Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g99 7/8 uku. 3
  • Mtindo Wako wa Maisha Unakabiliwa na Hatari Gani?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Mtindo Wako wa Maisha Unakabiliwa na Hatari Gani?
  • Amkeni!—1999
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Je, Ni Mtindo wa Maisha Ulio Bora?
  • Afya Imeboreka Tufeni Pote Lakini—Si kwa Kila Mtu
    Amkeni!—1999
  • Jinsi ya Kulinda Afya Yako
    Amkeni!—1999
  • Hali ya Afya Ulimwenguni—Mwanya Unaozidi Kukua
    Amkeni!—1995
  • Afya Njema—Waweza Kuifanyia Nini?
    Amkeni!—1990
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1999
g99 7/8 uku. 3

Mtindo Wako wa Maisha Unakabiliwa na Hatari Gani?

KATIKA njia nyingi mielekeo ya afya haijapata kutoa tumaini zaidi. Ripoti ya 1998 ya Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) yasema: “Watu wengi zaidi kuliko awali sasa wanaweza kujipatia utunzaji wa afya wa kiwango kidogo, maji safi na vifaa vya kutunza usafi.” Kwa hakika, watu wengi zaidi ulimwenguni bado wanavumilia hali duni za maisha, lakini kama vile Shirika la Utangazaji la Uingereza lilivyoripoti, “umaskini ulimwenguni pote umepunguzwa zaidi katika miaka 50 iliyopita kuliko miaka 500 ya awali.”

Kuboreshwa kwa mifumo ya utunzaji wa afya ulimwenguni pote kumeongeza miaka kwa muda ambao watu hutarajia kuishi kwa wastani wakati wanapozaliwa. Mnamo 1955 wastani ulikuwa miaka 48. Kufikia mwaka wa 1995 uliongezeka kufikia miaka 65. Sababu moja ya ongezeko hilo ni maendeleo ambayo yamefanywa dhidi ya maradhi ya utotoni.

Miaka zaidi ya 40 tu iliyopita, watoto wenye umri unaopungua miaka mitano walifanyiza asilimia 40 ya vifo vyote. Hata hivyo, kufikia mwaka wa 1998, kwa sababu ya dawa za chanjo, watoto wengi ulimwenguni walikuwa wamepewa kingamaradhi dhidi ya maradhi ya msingi ya utotoni. Hivyo, idadi ya vifo vya watoto walio na umri unaopungua miaka mitano, imepungua kufikia asilimia 21 ya vifo vyote. Kulingana na shirika la WHO, kumekuwa na “mwelekeo dhahiri kuhusu maisha yenye afya, na marefu zaidi.”

Bila shaka, maisha marefu zaidi yasiyoboreshwa vya kutosha yangekuwa ni ushindi usio na thamani yoyote. Wakitafuta hali bora za maisha, watu wengi hukazia sana raha zinazoletwa na vitu vya kimwili. Hata hivyo, mtindo wa maisha wa namna hiyo, unaweza kuwa na hatari za afya.

Je, Ni Mtindo wa Maisha Ulio Bora?

Maendeleo ya hivi karibuni ya kijamii na kiuchumi yametokeza mabadiliko makubwa sana katika mitindo ya maisha ya watu. Watu wengi sasa katika nchi zilizoendelea wanaweza kununua bidhaa na kupata huduma ambazo hapo awali ni matajiri peke yao wangeweza kuzigharimia. Na ingawa baadhi ya maendeleo haya yameongeza tazamio la maisha marefu zaidi, watu wengi wameshawishwa kufuatia mtindo wa maisha wa kujiangamiza wenyewe.

Kwa kielelezo, mamilioni wametumia uwezo wao wa kununua ulioongezeka, ili kununua vitu visivyo vya lazima kama vile dawa za kulevya, vileo, na tumbaku. Kwa kusikitisha, matokeo yamekuwa yenye kutabirika kabisa. “Hatari ya afya ya umma inayoongezeka haraka zaidi ulimwenguni si maradhi,” lasema gazeti World Watch, “ni matokeo.” Gazeti hilo laongezea hivi: “Katika miaka 25, maradhi yanayosababishwa na tumbaku yanatazamiwa kuchukua nafasi ya maradhi ya kuambukiza yakiwa tisho kubwa zaidi kwa afya ya binadamu ulimwenguni.” Isitoshe, Scientific American lasema: “Asilimia 30 inayoshangaza ya kansa zinazoua kwa msingi husababishwa na uvutaji wa sigareti, na idadi sawa na hiyo husababishwa na mtindo wa maisha, hasa mazoea ya desturi za milo na kukosa kufanya mazoezi.”

Bila shaka, machaguo tunayofanya kuhusu namna tunavyoishi huathiri sana afya yetu. Basi tunaweza kudumisha au kuboresha afya yetu jinsi gani? Je, milo na kufanya mazoezi kunatosha? Kwa kuongezea, mambo yahusuyo akili na ya kiroho huchangia fungu gani katika mtindo wa maisha wenye afya?

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki