Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g95 7/8 kur. 5-7
  • Ni Yapi Baadhi ya Hayo Matatizo?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Ni Yapi Baadhi ya Hayo Matatizo?
  • Amkeni!—1995
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Wakati Mazungumzo Yanapokoma
  • Kielelezo Chako Chaweza Kufanyiza Tofauti
  • “Uchangamfu kwa Maisha Zetu”
  • Kuishi Pamoja kwa Upendo
    Amkeni!—1995
  • Ninawezaje Kusitawisha Uhusiano wa Karibu Pamoja na Babu na Nyanya?
    Amkeni!—2001
  • Kwa Nini Niwajue Vyema Babu na Nyanya?
    Amkeni!—2001
  • Babu na Nyanya—Shangwe na Magumu Yao
    Amkeni!—1999
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1995
g95 7/8 kur. 5-7

Ni Yapi Baadhi ya Hayo Matatizo?

Wazazi-wakuu, wazazi, na wajukuu—vizazi vitatu vilivyotenganishwa kimiaka na miongo michache tu, hata hivyo kwa habari ya mwelekeo wa akilini na mtazamo yaonekana vimetenganishwa na mgawanyiko mkubwa mno.

WAZAZI-WAKUU wengi walipitia hali yenye kuogofya ya vita ya ulimwengu ya pili, pamoja na matokeo yayo yenye kuharibu. Watoto wao huenda walikuwa wachanga wakati wa harakati za kupinga vita na upanuzi wenye kuenea haraka wa kiuchumi wa miaka ya 1960. Wajukuu wao leo wanaishi katika ulimwengu wa utovu wa kanuni. Kukiwa na mabadiliko ya haraka leo katika violezo mashuhuri vya kuigwa, si rahisi kwa kizazi kimoja kukazia kizazi kifuatacho utambuliwaji wa thamani ya maono yacho. Kuna kitu kinachokosekana, kitu cha kuhimiza watu wa vizazi tofauti kushirikiana na kustahiana. Lakini hicho chaweza kuwa nini?

Mara nyingi, wazazi-wakuu wenye nia nzuri hujiingiliza katika mambo ya familia ya watoto wao waliooana, wakilalamika kwamba hao wazazi yaonekana wako wagumu sana au wamejilegeza sana kwa wajukuu wao. Kwa upande ule mwingine, methali ya Kihispania yasema hivi: “Adhabu kutoka kwa wazazi-wakuu haisaidii kutokeza wajukuu wema”—kwa kuwa wazazi-wakuu huelekea kuwa wenye huruma. Labda wanajiingiliza kwa sababu wangependa watoto wao waepuke makosa fulani ambayo, kwa sababu ya uzoefu wao wanaweza kuyatambua kwa wazi. Hata hivyo, huenda wasiweze kupima thamani tena na kufahamu maana ya mahusiano yanayobadilika pamoja na watoto wao waliooana katika njia ya usawaziko. Hao watoto, ambao kwa njia ya ndoa wamepata uhuru waliokuwa wametamani kwa muda mrefu, hawako tayari kuvumilia ujiingilizi. Sasa wanafanya kazi ili kutegemeza familia, hawanuii kukubali kuvunjwa kwa haki yao ya kufanya maamuzi yao wenyewe. Wajukuu, ambao huenda wakafikiri tayari wanajua yote, wanachukia sheria na maagizo na labda wanawaona wazazi-wakuu wao kuwa wasiofahamu mambo halisi ya maisha ya kisasa. Katika jamii ya kisasa, wazazi-wakuu yaonekana wamepoteza uvutio wao. Uzoefu wao mara nyingi hupuuzwa.

Wakati Mazungumzo Yanapokoma

Nyakati nyingine ukuta usiopenyeka wa ukosefu wa kuelewana hutenga wazazi-wakuu kutoka washiriki wengine wa familia hata wakati wanapoishi na watoto wao. Kwa kusikitisha, hili hutukia hasa katika wakati ambao, kwa sababu umri wa uzee unakuwa wenye kulemea sana, wazazi-wakuu wana uhitaji mkubwa sana wa kuonyeshwa shauku. Si lazima mtu awe peke yake ili ahisi upweke. Wakati mazungumzo yanapokoma, wakati mahali pa staha na shauku panachukuliwa na ushushwaji au kuchokozeka, matokeo huwa kujitenga kabisa na udhiko la kina kwa upande wa wazazi-wakuu. Mambo hayo yanaumiza katika hisia zao za ndani sana. Mwelimishaji Giacomo Dacquino aandika hivi: “Upendo katika familia, ambao mtu fulani hivi majuzi aliulinganisha na gari zee la muundo wa kale lililowekwa kando kwa kutofaa, bado ni dawa iliyo bora kupita zote za magonjwa na matatizo ya uzee. Wonyesho wa uso wenye kuelewa, tabasamu yenye fadhili, neno lenye kutia moyo, au mguso husaidia zaidi ya dawa nyingi.”—Libertà di invecchiare (Uhuru wa Kuzeeka).

Kielelezo Chako Chaweza Kufanyiza Tofauti

Mkazo unaotokana na mahusiano ya kifamilia yaliyodhoofika pia husababisha malalamiko yenye kuendelea ya kizazi kimoja dhidi ya kingine. Mshiriki mmoja wa familia huenda akahisi kwamba chochote mwingine afanyacho ni kosa. Lakini athari zilizo mbaya huhisiwa na wote. Watoto wanatazama jinsi wazazi wao wanavyowatendea wazazi-wakuu, na vilevile jinsi wazazi-wakuu wao wanavyoitikia. Ingawa wazee-wazee, kwa ujumla, huenda wakaumia kimya-kimya, wajukuu wanasikia, kuona, na kukumbuka. Hivyo namna yao wenyewe ya mwenendo wa wakati ujao inaathiriwa. Wakiwa watu wazima, yaelekea huenda wakawatendea wazazi wao sawa na vile wazazi hawa walivyowatendea wazazi-wakuu. Hakuna kupiga chenga ile kanuni ya Biblia: “Cho chote apandacho mtu, ndicho atakachovuna.”—Wagalatia 6:7.

Ikiwa wajukuu wanaona wazazi wakiwatendea wazazi-wakuu katika njia ya kuwashusha—wakiwafanyia dhihaka, kuwanyamazisha kijeuri, au hata kuwatumia kwa faida yao—hii ndiyo njia ambayo, kwa kufuata waliyoona, huenda wakatenda kuelekea wazazi wao wanapokuwa wazee. Haitoshi kuweka picha iliyowekewa fremu juu ya kabati—ni lazima wastahiwe na kupendwa wakiwa watu. Baada ya kupita kwa wakati, kutendewa hukohuko kwaweza kutolewa na wajukuu. Yasemekana kwamba kawaida ya kutendewa vibaya kwa wazazi-wakuu yaenea kwa kuendelea sana. Katika nchi fulani za Ulaya, laini za simu ambazo mtu aweza kupiga na kusema na mtu fulani aliye tayari kusikiliza matatizo na kutoa msaada zimewekwa kwa ajili ya uingilio kwa niaba ya watu wazee-wazee wanaotendewa vibaya, sawa na zile zinazofanya kazi kwa ajili ya ulindaji wa watoto.

Ubinafsi, kiburi, na ukosefu wa upendo hukuza na kuongeza ukosefu wa kuelewana. Kwa hiyo, idadi ya wale wajaribuo kujiondolea wazazi-wakuu kwa kuwaweka katika makao ya utunzaji yaendelea kukua. Wengine wako tayari kutumia viwango vikubwa vya fedha ili wajiondolee tatizo la kutunza wazee-wazee, wakiwakabidhi ama kwa vitovu maalum vilivyo na vifaa vyote vya tekinolojia ya karibuni zaidi au vijiji vya waliostaafu kama vile vilivyoko Florida au California, Marekani, ambapo kuna wingi wa maduka makuu na vitumbuizo lakini hata hivyo wanakosa ile tabasamu na mpapaso-papaso wa wapendwa wao na kumbatio la wajukuu. Hasa nyakati za likizo, wengi hutafuta mahali pa “kuegesha” nyanya na babu. Katika India hali nyakati fulani yaweza kuwa mbaya hata zaidi wakati ambapo wazazi-wakuu wanaachwa tu waendelee kuishi bila kusaidiwa.

Magumu ya kuwa na mahusiano ya karibu ya familia yanakuzwa na talaka. Ni familia 1 tu ya Uingereza kati ya 4 ambayo wazazi wote wawili wanaishi bado katika hiyo nyumba. Hata hivyo, talaka inaongezeka ulimwenguni pote. Katika Marekani, kuna zaidi ya talaka milioni moja kila mwaka. Kwa hiyo wazazi-wakuu bila kutazamia wanakutana ana kwa ana na matatizo ya ndoa ya watoto wao na mabadiliko makubwa yafuatayo katika mahusiano pamoja na wajukuu wao. Juu ya aibiko la kushughulika na aliyekuwa mwana-mkwe au binti-mkwe kunaongezewa tatizo la “kuja kwa ghafula kwa wajukuu ‘waliopatikana’” ikiwa, kama ilivyoripotiwa na gazeti la habari la Kiitalia Corriere Salute, “mwenzi mpya wa mwana au binti yao angekuwa amepata watoto kutokana na ndoa ya awali.”

“Uchangamfu kwa Maisha Zetu”

Walakini, uhusiano mchangamfu, wenye shauku pamoja na wazazi-wakuu wa mtu, iwe wanaishi pamoja na washiriki wengine wa familia au la, ni wa manufaa nyingi mno. “Kufanya jambo fulani kwa ajili ya watoto na wajukuu wetu,” asema Ryoko, nyanya fulani kutoka Fukui, Japani, “kwatosha kutoa uchangamfu kwa maisha zetu.” Kulingana na matokeo ya utafiti yaliyochapishwa na Corriere Salute, kikundi cha wataalamu wa Marekani charipotiwa kuwa kilisema: “Wakati wazazi-wakuu na wajukuu wanapokuwa na mambo mazuri ya kufurahia uhusiano wa kina na wenye shauku, manufaa ni nyingi mno si kwa watoto tu bali pia kwa familia nzima.”

Ni nini, basi, kiwezacho kufanywa ili kushinda tofauti za kibinafsi, tofauti kati ya vizazi, na vitabia visivyoepukika kuelekea ubinafsi ambao huwa na uvutano mkubwa wenye kudhuru kwa mahusiano ya kifamilia? Habari hii itazungumziwa katika makala ifuatayo.

[Blabu katika ukurasa wa 6]

“Jambo la kuogofya kuhusu kuzeeka ni kutosikilizwa.”—Albert Camus, mwanariwaya Mfaransa

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki