Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g95 12/8 uku. 30
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
  • Amkeni!—1995
  • Habari Zinazolingana
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
    Amkeni!—2005
  • Nifanye Nini Ikiwa Ninavutiwa na Watu wa Jinsia Yangu?
    Maswali Ambayo Vijana Huuliza—Majibu Yafanyayo Kazi, Buku la 2
  • Je, Kuna Sababu Zinazotetea Ushoga?
    Amkeni!—2012
  • Ninaweza Kuelezaje Maoni ya Biblia Kuhusu Ugoni-Jinsia-Moja?
    Maswali Ambayo Vijana Huuliza—Majibu Yafanyayo Kazi, Buku la 1
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1995
g95 12/8 uku. 30

Kutoka kwa Wasomaji Wetu

Watoto Waliopotea Kufikia wakati nilipomaliza kusoma ule mfululizo wa makala “Watoto Waliopotea—Msiba Utakwisha Lini?” (Februari 8, 1995), machozi yalikuwa yakitiririka usoni mwangu. Baadhi ya maono yaliyosimuliwa katika hizo makala yalifanana na langu. Namshukuru Yehova kwa kunipa nguvu za kuvumilia. Kupitia Neno lake nimepata tumaini la paradiso ambapo watu hawatapatwa kamwe na maovu kama hayo.

T. O., Brazili

Mfungwa wa Japani Nilitiwa moyo kusoma ile makala “Baba Yangu ‘Aliondolewa Gerezani na Kombora la Atomi.’” (Oktoba 8, 1994) Nilibatizwa hivi majuzi nikiwa Mkristo, na mara nyingi nimejiuliza kama ningedumisha uaminifu-maadili wangu chini ya kishawishi. Nilipokuwa nikisoma kuhusu imani ya Ndugu Katsuo Miura iliyo kama mwamba, hisia-moyo zenye nguvu zilinijaa moyoni. Ilinisaidia kufahamu kile ninachokosa katika imani yangu mwenyewe—kwamba nahitaji kumfanya Yehova Mungu kuwa chanzo cha tumaini langu.

K. T., Japani

Jeni Tumekuwa tukizungumza kuhusu msimbo jeni shuleni. Kwa hivyo nilichukua pindi hiyo kuweka lile gazeti lenye habari “Jeni ya Binadamu—Kinachokufanyiza ‘Wewe’” (Machi 22, 1995) kwenye kitabu changu cha kuandikia. Nilichanganua hiyo makala pamoja na mwalimu wetu wa sayansi. Aliniambia kwamba hata ingawa yeye ni mwanabiolojia na amejifunza DNA kwa miaka, alipendezwa na jinsi habari hiyo ilivyokuwa ya kina.

P. N., Italia

Makala hizo zilionyesha jinsi habari iliyo tata iwezavyo kuelezwa kwa mitajo yenye kueleweka. Zilinisaidia kuelewa vizuri zaidi habari ninayojifunza katika somo la biolojia. Hata hivyo, siwezi kunukuu kutoka hizo makala, kwani hamtoi habari za marejezo kama vile mtungaji na mtangazaji.

M. G., Ujerumani

Kwa sababu ya nafasi ndogo, kwa kawaida hatuchapishi orodha ya marejezo ya kilimwengu kama inavyofanywa mara nyingi katika majarida ya kiufundi na kisayansi. Kwa kuwa “Amkeni!” limeandikwa kwa ajili ya umma, si kwa ajili ya wataalamu tu, twahisi kwamba habari za marejezo ya vifaa hivi kwa kulinganisha zingependeza wasomaji wachache.—Mhariri

Ugoni-jinsia-moja Natumika nikiwa mtumishi wa huduma na painia, mweneza-evanjeli wa wakati wote. Zile makala za “Vijana Huuliza . . . ” kuhusu ugoni-jinsia-moja yaonekana ziliandikwa kwa ajili yangu! (Februari 8, Februari 22, na Machi 22, 1995) Katika miaka ya mapema na ya kati ya utineja wangu, nilijaribu ugoni-jinsia-moja. Niliacha, lakini tangu wakati huo nimeona vigumu kupigana na hisia hizi. Hata hivyo, kupitia kwa makala hizi, hatimaye naelewa hisia zangu, nimepata msaada ili kuendelea na hilo pigano!

Jina limebanwa, Denmark

Nimekuwa na hisia za ugoni-jinsia-moja tangu ubalehe. Nililelewa nikiwa Mkristo, hivyo hisia hizi zimekuwa zenye kunitatanisha kwelikweli. Kwa sababu niliona haya na kutatanika sana, singeweza kamwe kueleza hisia za ndani kwa yeyote, hata wazazi wangu mwenyewe. Sasa nimeoa mwanamke mrembo, lakini mara kwa mara mimi nina tamaa zisizofaa. Hatimaye, nilimweleza mke wangu siri yangu, naye alinitia moyo kuzungumza na wazee wa kutaniko. Walikuwa wenye kuelewa na wenye kutegemeza sana. Ikiwa ningeweza kusema lolote kwa yeyote anayeng’ang’ana na hisia hizi, lingekuwa hili: Usiliweke tatizo lako siri. Mwambie mwenzi wako, wazazi wako, mzee fulani, au rafiki unayemwamini—lakini usifiche.

Jina limebanwa, Marekani

Tangu utotoni, nilitendwa vibaya kingono. Hakuna upendo wala shauku niliyopata kuonyeshwa. Nilizoea ugoni-jinsia-moja, laiti vijana wangejua aibu, maumivu, huzuni, na kukata tamaa ambazo mtazamo wa ugoni-jinsia-moja huleta, wangezitoroka. Wengi huepuka kuzungumza kuhusu kichwa hiki, lakini mlikishughulikia kwa njia nzuri. Nawashukuru kwa moyo wangu wote kwa kuchapisha habari kama hizo.

Jina limebanwa, Brazili

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki