Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g94 9/22 uku. 30
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
  • Amkeni!—1994
  • Habari Zinazolingana
  • Tule Muhogo!
    Amkeni!—1993
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
    Amkeni!—1994
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
    Amkeni!—1995
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
    Amkeni!—1995
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1994
g94 9/22 uku. 30

Kutoka kwa Wasomaji Wetu

Talaka Nilipokuwa nikisoma “Maoni ya Biblia . . . Mungu Huchukia Talaka ya Aina Gani?” (Februari 8, 1994), niliguswa sana. Baada ya kupata talaka hivi majuzi tu baada ya miaka 20 ya ndoa kwa mwenzi asiye mwaminifu, niling’amua kwamba Yehova hachukii uamuzi wangu wa kutaliki na si lazima nijihisi mwenye hatia. Ni kweli, hisia za kushuka moyo, upweke, na hatia zaweza ‘kutokea ghafula.’ Lakini kupita kwa wakati na kutegemea Yehova ni viponyeshaji.

B. M., Marekani

Wakati wa ndoa yangu mume wangu alipinga sana kuwa kwangu mmoja wa Mashahidi wa Yehova. Hatimaye alihama kukaa na msichana rafiki yake na kuandikisha talaka. Nilihisi kwelikweli kwamba Mungu alikuwa ‘ameniita katika amani.’ (1 Wakorintho 7:15) Mvunjiko huo ulivuruga sana watoto wangu, na miaka hiyo iliyopita nilisoma mara nyingi Malaki 2:16 na kujiuliza kama nilifanya sawa. Makala yenu imenisaidia nipate maoni yenye usawaziko juu ya andiko hili.

J. C., Marekani

Kuhama Nilishukuru ajabu kupokea makala zenu “Vijana Huuliza . . .” kuhusu kuhama. (Februari 22, 1994, na Machi 8, 1994) Nina miaka 16 na niko karibu kuhamia mbali kutoka kwa rafiki zangu wote wa karibu. Nilikuwa nikilia kila usiku, nikiona ni laiti kungekuwa na njia fulani ya kuniwezesha kukaa. Ndipo nikasoma makala zenu. Niliamua kuanza kuwa na maoni chanya zaidi juu ya kuhama. Ingawa bado nahuzunika kwa kulazimika kuhama, mtazamo wangu umepata maendeleo sana.

A. D., Marekani

Makala hizo ndizo hasa nilizohitaji. Ushauri bora zaidi uliotolewa ulikuwa kutembea kwa utaratibu katika kawaida ileile kwa habari ya mambo ya kiroho. Nililazimika kung’amua kwamba hata nihamie wapi, sikuzote Yehova atakuwa huko. Basi mbona nisipate kumjua kindani kupitia funzo la kibinafsi lenye kina? Kufanya hivyo kulisaidia sana kunituliza katika makao yangu mapya.

T. T., Marekani

Kutojua Kusoma na Kuandika Mara nyingi nimetaka kuwaandikia na kuwashukuru baada ya kusoma makala fulani ya kupendeza. Lakini ule mfululizo “Kushinda Tatizo la Kutojua Kusoma na Kuandika” (Februari 22, 1994) mwishowe umenisadikisha kufanya hivyo. Juma lijalo nitaanza funzo la Biblia na bibi mmoja asiyejua kusoma au kuandika. Sikujua ningefanyaje hivyo, lakini sasa najua, kwa msaada wa makala hizi. Zilifika kwa wakati ufaao!

M. A. C., Italia

Majiji Nina miaka 17 na nimetumia miaka 14 ya kwanza ya maisha yangu katika New York City. Kwa hiyo nilifurahia sana makala zenu juu ya majiji makubwa. (Januari 8, 1994) Nilipenda mafumbo ya kujaza maneno yaliyokuwamo (katika Kiingereza).

S. H., Marekani

Muhogo Ile makala “Tule Muhogo!” (Novemba 8, 1993) ilikuwa ya kupendeza sana. Nikiwa Mnigeria, nimo miongoni mwa mamilioni ya Waafrika wafurahiao sana muhogo, hasa fufu na gari. Kwa kweli, naweza kumshukuru Muumba wetu kwa kufanya muhogo upatikane kwetu. Bila huo, mamilioni ya Waafrika wangetokomea.

O. N. Y. I., Nigeria

Mishonari Mwenye Moyo Mkuu Niliguswa sana na ono la Annama Abraham katika hadithi yake “Kuishinda Miito Migumu ya Maisha Katika Asia ya Kusini.” (Januari 22, 1994) Alifiwa na mume wake mpendwa lakini aendelea kumtumikia Yehova kwa uaminifu-maadili. Nataka kumwambia hadithi ya maisha yake ilinitia moyo sana.

I. I. C. S., Brazili

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki