Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g93 11/8 kur. 25-27
  • Tule Muhogo!

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Tule Muhogo!
  • Amkeni!—1993
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Ni Rahisi Kuukuza
  • Kuutayarisha ni Kazi Ngumu
  • Wakati wa Mlo!
  • Majani ya Muhogo—Chakula cha Kila Siku cha Mamilioni
    Amkeni!—1996
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
    Amkeni!—1994
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
    Amkeni!—1997
  • Kuutazama Ulimwengu
    Amkeni!—1998
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1993
g93 11/8 kur. 25-27

Tule Muhogo!

Na mleta habari za Amkeni! katika Nigeria

AKIWA na upanga mkononi, Janyere akata njia ya kupitia shamba lililomea sana muhogo. Kofia ya nyasi yamkinga kutokana na jua kali sana la ikweta. Akichagua mmea mmoja wenye kimo cha meta tatu, ashika shina kwa mikono miwili na kung’oa kwa uanana. Mizizi na mihogo yatokea ndani ya ardhi. Aikata kwa upanga na kuiweka katika sinia bapa pamoja na mihogo mingine aliyotoka tu kung’oa. Ngozi, mke wake, achukua sufuria hiyo aiweka juu ya kichwa chake, na pamoja waanza safari ya kwenda nyumbani.

Mamilioni ya watu kotekote sehemu za tropiki ambao hufurahia kula muhogo wajua sana njia hiyo sahili ya kuvuna.a[1] Katika Afrika pekee watu wapatao milioni 200 hutegemea muhogo kwa zaidi ya nusu ya kalori wanaokula kila siku.[2] Na unaendelea kupendwa. Wastadi fulani wasema kwamba kufikia mwaka wa 2000, idadi ya watu wanaotegemea muhogo huenda ikashinda kwa mara mbili idadi ya wale walioutegemea katika miaka ya katikati ya 1980.[3]

Je! umepata kula muhogo? Kama unaishi katika eneo la dunia lisilo la kitropiki, huenda ukasema bado. Lakini usiwe na uhakika sana! Wanga wa muhogo ni sehemu ya maana katika michuzi, rojorojo, vyakula vya watoto, haradali, vyakula vinavyotengenezwa kutokana na tapioka, vitu vya kutia uzito kwa chakula, vitu vitamu, na mikate.[5] Hata nyama unayokula au maziwa unayokunywa huenda yatoka kwa wanyama ambao wamelishwa unga wa muhogo ukiwa sehemu ya lishe yao.[6]

Kwa kuongezea mchango wao kwa vyakula mbalimbali, muhogo hutumika pia katika kutengeneza gundi, gamu, na rangi.[7]

Ni Rahisi Kuukuza

Lakini kwa Waafrika wengi, kama akina Janyere na Ngozi, muhogo hukuzwa ili uliwe. Inga-wa hauna protini nyingi, muhogo una wanga mwingi sana. Ukilinganishwa kwa kipimo sawa, muhogo una kalori mara mbili na nusu zaidi ya mahindi au kiazi-kikuu, vyakula vingine viwili vya maana vinavyofuata vya Afrika.[10] Miche yake na majani yake hufaa kwa chakula—huwa na vitamini nyingi, madini mengi, na protini nyingi.[11]

Jambo kubwa lifanyalo muhogo uwe wenye umaana ni kwamba ni rahisi sana kuukuza. Hakuna matayarisho mengi ya ardhi yanayohitajika, ila tu kuondoa vichaka na mimea itambaayo na kuhakikisha kwamba kuna mwangaza. Udongo unapokuwa na unyevu, mkulima apanda mashina yaliyokatwa ambayo muhogo utamea kutokana nayo.[12] Hauhitaji kupaliliwa sana, na huo hauhitaji mbolea nyingi, dawa za kuua ukungu, au za kuua wadudu au hata waweza kukua bila dawa hizo.[13] Pia waweza kuvunwa wakati wowote mwakani.[14]

Muhogo ni mvumilivu kwa njia ya kustaajabisha sana. Hukua vema kwenye udongo mzuri na udongo mbaya vilevile.[15] Hukua vizuri kwa mwinuko wa usawa wa bahari hadi mwinuko wa meta 2,000.[16] Hukua sana katika maeneo yenye mvua nyingi sana, na tena hufanya vizuri katika hali zisizokuwa na mvua kwa miezi tisa ya mwaka.[17] Hata moto ukiuchoma kabisa, muhogo utachipuka upya kutoka kwenye msingi wao![18]

Kuutayarisha ni Kazi Ngumu

Kwa hiyo kutokea wakati unapopandwa hadi unapovunwa, muhogo hauna kazi nyingi ukilinganishwa. Lakini, mara unapotoka ardhini ndipo kazi kubwa huanza. Kwa kweli, kazi ihusikayo kutokea kuvunwa hadi mlo yaweza kufikia au hata kupita kazi zote za kabla ya kuvunwa.[19]

Ni lazima kazi hiyo ianze haraka. Kama angetaka, Janyere angeweka mihogo ikiwa akiba kwa muda ufikao miaka miwili kwa kuiacha tu ardhini bila kuguswa. Lakini mara inapong’olewa, ni lazima mihogo itayarishwe kwa muda wa saa 48 ama itaanza kuoza.[20]

Ngozi ataka kutayarisha gari, chakula kipendwacho cha Wanigeria. Kwanza aambua muhogo kwa kisu; kisha auosha. Kisha Ngozi na Janyere wapeleka muhogo ulioambuliwa kwa rafiki yao Alex ambaye ana kisaga. Kisaga hicho huponda-ponda mihogo hiyo iwe mseto. Kisha mseto huo wawekwa ndani ya gunia lenye matundu, na umaji-maji wao kukamuliwa katika chombo cha Alex cha kukamua umaji-maji kutoka kwenye mseto.

Lakini kazi bado haijaisha! Kisha ni lazima mseto wa muhogo ukaushwe kwa siku kadhaa. Kisha Janyere aichunga kwa kichungio cha chane. Baada ya hapo, Ngozi aikaanga, akiipindua-pindua kwa sahani ya mbao ili isichomeke. Mohogo, ukiwa umefika kwenye hatua hii ya kutayarishwa, sasa waitwa gari.

Ingawa Ngozi amechagua njia moja tu kati ya njia nyingi za kutayarisha mihogo, mihogo mingi katika Afrika hutayarishwa na wanawake nyumbani.[21] Si vizuri kutumia njia za mikato kwa sababu muhogo huwa na viwango vidogo vya sianidi, ambayo ni sumu kali sana kwa wanadamu na wanyama. Matayarisho makubwa sana hupunguza kiwango cha sianidi kwa kadiri ambayo haiwezi kudhuru.[22]

Wakati wa Mlo!

Hatimaye, sasa ni wakati wa mlo! Gari, iliyochanganywa na tui (maziwa ya nazi), ni chakula kitamu cha kumalizia mlo. Yaweza kutengenezwa pia kuwa biskuti. Lakini badala ya hizo, Ngozi na Janyere waamua kula eba, itayarishwayo kwa kukoroga tu gari ndani ya maji moto.

Kotekote katika Afrika milo ya mihogo hutofautiana sana kama vile majina ya milo hiyo inavyotofautiana. Katika Côte d’Ivoire hiyo huandaliwa pamoja na nyama na mboga ikiwa attieke. Nchini Ghana, muhogo uliochanganywa na mchuzi wa samaki au wa mayai huwa chakula kimoja kiitwacho garifoto. Nchini Tanzania, unapoomba ugali, utapewa ugali wa muhogo na supu. Nchini Kameroon, watu hufurahia kumkum. Na katika Sierra Leone, hasa siku za Jumamosi, wapenda muhogo husisitiza kula foofoo![23]

Hata uuite nini, muhogo una fungu kubwa katika maisha ya Kiafrika. Kwa kweli ni fungu kubwa sana hivi kwamba watu wengi huhisi kwamba kama hawajala muhogo, hata kama wamekula chakula kingine, kwa kweli bado hawajala chochote!

[Maelezo ya Chini]

a Pia huitwa manioka, tapioka, na yuka.[4]

[Picha katika ukurasa wa 26]

Kuambua na kuosha muhogo

Kusaga

Kuchunga

Kukaanga

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki