Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g95 10/8 kur. 19-20
  • Kwa Kupepesa Jicho

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kwa Kupepesa Jicho
  • Amkeni!—1995
  • Habari Zinazolingana
  • Je, Watoto Wako Salama Wakiwa na Mbwa Wako?
    Amkeni!—1997
  • Jinsi ya Kumzoeza Mbwa Wako
    Amkeni!—2004
  • Uwezo wa Kunusa wa Mbwa
    Je, Ni Kazi ya Ubuni?
  • Je, Ni Mnyama-Kipenzi au Ni Muuaji Hatari?
    Amkeni!—2002
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1995
g95 10/8 kur. 19-20

Kwa Kupepesa Jicho

UMEFANYA tena. Jana ulifanya hivyo mara 15,000 hivi. Yaelekea sana hukujua kamwe kwamba ulikuwa ukifanya hivyo, lakini uliendelea kufanya hivyo na kwa njia hiyo kulinda viwili vya vitu vyako vyenye thamani kuliko vyote. Katika kufanya hivyo, huenda pia uliashiria bila kujua jinsi ubongo wako ufanyavyo kazi. Ulifanyaje yote haya? Ulipepesa.

Ikiwa macho yako yanafanya kazi vizuri, hayo ndiyo mfumo wa hisi ulio mwepesi na mnyetivu zaidi ulio nao. Likitambuliwa kwa mapana kuwa muujiza wa ubuni, jicho la binadamu limelinganishwa na kamera ya sinema yenye kujiendesha yenyewe, ya kuona pande tofauti-tofauti, yenye kujipimia umbali, ikipiga picha kwa mfululizo, na kwa rangi kamili. Wakati haitumiwi, lenzi ya kamera iliyo rahisi kuharibika hufunikwa na kifuniko cha lenzi. Lakini jicho hufanya vema zaidi ya hilo.

Sehemu kubwa ya duara la jicho imelindwa ndani ya tundu la jicho. Lakini asilimia 10 inayobaki ya sehemu ya juu ya jicho iko nje ambapo kuna vumbi lenye kuvurura na takataka zenye kudhuru. Ili kukinga jicho dhidi ya tisho hili la shambulio la daima, mwili umebuniwa ukiwa na “kifuniko [tata] cha lenzi” tata kiwezacho kurudi nyuma—ukope. Ukiwa umefanyizwa kwa ngozi iliyo nyembamba kuliko zote mwilini, na kutiwa nguvu kwa nyuzi-nyuzi, ukope huteleza kwa wororo chini na juu kuvuka jicho. Kupepesa huchukua sehemu ya kumi ya sekunde moja na hufanyika mara zipatazo 15 kila dakika.

Lakini tendo hilo dogo, lisiloonekana kwa urahisi hutimiza mengi. Kwa kufumba na kisha kufumbua, ukope huvuta utando mwembamba wa umajimaji kuvuka sehemu ya nje ya jicho, ukilisuza ifaavyo. Huo pia hung’arisha sehemu ya nje ya jicho. Kwa hiyo ukope waweza kulinganishwa na kifuniko cha lenzi, kisafisha-lenzi, na king’arisha-lenzi vyote pamoja. Ubuni kwelikweli, sivyo?

Lakini wanasayansi wametatanishwa kwa muda mrefu na jambo lisilo la kawaida: Kwa kiwango ambacho machozi yenye umajimaji hutoweka, kupepesa mara moja au mbili kwa dakika kunapasa kutosha kufanya kazi ya kusuza na kung’arisha. Kwa nini, basi, kupepesa kwingine kote kwa ziada? Yaonekana jibu liko akilini.

Watafiti wamepata uhusiano baina ya kupepesa na kufikiri. Kwa mfano, wasiwasi hukufanya upepese zaidi. Ikiwa unajaribu kupeleka helikopta, au unahojiwa na wakili mkali, au una tatizo la wasiwasi, yaelekea unapepesa zaidi kuliko kawaida. Ikiwa wewe ni mtangazaji wa habari katika televisheni, huenda umeelezwa usipepese ili watazamaji wako wasifikiri umeshikwa na woga kwa sababu ya habari hizo.

Kwa upande ule mwingine, ikiwa wakaza macho, kama vile kufuatia mstari kupitia mizingo, kuendesha gari katika barabara za jiji, au kusoma riwaya, unapepesa mara chache zaidi. Kwa mfano, marubani, wanahitaji kukaza fikira kuliko marubani wasaidizi, kwa hiyo wanapepesa mara chache zaidi. Kupepesa huzuiwa hasa wakati mtu yuko katika hatari halisi, macho yanahitaji kutazama upesi kutoka mbele hadi kando-kando na kurudi.

Kuna uhusiano mwingine kati ya ubongo na kupepesa. Kulingana na The Medical Post la Kanada, utafiti wadokeza kwamba “kila kupepesa kwaweza kutokea katika wakati barabara ambao tunaacha kuona na kuanza kufikiri.” Kwa kielelezo, mtu anayekariri jambo fulani labda atapepesa baada tu ya kuchungua habari anayotaka kuhifadhi. Au katika kufanya uamuzi, majaribio yanadokeza kwamba “ubongo huamrisha kupepesa wakati una habari ya kutosha kufanya uamuzi ufaao,” laonelea Post, likiongeza hivi: “Majaribio yanaonyesha kwamba kupepesa hutumika kuwa namna ya kiakili ya kutenga maneno kwa vituo.”

Ilikuwa karibu miaka elfu tatu iliyopita kwamba mwanamume mwenye hekima alipuliziwa kuandika hivi: “Nimeumbwa kwa jinsi ya ajabu ya kutisha.” (Zaburi 139:14) Maendeleo ya sayansi ya kitiba katika siku yetu yameunga mkono maoni hayo. Ebu wazia: kung’arisha na kutia utelezi lenzi tata, kupima kiwango cha ubongo cha kukaza fikira au wasiwasi, na kutenga kwa vituo mwingizo wa habari yenye kuonwa na macho—yote hayo kwa kupepesa jicho!

[Picha katika ukurasa wa 19]

Duara la jicho asilimia 10 tu ikiwa nje

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki