Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g96 7/8 kur. 20-21
  • Majani ya Muhogo—Chakula cha Kila Siku cha Mamilioni

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Majani ya Muhogo—Chakula cha Kila Siku cha Mamilioni
  • Amkeni!—1996
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Onja Ngunza Kidogo
  • Je, Utaonja Ngukassa au Kanda Kidogo?
  • Tule Muhogo!
    Amkeni!—1993
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
    Amkeni!—1997
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
    Amkeni!—1994
  • Siagi ya Karanga Mtindo wa Kiafrika
    Amkeni!—1999
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1996
g96 7/8 kur. 20-21

Majani ya Muhogo—Chakula cha Kila Siku cha Mamilioni

NA MLETA-HABARI WA AMKENI! KATIKA JAMHURI YA AFRIKA YA KATI

MAMBO yote yalianzia karibu na mwaka 1600, wakati Wareno walipoleta muhogo Afrika kutoka Amerika Kusini. Muhogo unaaminiwa ulianzia Brazili kwa sababu neno (la Kiingereza) “manioc” lilitokana na makabila ya Tupia ya Brazili katika Bonde la Amazon.

Muhogo unathaminiwa sana na Waafrika, lakini vipi juu ya majani yao ya rangi ya kijani chenye kiwi? Wengine huyatumia yakiwa dawa ya vidonda au kutibu tetekuwanga. Hata hivyo, kwa mamilioni katika Jamhuri ya Afrika ya Kati na katika nchi nyinginezo kadhaa za Afrika, majani hayo ni chakula cha kila siku, kwa kuwa hiyo yaweza kupikwa kuwa chakula kitamu. Hata mojayapo maneno ya kwanza ambayo mishonari wapya wa Watch Tower hujifunza ni ngunza. Hiyo ni mtokoto mtamu wa kisamvu na ndiyo chakula kikuu cha Jamhuri ya Afrika ya Kati—chakula ambacho mgeni azuruye Afrika ya kati ni lazima aonje.

Wazungu wengi wanaoishi Afrika hawataki kamwe kuonja mlo uliotayarishwa kwa kisamvu, kwa kuwa wao wanakiona kuwa chakula cha wenyeji, si cha watu wa nchi za kigeni. Lakini ni yapi mambo ya hakika? Katika nchi kama Jamhuri ya Afrika ya Kati, Sierra Leone, na Zaire, majani haya ni chakula cha kila siku kwa familia nyingi.

Unaposafiri kwa ndege au kwa njia nyingine ukivuka Jamhuri ya Afrika ya Kati, wewe waona nchi maridadi ya kijani kibichi—miti, vichaka, nyanda za nyasi, na, katikati mna mashamba madogo ya mihogo yenye rangi ya kipekee ya kijani chenye kiwi. Kila kijiji kidogo kimezingirwa na mashamba madogo ya muhogo. Watu hukuza muhogo kando ya nyumba zao, na hata katika jiji kuu, Bangui, utapata muhogo katika kila shamba dogo na kanda za ardhi kando ya nyumba kubwa au kandokando ya barabara kuu. Hakika, huo ni chakula muhimu katika sehemu hii ya ulimwengu.

Onja Ngunza Kidogo

Mishonari wapya wafikapo, upesi wao hualikwa na marafiki wao waje waonje ngunza kidogo. Huo ni mlo unaotia ndani chakula maarufu cha kisamvu. Wanawake wenyeji wanajua namna ya kuipika iwe tamu. Yaonekana kila mwanamke ana njia yake mwenyewe ya kuipika. Mojayapo mambo ya kwanza ambayo wasichana wadogo hujifunza kutoka kwa mama zao kuhusu upishi ni jinsi ya kupika ngunza.

Wao huona fahari wakieleza ngunza ni nini na jinsi ya kuipika. Wanawake hufurahi ukionyesha kupendezwa na chakula chao cha kienyeji. Kwanza, watakuambia kwamba majani ya muhogo si ghali nayo hupatikana kwa wingi na kwamba unaweza kuyachuna katika majira ya mvua na majira ya ukavu vilevile. Nyakati za matatizo ya kiuchumi na infleshoni, kisamvu hutimiza fungu kubwa katika kulisha familia. Na tafadhali kumbuka kwamba familia za Kiafrika huwa kubwa. Kuna wengi sana wanaohitaji kula. Kupika ngunza huchukua muda wa saa kadhaa. Ni lazima kisamvu iondolewe ukali wayo kabla ya kuliwa. Ukali huo huondolewa kwa upishi wa kidesturi, unaotia ndani kusagwa na kuchemshwa sikuzote.

Mafuta ambayo wanawake Waafrika hupendelea kutumia katika kupika ngunza ni mawese. Mafuta hayo yenye rangi nyekundu yenye kiwi ni lazima yatumiwe. Ngunza pamoja na siagi ya njugu na labda kitunguu na kitunguu saumu ni chakula cha kila siku cha familia. Lakini namna gani ikiwa unatarajia wageni? Basi, ngunza lazima iwe kitu cha kipekee, kitu ambacho watakumbuka. Basi, mwenyeji ataongeza kiungo akipendacho zaidi—samaki au vipande vya nyama vilivyokaushwa kwa moshi—pamoja na vitunguu na vitunguu saumu vingi pamoja na siagi nyingi ya njugu iliyotoka kutengenezwa nyumbani. Vyote hivyo vyawekwa katika nyungu moja. Sasa mambo yabakiyo ni subira na kuchemsha kwingi.

Leo, mwenyeji wetu atatupikia ngunza kwa wali. Rundo la wali lililomwagiwa ngunza moto ya vijiko viwili hufurahisha sana Waafrika na watu wengi wa nchi za kigeni pia. Ongeza pilipili kidogo, na basi sasa watambua ngunza. Pamoja na mlo huo, divai nyekundu katika gilasi hutokeza ladha halisi.

Je, Utaonja Ngukassa au Kanda Kidogo?

Usafiripo kutoka mashariki hadi magharibi katika nchi hiyo, utapata kwamba watu hupika ngunza kwa njia mbalimbali. Lakini namna gani ngukassa? Katika siku baridi yenye mvua, ngukassa, ambayo ni mchuzi au mtokoto wa kila kitu kikuzwacho shambani, yaweza kuwa ndicho kitu chenye kufaa zaidi. Mawese, ndizi, njugu, viazi vitamu, mahindi, na bila shaka, kisamvu kidogo vyote hupikwa pamoja, lakini chumvi haiwekwi—hata kidogo. Hiyo ndiyo siri! Matokeo ni chakula kitamu na chenye lishe. Unaposafiri safari ndefu, beba kanda kidogo. Hiyo imefanyizwa kwa kisamvu iliyopondwa pamoja na samaki au nyama iliyokaushwa kwa moshi. Kanda hupikwa kwa kufunika mchanganyiko huo kwa majani ya muhogo na kukaushwa kwa moshi kwa muda wa saa kadhaa mpaka iwe ngumu na kavu. Hiyo hukaa kwa siku kadhaa nayo yaweza kuliwa pamoja na mkate. Hiyo yawafaa sana wasafiri.

Ukizuru Afrika wakati wowote, mbona usiombe kisamvu? Uionje, ukajiunge na mamilioni yanayoifurahia!

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki