australia

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kasuku Washaufu-Shaufu wa Australia
  • Amkeni!—1995
  • Habari Zinazolingana
  • Kasuku Wamo Hatarini
    Amkeni!—2002
  • Kuwatazama Ndege—Je, Kwavutia Kila Mtu?
    Amkeni!—1998
  • Wakati Ndege Wanapogonga Majengo
    Amkeni!—2009
  • “Waangalieni kwa Makini Ndege”
    Amkeni!—2014
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1995
g95 3/8 kur. 15-16

Kasuku Washaufu-Shaufu wa Australia

MGENI wa muda katika Australia angeweza kuwiwa radhi kwa kufikiri kwamba kikundi cha ndege wa kigeni wa kitropiki kilikuwa kimetoroka kutoka kwa makao ya wanyama au hifadhi ya ndege ya mahali hapo. Viumbe ambavyo katika nchi nyingine vingepatikana katika vizimba vyaruka-ruka katika bustani. Kwa hakika hilo ni kweli kwa kasuku wa Australia—na hilo humaanisha familia ya ndege wenye rangi nyingi, na wenye makelele.

Kuna karibu spishi 330 za kasuku, nazo zapatikana kwenye mabara yote makubwa isipokuwa Antarktika, kusini mwa digrii 20 ya latitudo ya kaskazini. Ingawa si spishi zote zipatikanazo katika Australia, kunazo za kutosha katika bara hilo kufanyiza kuwapo kwazo kujulikane! Familia ya kasuku hutia ndani bajiriga (aitwaye na wengine parakiti), kokatoo, na wataalamu wa mbochi, lori. Katika Australia nyakati nyingine ndege hawa maridadi huonekana kana kwamba wako kila mahali.

Hakika hilo lilikuwa ono letu kwenye ziara yetu katika New South Wales. Nyakati nyingine kulikuwako na makumi ya bajiriga wakila uani, hasa mapema asubuhi na baadaye alasiri. Kwenye barabara zenye shughuli nyingi tuliona gala-kijivu, pia aitwaye kasuku-rositi. Mlio wao wa ukelele haupendezi kamwe. Wao ni wamojapo wale wapatikanao sana katika Australia, nayo makundi makubwa hukaa katika miji na majiji. Wao hutua kwenye waya za simu na umeme na wanajulikana kwa kusababisha kukatika kwa waya za mawasiliano katika maeneo ya mashambani. Mume na mke hukaa pamoja hadi kifo na kwa ujasiri wao hulinda viota vyao katika mashimo ya mti dhidi ya wadukizi. Kwa kusikitisha, “wamekuwa wengi sana hivi kwamba waonwa kuwa wadudu waharibifu wa kilimo.”—The Cambridge Encyclopedia of Ornithology.

Katika bustani ya umma, tulikuwa na rosela mwekundu akijilisha kutoka kwa mikono yetu. Akiwa haogopi kamwe makundi ya watalii, kwa wazi walijua mahali pa kupata riziki. Ulikuwa kama madhari ya paradiso kuwa na ndege waliofugwa kama hawa kutuzunguka.

Labda mshangao wetu mkubwa ulikuwa kumwona kokatoo kishungi-njano akifyatuka juu yetu. Kishungi chao cha manjano kwa wazi ni udhahiri wa jina lao. The Illustrated Encyclopedia of Birds yaeleza hivi: “Kikundi kikiwa chajilisha ardhini, ndege wachache hushika doria kwenye miti iliyo karibu na hutoa onyo la hatari kwa milio mikubwa na ya ukali.” Mara moja unajua kunapokuwa na kokatoo katika ujirani!

Ni nini hufanya kasuku kuwa wenye kutokeza hivyo? Kwa karne nyingi mwanadamu amewathamini kwa uwezo wao wa kuigiza sauti ya binadamu. Lakini wao huigiza ndege wengine? Ensaiklopidia ya Cambridge iliyonukuliwa hapo juu ilitaarifu hivi: “Hata ingawa makundi ya kasuku wa mwituni ni yenye kelele, hawajulikani kwa kuigiza spishi nyinginezo na hivyo si dhahiri kwa nini kasuku wana uwezo wa ‘kuongea.’” Tunapofikiria uigizaji wa ndege, Mockingbird wa Amerika ya Kaskazini angali bingwa.

Ndege hupatikana karibu kila mahali ulimwenguni pote—lakini, je, wewe huwaona? Je, wewe huwachunguza? Je, wawajua ndege wanaopitapita ujirani wenu? Je, waweza kubainisha utofauti wa mfanyizo wa rangi, milio, na nyimbo zao? Je, umepata kuona utofautiano wazo wa vigezo vya kuruka? Yote haya yanaweza kuwa uchunguzi wenye kusisimua.

Kukiwa na spishi zaidi ya 9,300 za ndege za kuchunguza, bila kutaja maajabu mengine yanayotuzunguka, ni nani awezaye kudai kwa haki kwamba uhai wa milele utakuwa na ukimwa? Kuna mengi ya kujifunza, kuna sababu nyingi za kumsifu Muumba! Jinsi tunavyoweza kushukuru kwamba Mungu aliona ni vizuri kutia ndani “viumbe virukao vyenye mabawa” katika kazi yake ya uumbaji.—Mwanzo 1:20-23, NW; Ayubu 39:26, 27; Ufunuo 4:11.

[Picha katika ukurasa wa 15]

Gala na (juu) rosela

[Credit line]

Kwa hisani ya Australian International Public Affairs

[Picha katika ukurasa wa 16]

Kokatoo kishungi-njano

[Hisani]

Kwa hisani ya Australian International Public Affairs

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki