Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g95 4/8 kur. 3-5
  • Hali ya Afya Ulimwenguni—Mwanya Unaozidi Kukua

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Hali ya Afya Ulimwenguni—Mwanya Unaozidi Kukua
  • Amkeni!—1995
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Ukweli Wenye Kutisha
  • Afya na Umaskini—Uhusiano Fulani
  • Magonjwa ya Kuambukiza Katika Karne ya 20
    Amkeni!—1997
  • Afya Imeboreka Tufeni Pote Lakini—Si kwa Kila Mtu
    Amkeni!—1999
  • Muungano Hatari
    Amkeni!—1998
  • Ulimwengu Usio na Magonjwa
    Amkeni!—2004
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1995
g95 4/8 kur. 3-5

Hali ya Afya Ulimwenguni—Mwanya Unaozidi Kukua

NA MLETA-HABARI WA AMKENI! KATIKA BRAZILI

WAKATI Ali Maow Maalin alipopata ugonjwa wa ndui katika Somalia mwaka wa 1977, ulimlaza hospitalini na pia ukamweka kwenye vichwa vya habari. Baada ya kutibiwa na kupona, WHO (Shirika la Afya Ulimwenguni) lilitangaza katika 1980 kwamba ndui—baada ya kusumbua mamilioni ya watu kwa karne nyingi—ilikuwa imeondolewa kutoka kwa jamii ya binadamu. Ali alisemwa kuwa wa mwisho ulimwenguni kupatwa na ugonjwa huo.

Katika 1992, WHO liliripoti mafanikio mengine ya utunzaji afya yaliyofikiwa: Wakati wa miaka ya 1980, watu wengi katika ulimwengu unaositawi walipata maji safi ya kunywa na vifaa vya kuleta usafi wa afya. Kwa kuongezea, asilimia iliyo kubwa ya idadi ya watu katika nchi zilizositawi kidogo mno ilipata huduma ya afya karibu na mahali pao. Kama tokeo, wakati wa mwongo uliopita, idadi ya vifo vya utotoni ilishuka mahali pengine.

Ukweli Wenye Kutisha

Hata hivyo, mafanikio haya yalipitwa na hasara na kufunikwa na hatari zilizovuvumka. Fikiria kweli chache zenye kutisha.

HIV/UKIMWI—Zaidi ya watu 17,000,000 ulimwenguni pote wameambukizwa na HIV, virusi isababishayo UKIMWI. Karibu 3,000,000 waliambukizwa katika mwaka mmoja majuzi, karibu 8,000 kwa siku. Zaidi ya watoto milioni moja waambukizwa na HIV. Vifo kutokana na UKIMWI miongoni mwa watoto huenda karibuni vikafyeka mafanikio yoyote yaliyopatikana katika kuokoa watoto katika miongo ya karibuni. Na ugonjwa huu sasa ndio waelekea kuzangaa kwa ghafula na kwa haraka katika maeneo mengi, kama vile Asia. Zaidi ya asilimia 80 ya wote walio na HIV, lasema Aids and Development, waishi katika nchi zinazositawi.

Kifua Kikuu (TB)—Ingawa ugonjwa huu umepuuzwa kwa miongo miwili iliyopita, TB mara nyingine tena yaufika ulimwengu, ikiua karibu watu milioni tatu kila mwaka, ikiifanyiza kuwa muuaji nambari moja ulimwenguni miongoni mwa maradhi yenye kuambukizwa. Zaidi ya asilimia 98 ya vifo hivyo vyote vilitukia katika nchi zinazositawi. Ili kufanya hali iliyo mbaya kuwa mbaya zaidi, ile bakteria ya TB ilijiunga pamoja na HIV, ikifanyiza muungano ufishao zaidi, ukiwa na matokeo yenye kuangamiza. Yatazamiwa kwamba kufikia mwaka wa 2,000, watu milioni moja walioambukizwa na HIV kila mwaka watakufa kutokana na TB.

Kansa—Idadi ya visa vya kansa katika nchi zinazositawi sasa ni kubwa kuliko ile ya nchi zilizositawi.

Maradhi ya Moyo—“Tuko karibu na msiba wa kitufe wa moyo,” aonya Dakt. Ivan Gyarfas wa WHO. Ugonjwa wa moyo sasa umekuwa si msiba wa mataifa yaliyo na viwanda pekee. Kwa kielelezo, katika Amerika ya Kilatini, mara mbili au tatu zaidi ya watu watakufa kutokana na maradhi ya moyo kuliko kutokana na maradhi yaambukizwayo. Katika muda wa miaka michache, usakamaji wa damu katika mshipa moyoni na ugonjwa wa ghafula wa moyo vitakuwa visababishi vikubwa vya vifo kote kote katika nchi zinazositawi.

Maradhi ya Kitropiki—WHO laonya hivi: “Maradhi ya kitropiki yaonekana yamevuka mipaka, kipindupindu kikiwa kimeenea katika Amerika . . . , homa ya manjano na homa kali yakiambukiza idadi iliyo hata kubwa zaidi, na hali ya malaria ikidhoofisha.” Gazeti la Time lasema hivi: “Katika nchi maskini sana za ulimwengu, vita dhidi ya magonjwa yaambukizayo tayari ni tatizo.” Idadi ya watu wanaokufa kutokana na malaria sasa ni karibu milioni mbili kwa mwaka—na hii ndiyo hali baada ya kufikiriwa kwamba yalikuwa yameondolewa yapata miaka 40 iliyopita.

Maradhi ya Kuharisha—Idadi miongoni mwa vijana katika nchi zinazositawi yashtusha. Karibu watoto 40,000 hufa kila siku likiwa tokeo la ambukizo ama utapiamlo; mtoto mmoja hufa kila sekunde nane kutokana na maradhi ya kuharisha pekee.

Afya na Umaskini—Uhusiano Fulani

Hali hii ya afya yaonyesha nini? “Nchi zinazositawi zinafikwa na tatizo maradufu,” akasema mtaalamu wa afya. “Sasa zimefikwa na maradhi yote yenye kusendesha yanayoibuka ya kisasa bali na maradhi ya kitropiki ambayo bado yangalipo.” Matokeo yakiwa nini? “Mwanya wa kijiografia” fulani wenye kufadhaisha wazuka, kikaandika kitabu Achieving Health for All by the Year 2000. Basi, utunzaji wa afya katika nchi zipatazo 40 za Afrika na Asia “hauendi sambamba na ulimwengu mwingine wote.” Mwanya wa afya ni mkubwa—na wazidi kukua.

Ingawa kuna sababu kadhaa za ukuzi wa mwanya huu, mmojapo kisababishi kikubwa cha afya mbaya, lasema gazeti World Health, “ni umaskini.” (Linganisha Mithali 10:15.) Mara nyingi umaskini hushurutisha watu kwa makao yasiyofaa yaliyo na ukosefu wa usafi wa afya, ukosefu wa maji yasiyodhuru na yatoshayo, na hali za kuishi zilizosongamana, na kufinyana. Hali hizi tatu si kwamba tu hudidimiza afya bali kwa hakika hukuza maradhi. Ukiongezea utapiamlo, ambao hudhoofisha kinga za mwili dhidi ya magonjwa, nawe waweza kuona bayana umaskini ufanyizacho kwa afya sawa na vile mchwa kwa gogo.

Maradhi yenye kufisha yachafuapo makazi, hulemaza miili, na huua watoto, maskini ndio hufikwa zaidi. Ona vielelezi fulani. Katika sehemu maskini za Afrika Kusini, visa vya kifua kikuu ni mara mia zaidi kuliko vilivyo miongoni mwa maeneo ya mapato ya juu katika taifa lilohilo. Katika maeneo maskini ya Brazili, mara sita zaidi watu wanakufa kutokana na homa ya mapafu na influenza kuliko katika ujirani wenye utajiri zaidi wapakanao nao. Na idadi ya watoto wanaokufa miongoni mwa familia za India maskini ni mara kumi zaidi ya ilivyo miongoni mwa familia za India zilizo tajiri kuliko zote. Ukweli wenye umizo ni wazi sana: ‘Umaskini ni hatari kwa afya yako!’

Si ajabu kwamba zaidi ya bilioni moja tufeni wanaoishi katika mitaa michafu wameachwa na hisi za kukosa tumaini. Sababu za msingi za wao kuwa maskini hawawezi kuzidhibiti, madhara yenye kuleta ugonjwa humiliki maisha zao. Ikiwa unapatwa na ugonjwa utokanao na umaskini, huenda ukajihisi kifungoni kwenye upande wenye kusononesha wa ule mwanya wa afya. Hata hivyo, uwe maskini au la, kuna hatua fulani waweza kuchukua ili kulinda afya yako na ile ya watoto wako. Ni hatua zipi hizo? Makala ifuatayo yatoa madokezo fulani.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki