Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g94 12/22 uku. 30
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
  • Amkeni!—1994
  • Habari Zinazolingana
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
    Amkeni!—1995
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
    Amkeni!—1995
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
    Amkeni!—1995
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
    Amkeni!—2000
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1994
g94 12/22 uku. 30

Kutoka kwa Wasomaji Wetu

Kujiua Nilisoma ile makala “Vijana Huuliza . . . Je! Suluhisho Ni Kujiua?” (Aprili 8, 1994) nikiwa na hisi za hofu na wasiwasi. Nina umri wa miaka 20 na ni mhudumu wa wakati wote sasa. Kitambo kifupi kilichopita, nilikuwa na msukumo wa kujiua. Yehova amenisaidia na anaendelea kunitegemeza. Siku chache zilizopita, wakati mmoja wa rafiki zangu wa karibu aliponiambia kuwa alikuwa amejaribu kujiua, nilitafuta shauri lenye kutumika ambalo lingemsaidia kutokata tamaa. Makala hii ilijibu sala zangu.

A. C., Italia

Ni wiki iliyopita tu mawazo ya kujiua yalikuwa yenye nguvu moyoni mwangu. Mzee mmoja Mkristo na mke wake walipata kuwa wasiri wa karibu na walinisaidia kufaulu kushughulikia jambo hilo. Makala zenu nyingi kuhusu mshuko wa moyo zimekuwa zenye kuokoa maisha kwangu.

D. J., Marekani

Ilinilazimu kuelezea shukrani zangu nyingi sana kwenu kwa ajili ya makala hiyo. Ilinisisimua zaidi ya makala nyingineyo ya wakati wowote ule niwezayo kukumbuka. Unajua, miaka michache iliyopita niliamini kwamba kujiua kulikuwa jambo la kuchagua—njia ya kutokea katika hali inayoelekea kuwa isiyovumilika. Lakini, kwa msaada wa wazazi na marafiki, nilikuja kujua kwamba nina sababu bora zaidi ya kuishi—Yehova alitaka niishi.

M. V., Marekani

Niliona makala hii ikiwa yenye kufahamika na iliyoandikwa vyema. Nahisi kwamba hiki ni chombo chenye thamani kabisa ili kusaidia watu wowote wawezao kuwa na fikira za kujiua. Niliguswa moyo na vielelezo vilivyotiwa ndani.

L. S., Marekani

Hipi Mwomba-Lifti Nataka kuwashukuru kwa ile makala kuhusu Richard Fleet, “Kutoka Kuwa Hipi Mwomba-Lifti Hadi Kuwa Mishonari wa Amerika Kusini.” (Machi 22, 1994) Baada ya arusi yetu mchumba wangu nami twapanga kuhamia Hungaria kusaidia katika kazi ya kuhubiri huko. Kabla ya wakati huu nilihisi wasiwasi sana kuhusu badiliko kamili katika mtindo-maisha na kujifunza lugha mpya. Makala hiyo ilionyesha waziwazi kwamba jambo la maana si mahangaiko ya kibinafsi bali watu tunaowahubiria.

S. H., Ujerumani

Nasadiki watu wote waseja wanapaswa kusoma makala hii na watambue kwamba unaweza kuwa mtumishi wa Yehova na uwe na furaha bila mwenzi. Inavutia kusoma jinsi mwanamume mseja alivyotumia kwa ukamili Mathayo 6:33 katika maisha yake. Tangu nilipoanza kutumikia kama mweneza-evanjeli wa wakati wote miaka miwili na nusu iliyopita, nimejionea shangwe sawa na ile ya Richard Fleet.

D. M., Marekani

Niliguswa moyo sana kujua kwamba kuna wanaume wenye huruma kwa wavulana wasio na baba. Mimi ni mama asiye na mume na nina wavulana wanne. Ndugu mmoja Mkristo alipendezwa na mmoja wao, na sasa mwana huyo anajiweka tayari kubatizwa karibuni sana. Inathaminiwa sana wakati mtu fulani anaposaidia wasio na baba.

P. T., Marekani

Chile Ndiyo sasa tu nimesoma lile toleo la Mei 8, 1994, na nilifurahia hasa ile makala “Chile—Nchi Isiyo na Kifani, Mkusanyiko Usio na Kifani.” Nilihisi kama nilikuwa nimehudhuria mkusanyiko huo mimi mwenyewe. Hata nilihisi hali ya kutotaka kuondoka programu ilipokwisha.

K. K., Japani

Diski-Songamano Asanteni kwa makala yenu “Diski-Songamano—Hiyo Ni Nini?” (Aprili 22, 1994) Ilifumbua lile fumbo katika akili yangu kuhusiana na diski hizi. Baada ya kusikiliza mfumo wa diski-songamano wa rafiki, nilistaajabia ubora wayo upitao mifumo mingine ya kutolea muziki.

S. D., Nigeria

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki