Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g95 5/22 kur. 24-26
  • Namna Gani Ikiwa Mzazi Wangu Hatimizi Matakwa ya Kimungu?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Namna Gani Ikiwa Mzazi Wangu Hatimizi Matakwa ya Kimungu?
  • Amkeni!—1995
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Kinachomaanishwa Hasa na Kuwaheshimu
  • Kushughulika na Hasira na Uchukizo
  • ‘Naweza Kumbadili’
  • Kutimiza Wokovu Wako Mwenyewe
  • Nini Ikiwa Mzazi Wangu ni Mraibu wa Dawa za Kulevya au Pombe?
    Maswali Ambayo Vijana Huuliza—Majibu Yafanyayo Kazi, Buku la 2
  • Nishughulikeje na Mzazi Wangu Aliyeondoka Nyumbani?
    Amkeni!—1992
  • Naweza Kumsaidiaje Mzazi Wangu Aliye Peke Yake?
    Amkeni!—1992
  • Naweza Kuishije Katika Nyumba Iliyogawanyika Kidini?
    Amkeni!—1992
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1995
g95 5/22 kur. 24-26

Vijana Huuliza...

Namna Gani Ikiwa Mzazi Wangu Hatimizi Matakwa ya Kimungu?

“Baba yangu amekuwa Mkristo kwa miaka kumi. Lakini hatendi. Yeye hajifunzi Biblia, na hahudhurii mikutano kwa ukawaida. Daima huwalaumu ndugu zake wa Kikristo kutanikoni. Na ana maoni ya kilimwengu kuhusu jamii mbalimbali na habari nyingine nyingi sana. Mimi namfikiria kuwa mnafiki.”—Msichana fulani tineja.

Hakuna mzazi aliye mkamilifu. “Kwa sababu wote wamefanya dhambi, na kupungukiwa na utukufu wa Mungu,” yasema Biblia. (Warumi 3:23) Lakini ni hali tofauti kabisa mama ama baba wa mmoja anapotenda kama kielelezo cha Kikristo cha kufuatwa anapokuwa hadharani na kuchukua mbadiliko usiofaa akiwa faraghani. “Akiwa miongoni mwa wengine, baba yangu ni mzuri,” asema msichana mmoja mchanga. “Lakini yeye ni mtu tofauti akiwa faraghani—yeye ni mwenye matata! Yeye huchambua lolote nifanyalo, na humfanya kila mmoja katika familia ajihisi vibaya. Niko katika hatua ambapo siwezi kupata shangwe maishani. Kile ninachohisi kumhusu ni chuki.”

Ghadhabu na uchukizo waweza hasa kuwa mwingi miongoni mwa vijana ambao kwa usiri wateseka na aina mbalimbali za kutendewa vibaya. Basi mwanamke aitwaye Mary aandika hivi kuhusu “jeuri, uchafuliwaji, na kutendewa vibaya kwa aina zote” ambako aliteseka kutoka kwa babaye—mraibu wa alkoholi wa faraghani. “Watu wangetufikia sisi watoto na kutuambia kwamba tulikuwa na baba wa ajabu na jinsi tulivyobarikiwa,” kwa huzuni akumbuka.

Biblia hushutumu aina zote za unafiki. (Yakobo 3:17) Inatuonya kwamba hata miongoni mwa waabudu wa kweli wa Mungu, kungekuwa na wengine ambao “huficha kile walicho.” (Zaburi 26:4, NW; linganisha Yuda 4.) Hata hivyo, kujua hili huenda kusifanye mambo yawe rahisi kamwe, wakati mmoja anayezoea unafiki ni mzazi wako mwenyewe—mmoja ambaye unapaswa kumpenda na kumstahi. Vijana wengine wanashindwa na hisia-moyo zenye kugongana ambazo hutokea. “Nahitaji msaada,” akalalama msichana mmoja mchanga. “Biblia husema ‘mheshimu babako,’ lakini siwezi.”

Kinachomaanishwa Hasa na Kuwaheshimu

Ni kweli kwamba Biblia huamuru kuheshimu wazazi wa mmoja huwa hakuna ‘kihepeo’ kwa vijana wanaohisi wazazi wao hawastahili. (Waefeso 6:1, 2) Hata hivyo, kuheshimu mzazi si lazima kumaanishe kwamba unakubali mtindo-maisha wake ama unafurahia vile anavyokutendea. Katika Biblia, “kuheshimu” kwa usahili kwaweza kumaanisha kufahamu ifaavyo mamlaka ihusikayo.

Kwa mfano, mtume Petro aliandika kwamba Wakristo wapaswa ‘kuheshimu mfalme.’ (1 Petro 2:17) Petro alijua vizuri sana kwamba wafalme mara nyingi walikuwa na tabia zenye kuchukiza. Kwa kielelezo, Mfalme Herode Agripa 1, alikuwa mwanamume mtumia mali vibaya na mwenye kupuuza mambo. Baada ya kuwekwa rasmi na Roma kuwa mfalme wa Palestina, alianzisha mnyanyaso dhidi ya Wakristo. “Akamwua Yakobo, ndugu yake Yohana, kwa upanga. Na akiona ya kuwa imewapendeza Wayahudi akaendelea akamshika na Petro.” (Matendo 12:1-3) Hata hivyo, Petro hakuhimiza uasi. Badala yake aliendeleza utii kwa wafalme. Na alifanya hivyo kwa sababu nzuri. Utii kwa wafalme wa kilimwengu ni mapenzi ya Yehova. Na katika siku ya Petro baadhi ya wafalme walikuwa na uwezo na mamlaka kamili. Sulemani alisema hivi: “Maana yeye hufanya lo lote limpendezalo. Kwa kuwa neno la mfalme lina nguvu; naye ni nani awezaye kumwambia huyo, Wafanya nini?”—Mhubiri 8:3, 4.

Katika njia inayofanana na hiyo, mzazi wako—hata pungukio liwe lipi—bado yeye ndiye msimamizi na ana uwezo wa kadiri juu ya maisha yako. Basi, si mwendo wa hekima, kumwasi ama kumtendea kwa kumdharau. Si kwamba tu kufanya hivyo kutafanya maisha yawe magumu kwako bali pia kungeweza kusababisha ukose ukubali wa Mungu. (Linganisha Mithali 30:17; Mhubiri 10:4.) Kwa upande ule mwingine, kushirikiana kwa kadiri uwezavyo kwaweza kusaidia kudumisha angalau amani na utulivu wa kadiri katika uhusiano wako na wazazi wako.—Wakolosai 3:20.

Kushughulika na Hasira na Uchukizo

Ni jinsi gani, basi, uwezavyo kushughulika kwa staha na mmoja ambaye amekuumiza kihisia-moyo na kukuvuruga hisia? Jambo hili si rahisi. Lakini kudumu katika makosa na mapungukio yake kutakuza uchukizo wako tu. Yawezekana kwamba unahitaji kufikiri kwa uchanya zaidi kuelekea mzazi wako, ukimsifu kwa sifa zozote nzuri ambazo huenda akawa nazo?

Ona vile Mithali 19:11 husema: “Busara ya mtu huiahirisha hasira yake.” Kujaribu kufahamu mzazi wako kwaweza kukupa mtazamo wa akili mpya kuhusu hali. Je, anafanya hivyo kwa kuwa mwovu tu? Ama yaweza kuwa ni mdhaifu tu, amevunjika moyo, na anahitaji msaada? Je, tabia yake yaweza kuwa ni tokeo la ugonjwa fulani, kushuka moyo, upweke, ama mkazo wa kazi? Ikiwa ndivyo, kufahamu matatizo haya kwaweza kukusaidia uhisi huruma zaidi kuelekea mzazi wako na labda kuwa na hasira kidogo.

Vyovyote viwavyo, inasaidia unapozungumza kuhusu hisia zako na mtu mwingine. (Mithali 12:25) “Baba yangu alikuwa anakunywa kileo kingi,” akumbuka msichana mmoja. “Singeweza kuambia wazazi wangu jinsi nilivyohisi, hivyo niliepuka kuonyesha hisia zangu kwa yeyote.” Hata hivyo, hupaswi kuteseka peke yako. Ingawa hawabadilishi wazazi, watu waliokomaa katika kutaniko la Kikristo wanaweza kufanya mengi ili kujazia ukosefu wowote wa utunzi nyumbani. (Linganisha Marko 10:30.) Mithali 17:17 husema hivi: “Marafiki sikuzote huonyesha upendo wao. Ndugu ni wa nini ikiwa si kushiriki matatizo?”—Today’s English Version.

‘Naweza Kumbadili’

Vijana wengine huteseka kihisia-moyo kwa sababu ya kuwa na hisia yenye kupotoka kwamba wana daraka. Ajikumbuka Mary na ndugu zake: “Tuliishi kwa hofu kubwa kwamba mtu fulani angegundua tatizo la baba la uraibu la alkoholi.” Wengine hujichosha kwa kufanya majaribio yasiyofua dafu ili kubadili mzazi wao mwasi.

Kadiri unavyoweza kumpenda na kumtunza mzazi wako, kwa kweli hupaswi kulaumiwa kwa mapungukio yake. Yeye ‘alichukua furushi lake’ la daraka mbele za Mungu. (Linganisha Wagalatia 6:5; Yakobo 5:14.) Si daraka lako kuangalia ama kudhibiti mwenendo wa mzazi wako. Kumdharau ama kumkemea mzazi wako kila wakati kutamkasirisha tu.

Hili halimaanishi huna lolote uwezalo kufanya. Angalau, unaweza “kuomba bila kukoma” kwamba mzazi wako apate mabadiliko ya moyoni. (1 Wathesalonike 5:17) Kwa kawaida kumwonyesha upendo na kumsifu kwa moyo mweupe, inapofaa, kwaweza kusaidia kulainisha mtazamo wake. Zaidi ya hilo, jambo pekee unaloweza kufanya ni kuvumilia hali kadiri uwezavyo.a

Bila shaka, ikiwa wewe pamoja na mzazi wako ni Wakristo na anafanya kosa zito, kama vile utumiaji mbaya wa alkoholi ama mifoko ya hasira, kwa kawaida utahisi kushurutika kuhakikisha mambo yamezungumzwa na wazee wa kutaniko. (Yakobo 5:14) Hili halingekuwa tendo la kukosa uaminifu mshikamanifu bali lingekuwa jaribio la upendo kuona kwamba mzazi wako anapata usaidizi wa msingi ahitajio. Ni kweli kwamba, wazazi wengine kwa hasira wamekataa utendaji makosa wowote na kutokeza kisasi kwa usiri, lakini wale vijana ‘wanaoteswa kwa sababu ya haki’ kwa upande huu wanaweza kuwa na uhakika kwamba Yehova akubali mwendo wao wa ujasiri na kwamba kwa wakati wake, atauweka ukweli wazi.—1 Petro 3:14; 1 Timotheo 5:24, 25.

Kutimiza Wokovu Wako Mwenyewe

Sulemani alisema hivi: “Jeuri [“uonevu,” NW] humpumbaza mwenye hekima.” (Mhubiri 7:7) Inasikitisha kusema kwamba, baadhi ya vijana wamekuwa na huzuni kwa sababu ya kielelezo kibaya cha mzazi wao nao wameanza kufanya isivyofaa. Wengine hata wamekuwa na hasira dhidi ya Mungu na wameacha njia ya Kikristo! (Mithali 19:3) Biblia yaonya hivi: “Basi ujitunze, isije hasira ikakuvuta hata ukafanya mzaha. Jitunze, usiutazame uovu.”—Ayubu 36:18-21.

Badala ya kufadhaika kupita kiasi kuhusu msimamo wa mzazi wako pamoja na Mungu, unahitaji ‘kutimiza wokovu wako mwenyewe kwa kuogopa na kutetemeka.’ (Wafilipi 2:12) Katika nyakati za kale, mwanamfalme mchanga aliyeitwa Hezekia alifanya hivyo chini ya hali zinazofanana na hizo. Baba yake, Mfalme Ahazi, alidai kuwa mwabudu wa Yehova. (Isaya 7:10-12) Kwa hakika alikuwa mwabudu wa vijimungu vya kipagani, akitoa wana wake mwenyewe kuwa dhabihu ya kibinadamu! (2 Wafalme 16:1-4) Ebu wazia jinsi uasi imani huu ulivyokuwa wenye kuumiza kwa Hezekia mchanga! Zaburi 119:28, ambayo wengine huamini iliandikwa na mwanamfalme huyu mchanga, yasema hivi: “Nafsi yangu imeyeyuka kwa uzito, unitie nguvu sawasawa na neno lako.”

Yehova alifanya hivyo hakika! Hezekia alipojitoa mwenyewe kwa sala na kujifunza Neno la Mungu, hali yake ya kiroho ikakua ijapo mazingira yake. (Zaburi 119:97) Pia kwa umakini alilinda ushirika wake. (Zaburi 119:63) Na tokeo likawa nini? Licha ya kielelezo chenye kusikitisha kilichowekwa na baba yake mnafiki, Hezekia mwenyewe “alishikamana na BWANA.” (2 Wafalme 18:6) Ndivyo nawe! Yawezekana kuwa mzazi wako anatenda kwa unafiki, lakini huhitaji kumshabihi. Endelea kushikamana na Yehova, na labda kielelezo chako kitulivu cha uaminifu kitamsukuma mzazi wako abadilike.

[Maelezo ya Chini]

a Hili halimaanishi kwamba vijana lazima wavumilie kutendewa vibaya kimwili au kingono. Kijana akiwa katika hali kama hiyo apasa kutafuta msaada, hata ikiwa itamaanisha kutoka nje ya familia ili kuupata.

[Picha katika ukurasa wa 25]

Hupaswi kukosa kutimiza matakwa ya Mungu kwa sababu mzazi wako hatimiziy

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki