Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g95 11/8 kur. 3-5
  • Usanii Ni Nini?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Usanii Ni Nini?
  • Amkeni!—1995
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Kufasili Usanii
  • Msanii Mwenye Uwezo Huo wa Kisanaa
  • Msanii Aliyepuuzwa Zaidi wa Wakati Wetu
    Amkeni!—1995
  • Maisha Yangu Nikiwa Mchoraji
    Amkeni!—2001
  • Kutumikia Msanii Aliye Mkubwa wa Wote
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1990
  • Je, Unatumia kwa Hekima Uwezo Wako wa Kuwazia?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova (Funzo)—2016
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1995
g95 11/8 kur. 3-5

Usanii Ni Nini?

NA MLETA-HABARI WA AMKENI! KATIKA HISPANIA

NI IPI mandhari yenye kupendeza kuliko zote uliyopata kuona? Je, ilikuwa machweo ya kitropiki, safu ya milima iliyofunikwa kwa barafu, maua mengi yaliyochanua jangwani, rangi zenye kupendeza za msitu wakati wa masika?

Wengi wetu huhifadhi akilini pindi ya pekee ambapo tulipendezwa mno na uzuri wa dunia. Tukiweza, sisi hupenda kutumia likizo zetu katika mazingira ya kiparadiso, nasi hujaribu kupiga picha mandhari zinazostahili kukumbukwa.

Wakati ujao unapotazama fahari hii isiyoharibiwa, kuna maswali ambayo huenda ukafikiria. Je, hungehisi kulikuwa na kitu kilichokosekana ikiwa kila mchoro katika nyumba ya sanaa ungekuwa umeandikwa “Mchoraji Hajulikani”? Ikiwa ulichochewa hisia mno na ubora na uzuri wa michoro hiyo katika maonyesho, je, hungetaka kujua ni nani aliyekuwa msanii? Je, tunapaswa kutosheka kutafakari maajabu ya dunia yenye uzuri na kisha tumpuuze Msanii aliyeyaumba?

Ni kweli, kuna wale wanaodai kwamba hakuna kitu kama sanaa katika asili—kwamba sanaa huhitaji ustadi wa kibinadamu wa ubuni na kuudhihirisha. Hata hivyo, fasili hiyo ya usanii, labda haielezi mengi. Hata hivyo usanii ni nini hasa?

Kufasili Usanii

Yaelekea ni vigumu kupata fasili ya usanii itakayotosheleza kila mtu. Lakini elezo zuri lapatikana katika Webster’s Ninth New Collegiate Dictionary, ambayo husema kwamba usanii ni “utumizi wenye utambuzi wa ustadi na uwezo wa kufikiri wenye ubuni hasa katika kutokeza vitu vyenye uvutio wa kisanaa.” Kwa msingi huu twaweza kusema kwamba msanii huhitaji ustadi na vilevile uwezo wa kufikiri wenye ubuni. Anapotumia vipawa hivi viwili vya kiasili, yeye anaweza kutokeza kitu ambacho wengine watakiona kuwa chenye kupendeza au kuvutia.

Je, udhihirisho wa ustadi na uwezo wa kufikiri wapatikana katika sanaa ya binadamu tu? Au unaonekana wazi pia katika ulimwengu wa asili unaotuzunguka?

Miti mikubwa mno ya misunobari ya California, miamba ya matumbawe iliyoenea sana ya Pasifiki, maporomoko makubwa mno ya maji ya misitu ya kitropiki, na makundi ya wanyama yenye fahari ya savana ya Afrika, katika njia tofauti, yana thamani kwa jamii ya kibinadamu kuliko ule mchoro wa “Mona Lisa.” Kwa sababu hiyo, UNESCO (Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi, na Utamaduni) limeteua Mbuga ya Kitaifa ya Redwood (Marekani), Maporomoko ya Maji ya Iguaçú, yaliyoko mpakani mwa Argentina na Brazili; Great Barrier Reef, Australia, na Mbuga ya Kitaifa ya Serengeti, Tanzania, kuwa sehemu ya “Urithi wa Ulimwengu” wa jamii ya kibinadamu.

Hazina hizi za kiasili zatajwa pamoja na majengo ya ukumbuko ya binadamu. Kwa nini? Lengo ni kuhifadhi chochote kilicho na “thamani ipitayo ya kawaida ya ulimwenguni pote.” UNESCO laonelea kwamba iwe uzuri ni ule wa kaburi Taj Mahal, India, au Grand Canyon, Marekani, huo wastahili kulindwa kwa ajili ya vizazi vijavyo.

Lakini huhitaji kusafiri hadi kwenye hifadhi ya kitaifa ili kuona ustadi huu wenye ubuni. Kielelezo kikuu kuliko vyote ni mwili wako mwenyewe. Wachonga-sanamu wa Ugiriki ya kale waliona umbo la binadamu kuwa mfano wa ubora wa kisanaa, na walijitahidi kuudhihirisha kwa njia kamilifu kwa kadiri walivyoweza. Tukiwa na ujuzi wa wakati huu wa jinsi mwili ufanyavyo kazi, twaweza kuthamini hata zaidi uwezo mkamilifu uliohitajika kwa uumbaji na ubuni wao.

Namna gani uwezo wa kufikiri wenye ubuni? Tazama vigezo bora sana kwenye wonyesho wa mabawa yaliyoinuliwa ya tausi, ua lenye kupendeza la waridi, au kikundi kama cha mchezo wa dansi wenye mwendo wa kasi wa ndege-mvumi mwenye kung’aa. Kwa hakika, ubora huo wa kisanaa ulikuwa sanaa, hata kabla ya kuchorwa au kupigwa picha. Mwandikaji wa National Geographic, akiwa amevutiwa na nyuzi zenye rangi ya zambarau iliyochakaa za ua liitwalo tacca lily, alimuuliza mwanasayansi mchanga ni nini lililokuwa kusudi lazo. Jibu lake sahili lilikuwa: “Hufunua uwezo wa kufikiri wa Mungu.”

Ustadi na uwezo wa kufikiri wenye ubuni haujajaa katika ulimwengu wa asili tu bali umekuwa chanzo cha daima cha kuchochea wasanii wa kibinadamu. Auguste Rodin, mchongaji Mfaransa ajulikanaye sana, alisema hivi: “Msanii ndiye msiri wa asili. Maua huwasiliana naye kupitia kujipinda kwa madaha kwa mashina yayo na uzuri uliotiwa rangi kwa upatano wa chipukizi zayo.”

Wasanii fulani walitambua waziwazi mapungukio yao walipojaribu kuiga uzuri wa asili. “Mchoro halisi wa sanaa ni wonyesho mdogo sana ukilinganishwa na ule wa kimungu,” akaungama Michelangelo, anayefikiriwa kuwa mmoja wa wasanii stadi zaidi wa wakati wote.

Huenda wanasayansi, na vilevile wasanii, wakashangazwa na uzuri wa ulimwengu wa asili. Profesa wa fizikia ya hisibati, Paul Davies, katika kitabu chake The Mind of God, aeleza kwamba “hata waatheisti washupavu mara kwa mara wamekuwa na kile ambacho kimeitwa hisi ya staha ya kina kwa asili, uvutio na staha kwa hekima na ukuu na uzuri wayo na hali yayo yenye kupendeza, ambayo yafanana na hofu ya kidini.” Hili lapasa kutufunza nini?

Msanii Mwenye Uwezo Huo wa Kisanaa

Mwanafunzi wa sanaa hujifunza kuhusu msanii ili afahamu na kuthamini usanii wake. Yeye hutambua kwamba kazi ya msanii huonyesha jinsi mtu huyo alivyo. Sanaa ya asili pia huonyesha utu wa mwanzilishi wa asili, Mungu Mweza Yote. “Sifa zake zisizoonekana zaonwa waziwazi . . . kwa vitu vilivyofanywa,” akaeleza mtume Paulo. (Warumi 1:20, New World Translation) Isitoshe, Mfanyi wa dunia si asiyejulikana hata kidogo. Kama Paulo alivyowaambia wanafalsafa Waathene wa wakati wake, “[Mungu] hawi mbali na kila mmoja wetu.”—Matendo 17:27.

Kazi ya sanaa katika uumbaji wa Mungu si isiyo na kusudi au ya kiaksidenti. Zaidi ya kuboresha maisha zetu, hiyo hufunua stadi, uwezo wa kufikiri, na ukuu wa Msanii mkuu kuliko wote, Mbuni wa Ulimwengu Wote Mzima, Yehova Mungu. Makala ifuatayo itazungumzia jinsi usanii huu uwezavyo kutusaidia kupata kumjua vizuri zaidi yule Msanii Mkuu Kuliko Wote.

[Hisani ya Picha katika ukurasa wa 3]

Musei Capitolini, Roma

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki