Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g99 9/22 uku. 19
  • Afya Imeboreka Tufeni Pote Lakini—Si kwa Kila Mtu

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Afya Imeboreka Tufeni Pote Lakini—Si kwa Kila Mtu
  • Amkeni!—1999
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Umaskini Ungali Unahatarisha Afya
  • Hali ya Afya Ulimwenguni—Mwanya Unaozidi Kukua
    Amkeni!—1995
  • Mtindo Wako wa Maisha Unakabiliwa na Hatari Gani?
    Amkeni!—1999
  • Magonjwa ya Kuambukiza Katika Karne ya 20
    Amkeni!—1997
  • Jitihada za Kuwaokoa Watoto
    Amkeni!—1994
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1999
g99 9/22 uku. 19

Afya Imeboreka Tufeni Pote Lakini—Si kwa Kila Mtu

KULINGANA na The World Health Report 1998, iliyochapishwa na Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO), watu wanaelekea kuwa na afya bora na kuishi muda mrefu zaidi. Ripoti hiyo yatoa mifano kadhaa.

Watu wengi zaidi kuliko ilivyopata kuwa wana vifaa vya utunzaji wa afya, maji safi, na utunzaji wa afya wa msingi. Kwa kuongezea watoto wengi zaidi ulimwenguni sasa wamepewa chanjo dhidi ya maradhi makubwa sita ya utotoni.a Jambo hilo limepunguza vifo miongoni mwa watoto. Ingawa watoto milioni 21 wenye umri unaopungua miaka mitano walikufa mnamo mwaka wa 1955, idadi hiyo imepungua kufikia takriban milioni 10 katika 1997. Wakati uleule, katika nchi kadhaa zilizositawi, vifo vinavyosababishwa na maradhi ya moyo vimepungua sana katika miongo ya karibuni.

Hata hivyo, ripoti hiyo yaongezea kwamba maendeleo ya afya hayajaenea ulimwenguni pote. HIV/UKIMWI wazidi kuwa hatari yenye kufisha. Pasipo kujulikana mpaka mwaka wa 1981, UKIMWI unaoenea umeua watu wapatao milioni 11.7 tangu ulipoanza. Na hakuna tumaini la kupata kitulizo katika wakati ujao ulio karibu. Mnamo mwaka wa 1996, watoto 400,000 wenye umri unaopungua miaka 15 waliambukizwa HIV. Mnamo mwaka wa 1997 idadi mpya ya watoto walioambukizwa wa rika hilo walikuwa takriban 600,000.

Umaskini Ungali Unahatarisha Afya

Afya ya mamia ya mamilioni ya maskini hasa haijaboreka kwa njia yoyote. Wanaishi hasa katika nchi maskini ambako kuna wasiwasi mkubwa wa maradhi, bila matumaini, na maisha ni mafupi. Dakt. Hiroshi Nakajima, mkurugenzi mkuu wa awali wa WHO asema: “Pengo lililopo kati ya hali ya afya ya matajiri na maskini bado ni pana kama lilivyokuwa nusu karne iliyopita.” Kwa kusikitisha, pengo hilo bado linazidi kupanuka, asema mtaalamu mmoja wa WHO, kwa sababu “nchi zinazositawi zimeathiriwa na pigo maradufu. Hazikabiliani tu na maradhi ya kisasa ya kudumu yanayoibuka, bali pia na maradhi ya kitropiki yaliyopo.”

Ijapokuwa hivyo, maendeleo yaweza kufanywa. Kwa hakika, vifo vingi vya kabla ya wakati tayari vinaweza kuzuiwa. Mathalani, “angalau watoto milioni 2 hufa kila mwaka kutokana na maradhi ambayo yana chanjo,” asema Dakt. Nakajima. Akitoa hoja kwamba lazima pengo lililopo katika kiwango cha afya kati ya matajiri na maskini lipunguzwe, Dakt. Nakajima aongezea: “Wakati umewadia wa kung’amua kwamba afya ni suala la tufeni pote.” Ulimwengu unahitaji kwa hima “ushirikiano wa kimataifa kwa ajili ya afya, unaotegemea haki ya kijamii, usawa na umoja.”

Ijapokuwa ushirikiano huo huenda usisitawi karibuni, kila taifa tayari laweza kufanya mengi kuboresha afya ya watu wake, yasema The World Health Report 1998. Jinsi gani? Kwa kuelimisha watu wake wasitawishe “stadi na mitindo ya maisha inayofaa” ambayo huzuia au hupunguza maradhi. Katiba ya WHO yasema hivi: “Maoni ya umma yanayotegemea ujuzi na ushirikiano wenye kuendelea ni mambo yaliyo ya maana zaidi katika kuboresha afya.”

[Maelezo ya Chini]

a Magonjwa hayo sita ya utotoni ni surua, polio, kifua kikuu, dondakoo, kifaduro, na pepo punda inayoathiri watoto.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki