Kutoka kwa Wasomaji Wetu
Vijana Waaminifu Niliguswa moyo na ule mfululizo “Vijana Ambao Hutanguliza Mungu.” (Mei 22, 1994) Nilipokuwa tineja, nilikuwa na uvimbe wa ubongo. Nikiwa mmoja wa Mashahidi wa Yehova, niliwaambia madaktari: “Sitaki kutiwa damu mishipani.” Ingawa agizo la mahakama lilitolewa ili kunilazimisha nitiwe damu, upasuaji huo uliendelea vizuri bila ya hiyo. Nilipokuwa nikisoma juu ya watumishi wachanga hawa wa Mungu, nilikuwa na machozi machoni. Walikuwa wamepitia lilelile kama mimi! Visa vyao vimegusa moyo wangu na kuimarisha upendo wangu kwa Mungu.
M. P., Marekani
Nina umri wa miaka 17 na nimekuwa na hofu ya kujipata katika hali kama hiyo siku moja. Kufa hakunitishi mimi, lakini lile wazo la kupuuza sheria za Yehova hunitisha. Lingekuwa jambo baya sana kuridhiana chini ya mbano. Makala hiyo ilinipa nguvu nyingi.
C. K., Ujerumani
Niliposoma makala hizo, singeweza kuzuia machozi. Baadaye, nilisoma kwa makini sana kile kijitabu Damu Yaweza Kuokoaje Uhai Wako? (kilichochapishwa na Watchtower Society). Sasa najua jinsi ya kutenda iwapo nitakuwa katika hali kama hiyo.
Y. G., Ujerumani
Kwa kuwa mimi ni mgonjwa wa aina ya leukemia isiyopona, yale maono ya walio wachanga waliothibitisha ujitoaji wao kwa Yehova yalikuwa yenye kutia moyo sana kwangu nikiwa mtu mzima. Shukrani nyingi.
H. K., Austria
Nina umri wa miaka 18. Nilisisimuliwa na kutetemeshwa niliposoma makala hizo jana. Singeweza kuacha kulia nilipokuja kuona kwamba watoto hawa waaminifu walikufa. Imani yao ilinifanya kujiuliza kama naweza, chini ya hali kama hizo, kudumisha uaminifu wangu wa maadili.
E. A. O., Nigeria
Hakika nilipigwa na uimara usioshindika wa vijana wote waliotajwa. Baada ya kuzisoma makala hizo, nililia sana na kushukuru Yehova kwamba aliwapa nguvu kukabili magumu hayo hadi kifo chao. Naweza kusema kwa moyo mweupe kwamba matatizo yangu ya utineja si chochote kwa kulinganisha.
R. C., Italia
Ni wazi kwamba makala hizi zenye kuvuta sana zitatia moyo vijana wote wazisomao. Vijana wote hawa walikuwa imara katika katao lao la damu; wakati uleule, wangeweza kujifahamu na kujieleza kwa wazi. Nilitiwa moyo kujua hata kuje misongo na majaribu yawayo yote, Yehova hatashindwa kutupa sisi nguvu na msaada uhitajikao.
R. T., Japani
Kutojua Kusoma na Kuandika Nilithamini ule mfululizo “Kushinda Tatizo la Kutojua Kusoma na Kuandika.” (Februari 22, 1994) Nilipokimbia kutoka China hadi Afrika Kusini katika miaka ya 1950, nilikuwa siwezi kusema yoyote ya lugha zisemwazo huku. Hata hivyo, Mashahidi wa Yehova kwa subira walinisaidia kuelewa Biblia katika Kiingereza. Nilihudhuria mikutano yao pia, kutia ndani Shule ya Huduma ya Kitheokrasi. Polepole Kiingereza changu kiliboreka, na sasa nina uhakika katika huduma ya mlango kwa mlango.
W. W., Afrika Kusini
Kuzaliwa Upya Katika Mwili Mwingine Ingawa mimi ni Mwislamu, mimi ni msomaji wa kawaida wa Amkeni! Ningependa kueleza shukrani zangu za moyo mweupe kwa mfululizo wenu wa majuzi “Je! Umepata Kuishi Awali? Je! Utaishi Tena?” (Juni 8, 1994) Niliipata kuwa yenye kuarifu sana. Kwa muda mrefu nimekuwa nikitafuta habari ambayo ingeweza kutumiwa kurekebisha baadhi ya marafiki wangu ambao husisitiza juu ya kuwapo kwa kuzaliwa upya katika mwili mwingine. Nikiwa na habari iliyotolewa, ninaamini hakika watakubali kwamba kwa sababu kuna ufufuo, hakuwezi kuwa na kuzaliwa upya katika mwili mwingine.
K. S., Nigeria