Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g95 4/22 kur. 28-29
  • Kuutazama Ulimwengu

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kuutazama Ulimwengu
  • Amkeni!—1995
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Sayari ya Ajabu
  • Televisheni ama Magazeti Ipi Iendewe kwa Habari Sahihi?
  • Uhusiano wa Mzazi/Mtoto Uweje?
  • Kuzaa kwa Upasuaji Kwaongezeka
  • Kudumisha Sura
  • Ni Nini Huwafanya Walimu Wawe Maarufu?
  • Watoto Wasiotunzwa
  • Maongezi ya Takataka Zetu
  • Chanjo ya UKIMWI “Isiyo na Faida”
  • Mwongozo wa Kimzazi Wahitajiwa
  • Mama Kwenye 62
  • Funguo za Elimu Nzuri
    Amkeni!—1995
  • Kuutazama Ulimwengu
    Amkeni!—1998
  • Kuutazama Ulimwengu
    Amkeni!—1993
  • Kusuluhisha Tatizo la Taka Nyingi—Kwa Uozeshaji
    Amkeni!—1995
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1995
g95 4/22 kur. 28-29

Kuutazama Ulimwengu

Sayari ya Ajabu

Wanasayansi kwa muda mrefu wamekisia kuhusu uwezekano wa kwamba kuna uhai katika sayari nyingine. Ilichukuliwa kwamba hali zifanyizazo uhai uwezekane duniani lazima ziweko vilevile mahali fulani miongoni mwa mamia ya mamilioni ya magalaksi ya ulimwengu-wote-mzima. Hata hivyo, gazeti la Kifaransa Le Nouvel Observateur, lasema kwamba sasa ni wazi zaidi sana kwamba “sadfa nyingi za kimuujiza zilitangulia kutokea kwa mwanadamu duniani” na kwamba uvumbuzi wa karibuni kuhusu ulimwengu-wote-mzima na dunia yenyewe “umepunguza uwezekano kwa kiwango kikubwa, ulio mdogo sana tayari, kwamba utaratibu huohuo ungeweza kuwa ulitokea kwingineko.” Likieleza juu ya kutowezekana kihesabu kwa hali zifananazo kuwako katika sayari nyingine, gazeti laeleza kwamba wanasayansi wana uhakika kwamba uhai uko angalau kwa sayari moja—yetu.

Televisheni ama Magazeti Ipi Iendewe kwa Habari Sahihi?

Katika Australia, habari za televisheni zapungua mno ilhali magazeti yazidi kunawiri. Kulingana na uchunguzi wa vyombo vya habari uliochapishwa katika The Australian, “televisheni [ime]puuza mno usahihi, utegemekaji na haki kwa watazamaji wayo katika ufuatiaji wa ‘hadithi murua.’” Kwa kielelezo, baadhi ya habari za televisheni hutokezwa kwa tepu za zamani ili kufanya hadithi yenye kusisimua zaidi. Uchunguzi huo ulipata kwamba kati ya hadithi za habari 500 zilizochanganuliwa, faili za tepu 260 zilitumiwa kwa muda mrefu. Ikiwa ripoti ya televisheni ilitia ndani faili za tepu, kwa kawaida watu hutazamia hili lithaminiwe, lakini sikuzote hili halifanywi. Ripoti hiyo yaarifu hivi: “Utafiti uliofanywa na Kitovu cha Utafiti cha Ray Morgan . . . waonyesha idadi ya watu walioamini televisheni kuwa njia bora zaidi kwa ajili ya ‘habari sahihi na zitegemekazo’ ilipungua kwa zaidi ya pointi asilimia 12, kutoka kwa kilele cha asilimia 53.7 katika 1986 hadi asilimia 41.5” katika 1993.

Uhusiano wa Mzazi/Mtoto Uweje?

Je, wazazi wanapaswa wawatendee watoto wao kama marika? Mwelimishaji Lisandre Maria Castello Branco wa Chuo Kikuu cha São Paulo asema kwenye gazeti O Estado de S. Paulo la Brazili: “Wazazi hawako sawa na watoto wao, na hili lapasa kuwekwa wazi. . . . Nafasi ya mamlaka inapobaki tupu, kijana anakuwa ameachwa, yatima. Sikuzote mtoto hutazamia wazazi wake wachukue daraka lao kuelimisha mtoto.”

Kuzaa kwa Upasuaji Kwaongezeka

“Wanaginakoloji elfu kumi walaumu Italia: kuzaa kwingi mno kwa upasuaji,” laripoti gazeti Il Messaggero la Rome. Kwa ajili ya idadi ya kuzaa kwa upasuaji, Italia yawa ya kwanza katika Ulaya na ya tatu ulimwenguni, ikifuata Marekani na Brazili. Tangu 1980, oparesheni za kuzalisha zimekuwa maradufu katika Italia; sasa karibu mtoto 1 katika 4 anazaliwa kwa upasuaji. Kwa nini ongezeko hili? Kulingana na Il Messaggero, kuna sababu mbili zaidi ya zile za kitiba: Wanawake wanataka kuepuka kuzaa kwa maumivu, na madaktari, kwa kuogopa kuchukuliwa hatua na mahakama, wapendelea utaratibu ulio na hatari kidogo. Hata hivyo, ingawa kuzaa kwa upasuaji kwa muda mrefu kumeonekana kuwa salama, madaktari wengi waamini kwamba kumetumiwa kupita kiasi na sikuzote si kwa kusudi nzuri. Carlo Signorelli, wa Chuo Kikuu cha La Sapienza, Roma, alisema: “Hakungeonekana kuwa na uhusiano wowote kati ya kuzaa kwa upasuaji na kifo cha wakati wa kuzaliwa.” Na Luciano Movicelli, wa Hospitali ya S. Orsola, Bologna aonelea hivi: “Ule usadikisho kwamba kuzaa kwa upasuaji ni salama zaidi wapaswa kutupiliwa mbali kwa sababu ni uwongo mtupu.”

Kudumisha Sura

Mwanamume Mjapani afanyeje anapopata watu wa ukoo au marafiki wachache ili kudumisha nyuso zinazofaa kwenye arusi na mazishi? Jibu ni: Wakodi. Bwana na bibi arusi kila mmoja kwa kawaida hujaribu kualika idadi sawa ya wageni. Hata hivyo, ikiwa vikundi hivyo viwili si sawa ama ni vidogo mno ili kutokeza, bwana au bibi arusi huenda kwa faragha aombe huduma za benriya, kihalisi “watu wenye mafaa.” Benriya hufanya karibu kazi yoyote ya ziada, kutia ndani kuwa badala ya watu wa ukoo na marafiki. Katika kisa cha mazishi, wanalipwa si kama waombolezaji wenye ujuzi bali kama badala ili majirani wasigundue kwamba, kwa kielelezo, washirika wa kazini wa aliyekufa hawakuhudhuria. Mwenye kampuni ya benriya aliripotiwa katika Mainichi Daily News akisema kwamba katika mazishi fulani ya ofisa mkuu aliyohudhuria, karibu 60 kati ya watu 100 waliokuwako walikuwa benriya. “Familia lazima ilialika kampuni za benriya zifikazo 3 au 4,” akasema.

Ni Nini Huwafanya Walimu Wawe Maarufu?

“Hata ingawa watoto wengi huguna mara nyingi zaidi kuhusu shule, wengi wao bado wana mwalimu maarufu,” laripoti gazeti la Kijerumani Nassauische Neue Presse. Hakika, asilimia 91 ya wasichana na asilimia 83 ya wavulana wana mwalimu maarufu. Uchunguzi wa wanafunzi 2,080 wa umri wa kati ya miaka 7 na 16 ulijaribu kugundua ni sifa gani huwafanya walimu kuwa mashuhuri kwa wanafunzi wao. Huenda ikashangaza kwa wengi kwamba “mwalimu anayepatiana kazi chache mno za kufanyia nyumbani lazima awe ndiye maarufu.” Jambo la maana zaidi ni kwamba mwalimu awe anafuata haki, awe na hali ya ucheshi, na ayafanye masomo yapendeze. Zaidi ya yote wanafunzi wanathamini walimu wanaoweza kueleza mambo vizuri, watulivu, na wanaoonyesha kuelewa hali.

Watoto Wasiotunzwa

Wazazi wengi zaidi na zaidi wa Australia huwaacha watoto wao wajitunze wakati wazazi wangali kazini au wanafanya kazi nyingine. Mwelekeo huo wenye kuhangaisha hasa ulifunuka tangu kuanzishwa kwa simu ya kitaifa ya wasemaji wasiotambulikana kwa ajili ya watoto. Sasa inapokea karibu simu 35,000 kwa juma kutoka kwa wachanga wenye mkazo. Kulingana na The Sunday Telegraph la Sydney, mkurugenzi wa simu hiyo asema: “Tuna mmiminiko wa walio katika hali yenye kutatanisha sana—vitoto vilivyoachwa bila chakula ama utunzaji wowote wa kimzazi.” Gazeti hilo laeleza hivi: “[Huu] ni uidhinisho wa maisha ya familia ya kisasa kama tujuavyo.” Kwa kweli, baadhi ya watoto hawa ni wadogo kama kichezeo; mpiga simu mmoja kwa namba fulani ya dharura alikuwa msichana mwenye hofu wa umri wa miaka minne.

Maongezi ya Takataka Zetu

Takataka zetu zasema nini? Zatuambia namna ya kigezo cha tabia za binadamu tunachofuata. Takataka zafunua kile tulacho na kile tutupacho. “Watu wanaoishi maisha ya kawaida, sahili hutupa kidogo, kwani wao huelekea kununua kile tu wanachohitaji na wanakula kile wanachonunua,” likasema The Toronto Star. Kwa kushangaza, kunapokuwa na upungufu wa kitu fulani, “watu, kwa kinyume, hutupa kingi chacho mno kuliko kinapopatikana kwa wingi,” likaongezea Star. Kwa nini inakuwa hivyo? Watu huweka akiba. Wananunua vingi kuliko wahitajivyo na kisha wanatupa wasivyotumia. Hoti dogi—hoti dogi nyingi—ndivyo vyakula vipatikanavyo kwa ukawaida katika takataka zenye unyevu. Makaratasi, wingi wa makaratasi, hasa yasiyochapwa habari, huishia katika marundo ya takataka. Kizazi cha kompyuta kimeongezea zaidi, si makaratasi machache kwa takataka zetu nyaufu. Ujumbe wa ujumla wa takataka zetu ni kwamba twaishi katika jamii yenye kutumia vitu vibaya.

Chanjo ya UKIMWI “Isiyo na Faida”

Mkurugenzi wa utafiti na maendeleo wa Shirika la Afya Ulimwenguni, Dakt. Piot, ametangaza kwamba ufikirio wa uchumi umesababisha baadhi ya maabara za kimadawa kuacha utafiti wao wa chanjo ya UKIMWI na madawa yatakayosaidia kutibu wagonjwa wa UKIMWI. Imeripotiwa kwamba maabara zahofu kwamba ikiwa chanjo fulani yenye matokeo ya UKIMWI itasitawishwa, msongo wa serikali ungewalazimu kutoa dawa hiyo kwa umma, ikiwaachia nafasi ndogo kwa ajili ya faida.

Mwongozo wa Kimzazi Wahitajiwa

Uongeaji kwa njia ya makompyuta, mara nyingi watoto hupata jumbe zenye shime za kingono ama mapendekezo ya moja kwa moja. Wanaweza kuwasiliana na walawiti-wanaume na wagoni-jinsia-moja. Wanaweza kujifunza jinsi ya kutengeneza mabomu, jinsi ya kuiba namba za kadi ya akiba, na jinsi ya kuingia ndani ya habari za wengine katika mfumo wa kompyuta na kufanya matendo ya uhalifu. Michezo fulani ya kompyuta hushawishi watoto katika hali ya kutoona mambo kwa uhakika, na idadi kubwa huwa waraibu kwayo. Wengine wasema “suluhisho liko katika kazi hiyo ya ujasiri: kufunza maadili,” laandika The Washington Post National Weekly Edition.

Mama Kwenye 62

Kwenye umri wa 62, mwanamke fulani Mwitalia alimzaa mtoto. Mama na mtoto, mvulana aliyekuwa na uzani wa kilogramu 3 na gramu 270, wanaendelea vizuri. Pamoja na hongera kwa ajili ya tukio hilo lenye furaha, kisa hicho pia kilitokeza mwamko katika nyanja ya makabila. Kwa nini? Mama huyo akawa mjamzito kupitia kwa uhimilishaji bandia. “Najua kisa hiki kitatokeza dhoruba,” akasema Profesa Severino Antinori, mwanaginakoloji aliyesaidia kuzaa huko, “lakini inapasa kufikiriwa kama hatua ya kupita kiasi.”

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki