Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g95 4/22 uku. 30
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
  • Amkeni!—1995
  • Habari Zinazolingana
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
    Amkeni!—1995
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
    Amkeni!—1995
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
    Amkeni!—1995
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
    Amkeni!—2005
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1995
g95 4/22 uku. 30

Kutoka kwa Wasomaji Wetu

Elimu Nimehitimu tu kutoka chuo kikuu fulani cha Nigeria na nilikosa kupata gredi za juu zaidi kwa nafasi ya asilimia mbili. Nilishuka moyo kwa kiasi fulani. Kwa hivyo mlipochapisha makala “Kutokuza Elimu” (Agosti 22, 1994) na kuonyesha kwamba elimu haipasi kufuatiwa kwa kusudi la kutaka kuwa bora kielimu, nilianza kuona mambo kwa mtazamo unaofaa. Ingawa maprofesa wangu wamenitia moyo nifuatie masomo ya baada ya kuhitimu, nayafikiria mambo kwa uzito katika uwelewevu wa lile ambalo nimejifunza.

G. J., Nigeria

Nina umri wa miaka 14 na niko chini ya msongo mwingi ili nifuatie masomo ya juu. Kwa msaada wa makala yenu, nimeamua lile ningependa kufanya. Nataka kuwa painia [mweneza-evanjeli wa wakati wote], na nikitaka mazoezi ya ziada ili kupata kazi, ningependa kwenda katika shule ya kazi-maisha ili nijifunze upigaji picha.

H. O., Marekani

Nilichagua kutopata elimu ya ziada. Napendelea kutumia wakati huo kufunza wengine juu ya Muumba wetu. Kwa kawaida watu hushangazwa na kadiri nijuavyo juu ya habari mbalimbali. Wao huuliza, “Wewe uko koleji?” Mimi huwaambia nilijifunza yale nijuayo kutoka kwenye Biblia na fasihi ziandaliwazo na Watch Tower Society.

M. L., Marekani

Makala yenu ilionyesha uhitaji wa kufikiria manufaa na hasara za elimu ya ziada. Nilihisi uhitaji wa kwenda shuleni tena lakini sikutaka kupuuza utendaji wa kiroho. Nilimweleza mwandishi wa shule yangu kuhusu ratiba yangu ya mikutano ya Kikristo, naye akapanga masomo yangu hivi kwamba ningeweza kuhudhuria mikutano yote.

M. F. S., Brazili

Chombo Dhaifu? Asanteni sana kwa makala yenu yenye kuelewesha “Maoni ya Biblia: Kile ‘Chombo Dhaifu’—Je, Ni Kuvunjia Wanawake Heshima?” (Oktoba 8, 1994) Kila mwanamume apaswa kusoma makala hii, kwa kuwa imeelezewa vizuri sana.

G. B., Marekani

Sikuwa kamwe nimeelewa elezo la Biblia kwenye 1 Petro 3:7 kuhusu wanawake kuwa ‘vyombo dhaifu.’ Sikuzote nilifikiri kwamba wanawake walikuwa viumbe wasio na umuhimu sana, kwa kuwa nilikua nikiona wanaume wakiwatendea wanawake kwa heshima kidogo sana. Lakini makala hiyo ililainisha kufikiri kwangu.

T. C., Marekani

Jinsia Tofauti Asanteni sana kwa zile makala “Vijana Huuliza . . . “Kwa Nini Ni Vigumu Sana Kwangu Kuacha Kufikiria Watu wa Jinsia Tofauti?” na “Naweza Kuachaje Kufikiria Watu wa Jinsia Tofauti?” (Julai 22, 1994; Agosti 8, 1994) Ilikuwa vyema kujua kwamba mimi si mwehu, tangu umri wa miaka 12 nimekuwa na hisia zenye nguvu kuelekea mvulana fulani nimjuaye. Makala ya pili ilinisaidia kuacha kufikiria juu yake mno. Nilimwambia dada fulani Mkristo aliye mzee zaidi katika kutaniko langu, naye alinisaidia.

P. Z., Marekani

Ile sehemu juu ya punyeto ilinihusu mimi moja kwa moja. Nilifikiri kupiga punyeto kungenisaidia kupunguza uchu wa kingono, lakini huzifanya kuwa mbaya zaidi. Naomba Yehova anisamehe kwa kuhusika katika zoea hili lenye kinyaa.

P. M., Marekani

Makala hiyo ilikuja kwa wakati ufaao kwa ajili yangu. Katika shule kichwa kizungumzwacho sana ni ngono. Kuna msichana fulani shuleni anayehudhuria kutaniko lilelile nihudhurialo. Namwona kuwa mwenye akili sana, mwerevu, na mrembo. Makala hiyo ilinisaidia kuepuka kumwazia kwa kuendelea na kumtazama daima.

M. F., Ujerumani

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki