Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g95 1/8 uku. 30
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
  • Amkeni!—1995
  • Habari Zinazolingana
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
    Amkeni!—1994
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
    Amkeni!—1995
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
    Amkeni!—1995
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
    Amkeni!—1994
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1995
g95 1/8 uku. 30

Kutoka kwa Wasomaji Wetu

Kuzaliwa Upya Katika Mwili Mwingine Asanteni kwa ule mfululizo mzuri sana wa makala “Je! Umepata Kuishi Awali? Je! Utaishi Tena?” (Juni 8, 1994) Makala hizi zaeleza ile kweli juu ya hali ya wafu kwa njia sahili na ya kiakili. Mimi naamini kwamba mtu yeyote anayetafuta kweli kuhusiana na habari hii hana jingine ila kukubali tu yale ambayo mmeandika.

F. P., Italia

Aliyekuwa Mwanandondi Asanteni sana kwa ile makala “Nilijifunza Kuchukia Kile Nilichokuwa Nimependa.” (Juni 8, 1994) Kisa cha Obdulio Nuñez kimetusaidia kuelewa baadhi ya matatizo ya kitiba ya mume wangu. Akiwa mwanandondi zamani, yeye pia hupatwa na mshuko wa moyo. Kweli, ni Yehova Mungu ambaye amesaidia mume wangu kugeuza maisha yake!

S. S., Marekani

Maumivu Mimi ni tabibu wa kukanda mwili nami nataka kuwashukuru kwa ule mfululizo “Je! Maisha Bila Maumivu Yawezekana?” (Juni 22, 1994) Nilivutiwa sana na ufahamu wenye kina, usawaziko, na hekima iliyoonekana wazi katika utafiti na utoaji wa habari hii. Makala hiyo itakuwa msaada wenye thamani kubwa kwa wataalamu, wagonjwa, na wengine. Kwa kutumia mbinu za kukanda mwili, mimi naendelea kupambana na maumivu, nikingojea siku ile ambapo maumivu ya kuendelea hayatakuwapo chini ya Ufalme wa Mungu.

D. T., Denmark

Makala hizi zilinifariji sana. Nilizishiriki pamoja na watu wengine kadhaa ambao, kama mimi, hukabiliana na maumivu kila siku.

M. G., Marekani

Nimelala hapa nikiwaandikia nikiwa kwenye kitanda changu, ambapo nimekaa sana pindi kwa pindi muda wa miaka miwili na nusu iliyopita kwa sababu ya kuteguka vipingili viwili vya uti wa mgongo. Asanteni kwa ile makala nzuri ajabu “Je! Wewe Huumwa na Mgongo?” (Juni 8, 1994) Nililia nilipokuwa nikiisoma, kwa maana ilikuwa ni kama kwamba mnaongea nami. Singeweza kamwe kuamini kwamba mtu yeyote angeweza kuelewa tatizo hili waziwazi hivyo.

B. H., Uingereza

Siku kumi tu zilizopita, nililazimika kufanyiwa upasuaji wa mgongo, nami nawashukuru kwa hiyo habari sahihi. Hiyo makala ilinisaidia kuelewa kisababishi cha maumivu yangu. Madokezo yaliyotolewa ni yenye mafaa sana, nami natumaini wengi watayatumia na kuepuka upasuaji.

K. G., Hungaria

Ni Kosa la Tarehe ya Kimuziki? Nilipenda sana ile makala “Kutoka Kuwa Hipi Mwomba-Lifti Hadi Kuwa Mishonari wa Amerika Kusini.” (Machi 22, 1994) Lakini jambo moja lilinitatanisha. Richard Fleet ataja kwamba alienda Liverpool kuwaona Beatles katika Septemba 1973. Kwa kadiri nijuavyo, Beatles walifanya maonyesho hadharani kwa mara ya mwisho katika 1969 na wakagawanyika katika 1970.

C. S., Ujerumani

Pole kwa kutokuelewa vizuri. Richard Fleet alikusudia kusema kwamba alienda Liverpool ili aone klabu fulani ambapo Beatles walikuwa wamefanya maonyesho wakati mmoja.—Mhariri.

Kujiua Nawashukuru kwa moyo wangu wote kwa ile makala “Vijana Huuliza . . . Je! Suluhisho Ni Kujiua?” (Aprili 8, 1994) Mimi nimetamani sana kuchukua hatua hiyo mara nyingi sana. Nilipokuwa mdema, nilitendwa vibaya kingono na mtu fulani niliyemtumaini. . . . Wakati uliopita, nimeandika vibarua vingi sana vikisema, ‘Nataka kufa’ hata siwezi kukumbuka ni vingapi. Tangu wakati huo nimekuwa mmoja wa Mashahidi wa Yehova, na sasa natumikia nikiwa mweneza-evanjeli wa wakati wote, lakini kichocheo hiki bado hunijia mara kwa mara. Nilikuwa na hisia hii siku ile tu iliyotangulia kupokea makala hiyo. Ilinifanya nilie. Lakini Yehova ameniruhusu nibaki hai, naye aonekana ni kama ananiambia kwa uanana hivi, ‘Fuliza kuishi.’ Kwa kweli, nawashukuru nyinyi sana.

Y. K., Japani

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki