Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g95 4/8 uku. 30
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
  • Amkeni!—1995
  • Habari Zinazolingana
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
    Amkeni!—1994
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
    Amkeni!—1995
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
    Amkeni!—1994
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
    Amkeni!—1995
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1995
g95 4/8 uku. 30

Kutoka kwa Wasomaji Wetu

Uhuru wa Mawazo Mara nyingi nilikuwa nimeacha akili yangu itangetange, nikidumu katika mawazo yasiyofaa. Hiyo ndiyo sababu nilishangazwa kusoma makala “Maoni ya Biblia: Je! Biblia Hukataza Uhuru wa Mawazo?” (Juni 8, 1994) Sikuwa nimetambua kuwa Yehova Mungu angeiona kuwa dhambi ikiwa mtu kwa kutaka angetafakari juu ya mwendo wenye kosa. Namshukuru Yehova kwa kunipa shauri hilo la moja kwa moja litakalonisaidia kurekebisha kuwaza kwangu kulikopotoka!

J. P., Filipino

Matatizo ya Mahaba Asanteni sana kwa makala “Vijana Huuliza . . . Namna Gani Nikishikwa na Mahaba kwa Mtu Asiye Mwamini?” (Mei 22, 1994) na “Naweza Kuachaje Kuvutiwa Kimahaba na Mtu Fulani?” (Juni 8, 1994) Mfanya-kazi mwenzangu alikuza hisia zenye nguvu kunielekea, nami nilijikuta mwenyewe nikija kuvutiwa naye. Nilijua kuwa hili lilikuwa kosa na nikasali kwa Yehova kwa ajili ya msaada. Nilipoona makala hizi, nilizisoma tena na tena. Sasa natambua kwamba maumivu ya moyo ya kipindi kifupi ambayo yangetokea kwa kuachisha uhusiano huo ni bora sana kuliko matatizo ya maisha yote ambayo yangetokea kutokana na uhusiano wenye kuumiza.

P. J., Marekani

Yaonekana makala hizo ziliandikwa kwa ajili yangu hasa! Nashindwa ni nini kingalitukia kwangu ikiwa makala hizi hazingeandikwa. Asanteni kwa kujua matatizo wanayokabili vijana.

S. J., Nigeria

Nina upendo wa kupumbazwa juu ya mvulana mmoja darasani mwangu. Yeye ni mwenye kuvutia na mwanana sana. Ingawa hivyo, tangu nisome makala hiyo, mimi huendelea kujiuliza, ‘Je, yeye hushiriki miradi na njia yangu ya maisha?’ Baada ya kufikiria hili, natambua jinsi nimeendelea kuwa mpumbavu hadi wakati huu. Nataka kushinda upendo huu wa kupumbazwa hivi karibuni!

S. T., Japani

Nilimpenda mtu asiye mwamini na kuolewa naye. Alienda kwenye mikutano ya Kikristo ili kunipendeza tu. Baada ya kuoana, alibadilika. Hata alijaribu kunizuia kumtumikia Yehova. Halafu alinipiga na hakuwa mwaminifu. Sasa najipata nikiwa nimetalikiwa. Laiti wachanga wote wangeweza kuona jinsi ilivyo hatari kupeana miadi ya kijinsia na mtu asiye mwamini! Sipendi yeyote apitie hali niliyopitia.

T. F., Puerto Riko

Mkazo Asanteni sana kwa makala “Maoni ya Biblia: Ni Nini Kiwezacho Kusaidia Mkazo Wako?” (Septemba 8, 1994) Nililelewa nikiwa Mkristo lakini nikaacha kweli katika miaka yangu ya utineja. Nimerudi kwa miaka mitatu sasa, lakini nimeolewa na mtu asiye mwamini. Mimi hufikiria kwa wasiwasi na kwa kuhuzunika juu ya makosa niliyofanya, bila kutambua kwamba ndiyo sababu nimekuwa nikipata mkazo mwingi sana. Asanteni kwa kunifanya nione kwamba haisaidii kudumu katika mambo ya wakati uliopita. Badala yake, napaswa kufanyia kazi wakati wangu ujao.

R. L., Marekani

Mlisema kuwa ‘watu wa umri wote hupatwa na mkazo.’ Nina miaka 21 na huwa mgonjwa wa mkazo mkali. Nimekuwa hospitalini mara mbili kati ya miezi minane kwa sababu ya mikazo ya ghafula ya misuli na kuumwa sana kichwa kunakohusianishwa na mkazo. Kila wakati madaktari wamenieleza kwamba mimi ni mchanga sana kupatwa na mkazo. Hivyo makala yenu ilinipa hisi ya kitulizo.

V. P., Marekani

Somo la Jiografia Mimi ni msichana mwenye umri wa miaka 11, na nilithamini sana ile makala “Visiwa Vinavyoelea vya Ziwa Titicaca.” (Juni 22, 1994). Katika darasa la jiografia mwalimu alituuliza ikiwa watu waliishi kwenye Ziwa Titicaca. Wanadarasa wenzangu wote walisema la. Nikiwa nimesoma Amkeni!, nilijibu ndiyo. Mwalimu aliniuliza jinsi nilivyojua, akiniandalia fursa ya kumtolea ushahidi mzuri.

S. B., Italia

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki