Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g93 6/22 kur. 28-29
  • Kuutazama Ulimwengu

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kuutazama Ulimwengu
  • Amkeni!—1993
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Kashfa ya Damu Katika Ufaransa
  • Unyoofu Wadidimia
  • Ufugaji wa Emu?
  • Matumbawe ya Indonesia Yatishwa
  • Mazoezi na Usingizi
  • Wanywaji Pombe Wachanga
  • Kushindwa kwa Kanisa Kwaendeleza Upagani
  • Kuokoa Ndovu wa Jangwa
  • Kuendesha Gari kwa Njia ya Hatari
  • Je! Kujifungua Mtoto Kupitia Upasuaji ni Salama Zaidi?
  • Tauni Mbaya Zaidi Katika Historia
  • Brolga, Kasowari, Emu, na Jabiru—Baadhi ya Ndege Wenye Kutazamisha wa Australia
    Amkeni!—1996
  • Kuutazama Ulimwengu
    Amkeni!—1995
  • Aksidenti za Magari Je, U Salama?
    Amkeni!—2002
  • Miamba ya Matumbawe Inayokufa—Je, Wanadamu Wanahusika?
    Amkeni!—1996
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1993
g93 6/22 kur. 28-29

Kuutazama Ulimwengu

Kashfa ya Damu Katika Ufaransa

“Msiba usio na kifani katika Ulaya ya Magharibi.” Hivyo ndivyo gazeti la Kifaransa Le Monde lilivyoeleza hivi karibuni juu ya kashfa ya zoea la kukusanya damu kutoka kwa wafungwa ili itiwe mishipani. Katika miaka ya 1980 wagonjwa Wafaransa wapatao 5,000 walipata UKIMWI kutokana na damu iliyoambukizwa—inasemekana kuwa kiasi hicho cha ambukizo ni cha juu zaidi ulimwenguni. Katika 1985, damu iliyokusanywa kutoka kwa magereza ilifanyiza zaidi ya asilimia 25 ya vipimo vya damu yenye ambukizo. Kulingana na ripoti iliyotayarishwa na Halmashauri ya Mainspekta ya Mambo ya Jamii na Halmashauri ya Mainspekta ya Utumishi wa Sheria, zoea la kukusanya damu katika magereza lilianza katika 1954, inaonekana kwa sababu ya uvutano wa kile ripoti hiyo inachoita “sababu za kiuchumi.” Mapema kama 1983, Halmashauri ya Afya ya Ufaransa ilipendekeza kwamba damu isikusanywe kutoka kwa wachangaji wenye uwezekano wa juu wa kuambukiza; na bado maofisa wa magereza hata waliongeza kiasi cha mkusanyo wao wa damu katika mwaka uliofuata.

Unyoofu Wadidimia

“Kuna shimo katika tabaka ya ozoni ya maadili na labda linaendelea kuwa kubwa zaidi.” Akata kauli hivyo Michael Josephson, mwanzilishi na msimamizi wa Taasisi ya Tabia katika Kalifornia, U.S.A. Taasisi yake ilifanya uchunguzi kwa karibu wanafunzi 7,000 wa shule za sekondari na wa vyuo na wakagundua mambo yasiyopendeza. Theluthi moja ya wanafunzi wa shule za sekondari na sehemu moja kwa saba ya wanafunzi wa vyuo walikiri kuiba kitu dukani katika mwaka uliopita. Kila mmoja kati ya wanafunzi wanane wa vyuo walikuwa wamefanya mambo haya yanayofuata: kudanganya kampuni ya bima, kudanganya katika fomu za kutaka msaada wa kifedha, kudanganya juu ya matumizi, na kukopa pesa bila nia ya kulipa. Kulingana na Josephson, ukosefu huo wote wa unyoofu wa vijana ni “ishara tu ya mabaya zaidi yanayofanywa katika ulimwengu wa watu wazima.” Gazeti The Washington Post lataja kifupi maoni yake: “Ukosefu wa unyoofu na tabia mbaya zimeenea sana miongoni mwa vijana wa Amerika kwa sababu zinaenea hata zaidi miongoni mwa watu wazima.”

Ufugaji wa Emu?

Emu wa Australia—ndege mkubwa asiyeweza kupuruka anayefanana na mbuni—huenda hivi karibuni akawa chanzo kikuu cha mapato. Katika 1991 nyama ya emu iliorodheshwa kisheria kuwa namna ya nyama ya ndege. Ufugaji wa emu huenda ukasitawi katika wakati ujao ulio karibu. The Sydney Morning Herald lamnukuu msemaji kutoka Utumishi wa Mbuga za Kitaifa na Wanyama wa Australia akisema hivi: “Karibu mnyama mzima aweza kutumiwa. Hata kuna soko la makucha; makucha hupigwa msasa na kutengenezwa kuwa vito.” Nyama ya emu inasemekana haina mafuta na kolesteroli nyingi, lakini ina protini nyingi. Ndege hao wakubwa hutoa pia ngozi ya aina mbili: ngozi ya aina ya nguo kutoka mwilini mwao na ya aina ya wanyama wanaotambaa kutoka miguuni mwao. Emu hata hutoa mafuta yanayoweza kutumiwa katika kutengeneza marashi. Vitu vinavyotoka kwa emu mkubwa vina thamani ya kati ya dola 300 na 350 za Australia.

Matumbawe ya Indonesia Yatishwa

“Sehemu ya bahari ya Indonesia ina jamii ya matumbawe nyingi zaidi na zenye unamna-namna zaidi ulimwenguni,” gazeti The Jakarta Post lilisema hivyo karibuni. Mbali na kuwa sehemu kuu ya kuvutia watalii na kuwa chanzo cha vitu vingi vinavyotengenezwa vya dawa na tiba, matumbawe na mazingira hayo ya asili yaliyo mazuri hulinda ukingo wa maji usimomonyoke na kupunguza pigo la dhoruba kwa jamii za pwani. Gazeti Post laripoti kwamba kuwapo kwenyewe kwa matumbawe hayo yenye thamani kunahatarishwa na uchafuzi wa binadamu, kwa kuchimba kwake matumbawe yakatumiwe kwa ujenzi, kukusanya kwake matumbawe, na kwa njia za uvuvi zenye uharibifu sana kama vile matumizi ya baruti, na matumizi ya sumu. Gazeti Post laripoti hivi: “Matumbawe yakiisha haribiwa, yatachukua muda wa karibu miaka 20 kwa aina hiyo kutokea tena na miaka 50 hadi 100 kwa unamna-namna wa aina yoyote kutokea tena.”

Mazoezi na Usingizi

“Kwa watu wazee, mazoezi huenda yakawa ndiyo suluhisho la kupata usingizi mzuri, laripoti gazeti Arthritis Today. Katika uchunguzi wa hivi karibuni katika Karolina ya Kaskazini, U.S.A., kikundi cha watu 24 wenye umri wa kati ya miaka 60 na 72 kiligawanywa katika vikundi viwili. Kwa angalau mwaka mmoja, kikundi kimoja kilifanya mazoezi makali mara tatu kwa juma au zaidi; kikundi kile kingine kilifanya mazoezi mara chache sana na si kwa ukawaida. Ilionekana kwamba wale watu waliofanya mazoezi makali kwa ukawaida walikuwa wanapata usingizi haraka mara mbili kuliko wale waliofanya mazoezi kidogo. Jambo hilo lilikuwa kweli hata uchunguzi huo uwe ulifanywa katika siku waliyofanya mazoezi au katika siku nyingine. Gazeti hilo laongeza hivi: “Pia walitumia wakati mchache zaidi wakiwa macho wakati wa usiku.”

Wanywaji Pombe Wachanga

“Karibu watoto 90,000 katika Uingereza wanaonwa kuwa wanywaji pombe kupita kiasi,” laripoti The Sunday Times la London. Serikali ya Uingereza yaeleza kiwango cha juu zaidi cha kileo kuwa kipimo cha 21 kwa wanaume na 14 kwa wanawake. Kipimo kimoja ni glasi moja ya mvinyo au kiasi kidogo cha kinywaji ambacho kina nguvu zaidi au robo ya lita ya bia. Uchunguzi mmoja wa watoto wa shule wa Uingereza 18,000 uligundua kwamba asilimia 11.5 ya wavulana wenye umri wa miaka 15 walikuwa wakinywa zaidi ya kiwango kinachokubalika kwa wanaume wazima kila juma. Miongoni mwa wasichana, 1 kati ya 20 wa wasichana wenye umri wa miaka 14 na 15 walikiri kuwa wanakunywa kupita kiwango kinachokubalika kwa wanawake wazima. Watafiti wanaamini kwamba takwimu hizo zenye kuhangaisha hazionyeshi ukubwa halisi wa tatizo hilo.

Kushindwa kwa Kanisa Kwaendeleza Upagani

Mamia ya watu walihudhuria ile sherehe ya usiku wa kuamkia Katikati ya Kiangazi iliyofanywa karibuni katika sehemu yenye miti mingi ya mashambani ya katikati ya Urusi. Jambo hilo laonyesha kuamka kwa upagani, asema Alexei Dobrovolsky, kiongozi wa kikundi kidogo cha waabudu asili. Desturi zake za ibada zinatia ndani kutembea katikati ya moto na “kuondoa ubatizo” wa watu, akiwatakasa kutokana na “maji matakatifu” waliyonyunyiziwa kanisani. “Wapagani” hao pia husherehekea kuzaliwa kwa jua kila mwaka katika Desemba 25. Baada ya kutumia miaka yapata 13 katika kambi za kazi ngumu, Dobrovolsky alianza kuhubiri kurudi kwa upagani. Ni kwa nini atie moyo upagani? Inaripotiwa kwamba anaamini Kanisa la Orthodoksi la Urusi liliridhiana kwa kushirikiana na serikali iliyovunjwa ya Ukomunisti. Yeye anadai hivi: “Nyakati zote kanisa lilikuwa msaliti. Nyakati zote lilitumikia tu wenye nguvu.”

Kuokoa Ndovu wa Jangwa

Ugonjwa kimeta au anthrax hivi majuzi ulitisha wale ndovu 29 katika Jangwa la Namib lililo kubwa la Afrika. Wahifadhi walikuwa na mahangaiko kwa sababu ndovu mwenye ugonjwa kimeta anaweza kufa katika muda wa saa 24. Kwa hiyo, kwa msaada wa kifedha kutoka nchi za kigeni, walianza kazi ngumu ya kuchanja kundi hilo kutoka kwenye helikopta. Watu wawili, wakining’inia kwa njia iliyo hatari kwenye kila upande, walimlenga shabaha kila ndovu mwenye kutangatanga na mwenye wasiwasi kupitia mavumbi yaliyotifuliwa. Mtu mmoja alifyatua vishale vyenye dawa za kuchanja, yule mwingine alirusha kwa bastola rangi ya kutia alama kila ndovu aliyechanjwa. Kwa ujumla, ndovu 21 “walichanjwa” kwa mafanikio na wahifadhi wakaridhika. Utendaji huo wenye kugharimu sana na ulio hatari ulionwa kuwa unafaa ili kuokoa wale ndovu halisi pekee wa jangwa ulimwenguni.

Kuendesha Gari kwa Njia ya Hatari

Kusoma ramani za barabara, kusema ndani ya tepu-rekoda, kutumia simu zinazochukulika, wanawake kubadili soksi ndefu. Mambo hayo, kulingana na The Star, gazeti la Afrika Kusini, ndiyo baadhi ya mambo ambayo watu hufanya wanapoendesha gari, nyakati nyingine wakiwa kwenye mwendo wa zaidi ya kilometa 100 kwa saa. Ofisa mmoja wa usalama wa barabarani asema kwamba mara nyingi yeye huona watu wakisafisha meno yao kwa kutumia mikono yao yote miwili huku wakiendesha gari! Madereva pia wameonekana wakipiga mswaki na kusukutua meno. Mwanamke mmoja alimnyoa kichwa mwana wake alipokuwa akiendesha gari kumpeleka shuleni. Mama mmoja alionekana akibadili nepi za mtoto akiwa anaendesha gari kwa mwendo wa kilometa 90 kwa saa. Ni kwa nini madereva hujihatarisha hivyo? Ofisa mmoja alisema kwamba mwendo mrefu na msongamano wa magari unaweza kushawishi madereva watumie kwa “ubora” wakati wanaotumia ndani ya gari. Lakini, alisema kwamba vikengeusha fikira hivyo vinaweza kutokeza aksidenti mbaya sana.

Je! Kujifungua Mtoto Kupitia Upasuaji ni Salama Zaidi?

Wanawake wengi huchagua kuzaa kwa kupasuliwa wakiamini kwamba upasuaji utakuwa salama na hautakuwa na uchungu zaidi. Kulingana na Jornal do Brasil, madaktari wengi pia hupendelea kupasua kwa sababu ingawa “uzazi [wa kawaida] huchukua kwa kawaida wastani wa muda wa saa 8 hadi 12 na hauna tarehe kamili ya kutukia, upasuaji waweza kupangwa na ukichelewa zaidi unachukua muda wa saa moja.” Hata hivyo, daktari-mkunga Fernando Estellita Lins anukuliwa kuwa akisema: “Idadi wa vifo, vinavyotokana na maambukizo na kuvuja damu kwa sababu ya upasuaji, ni juu zaidi miongoni mwa wanawake wanaopasuliwa.” Utafiti wa Brazil umeonyesha kwamba vifo vya akina mama “kutokana na uzazi wa kupitia uke vlikuwa 43 kwa kila elfu 100, huku [vifo] vya upasuaji vikiwa 95 kwa kila elfu 100.”

Tauni Mbaya Zaidi Katika Historia

Jamii ya kisayansi inathibitisha tena ukali wa homa ya Kihispania. Kulingana na The New York Times Magazine, watu 196,000 walikufa katika United States pekee katika mwezi wa Oktoba 1918. “Kufikia mwisho wa kipupwe cha 1918-19, watu bilioni mbili ulimwenguni pote walikuwa wameambukizwa homa, na kati ya milioni 20 na milioni 40 walikuwa wamekufa,” gazeti hilo likasema. John R. La Montagne, ofisa mmoja wa Taasisi ya Kitaifa ya Mizio na Magonjwa ya Kuambukiza katika Bethesda, Maryland, alisema kwamba homa ya Kihispania ya 1918 ilikuwa “ugonjwa wa kipuku ulio mbaya zaidi ambao umepata kutukia katika historia.” Ni kweli kwamba huko nyuma katika 1347, tauni ya jipu, au Kifo Cheusi, ilipatia ainabinadamu pigo lenye uharibifu mkubwa sana lililochukua muda wa miaka minne. Lakini kulingana na gazeti hilo, “ugonjwa huo wenye kuenea [wa 1918] uliua watu wengi kwa mwaka mmoja kwa kadiri ya wale waliouawa na Kifo Cheusi cha miaka minne.”

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki