Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g95 12/8 kur. 28-29
  • Kuutazama Ulimwengu

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kuutazama Ulimwengu
  • Amkeni!—1995
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Kujua Kusoma na Kuandika na Afya
  • Kongamano Lenye Utupu
  • Kujifunza Hisia-Mwenzi
  • Wanawake au Wanaume —Ni Nani Wafanyao Kazi kwa Muda Mrefu Zaidi?
  • Idadi ya Watu wa China Yafikia Bilioni 1.2
  • Konokono Wavamia
  • Tukio Dogo Linalohusiana na Vita ya Ulimwengu 2
  • Kuna Yeyote Angependa Kucheza Tenisi?
  • Mimea Iliyo na “Kumbukumbu”
  • Makasisi wa Ziada
  • Watoto—Ni Faida au Ni Hasara?
    Amkeni!—1993
  • Kuutazama Ulimwengu
    Amkeni!—1997
  • Wanawake Waishi Zaidi Lakini si Lazima Maisha Bora
    Amkeni!—1997
  • Je! Nchi Yako Ni Shabaha Kubwa ya Kuuziwa?
    Amkeni!—1990
Amkeni!—1995
g95 12/8 kur. 28-29

Kuutazama Ulimwengu

Kujua Kusoma na Kuandika na Afya

Kiwango cha juu zaidi cha kujua kusoma na kuandika huenda kikachangia matarajio ya kuishi muda mrefu, kulingana na tarakimu zilizonukuliwa na UNESCO (Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi, na Utamaduni). “Watu ambao wamejifunza kusoma na kuandika,” laonelea gazeti UNESCO Sources, “hukaza fikira zaidi kwa elimu-siha na utunzi wa afya; huelekea kutokuwa wenye imani kwamba yote yalitangulia kupangwa kimbele na, wanapokuwa wagonjwa, huelekea sana kwenda kwa daktari.” Ingawa hivyo, kujua kusoma na kuandika, ni moja tu ya mambo yanayoathiri matarajio ya kuishi. “Kuweza kufikia matibabu ya kitiba, hali za kifedha za familia na mazingira ya kijamii” pia huwa na sehemu muhimu.

Kongamano Lenye Utupu

Wajumbe wapatao 20,000 kutoka ulimwenguni pote walikutana katika Copenhagen, Denmark, mnamo Machi 6-12, 1995, ili kuhudhuria mkutano uliodhaminiwa na Umoja wa Mataifa uliokuwa na kichwa: “Kongamano la Ulimwenguni Kwa Ajili Ya Maendeleo ya Kijamii.” Kusudi la kukutana? Ili kuzungumza juu ya njia za kumaliza umaskini, ukosefu wa kazi ya kuajiriwa, na ubaguzi katika nchi zinazositawi. Hata hivyo, haikuchukua muda mrefu kutambulisha kizuizi kikubwa mno—ukosefu wa fedha. Inaonekana kwamba nchi nyingi zinazokumbwa na umaskini zina deni kubwa mno kwa mataifa tajiri hivi kwamba haziwezi hata kulipa riba zao. Taifa lililoandaa tukio hilo, Denmark, lilidokeza kwamba mataifa tajiri yafuate kielelezo chalo na kuondoa madeni ya mataifa maskini zaidi. Ingawa hivyo, kuna tatizo moja. Madeni mengi ya mataifa yaliyo maskini zaidi yametokana na kununua silaha. Kwa hivyo, kama mshauri mmoja wa UM alivyoeleza, deni likiondolewa, mataifa hayo yatatumia fursa hiyo kununua bunduki zaidi.

Kujifunza Hisia-Mwenzi

Watafiti wanaochunguza hisia-mwenzi katika watoto wamedokeza kwamba uwezo wa kuelewa hisia za wengine hupatikana kwa kujifunza. “Imeonyeshwa kwamba watoto ambao wametendwa vibaya hawaitikii kwa hisia-mwenzi kuelekea mkazo wa watoto wengine,” asema Dakt. Mark A. Barnett, profesa katika Chuo Kikuu cha Jimbo la Kansas katika Manhattan, kama ilivyonukuliwa katika The New York Times. “Huenda wakamtazama mtoto aliye na mkazo na wasifanye lolote, au humwendea na kumpazia sauti na kumsukuma huyo mtoto.” Kwa upande ule mwingine, yeye aongeza kwamba “mtoto ambaye mahitaji yake mwenyewe ya kihisia-moyo yanashughulikiwa huitikia zaidi kwa hisia-moyo za wengine.” Hata hivyo, zaidi ya kuandaa usalama wa kihisia-moyo, wazazi wanahitaji kuonyesha watoto wao jinsi ya kuwa wenye hisia-mwenzi. Kama Dakt. Barnett asemavyo, wazazi wenye hisia-mwenzi kwa kawaida hulea watoto wenye hisia-mwenzi.

Wanawake au Wanaume —Ni Nani Wafanyao Kazi kwa Muda Mrefu Zaidi?

Isipokuwa katika Amerika ya Kaskazini na Australia, wanawake kila mahali hufanya kazi kwa muda wa saa nyingi zaidi kuliko wanaume, laripoti Populi, gazeti la UNFPA (Wakf wa Umoja wa Mataifa wa Idadi ya Watu). Pengo kubwa kuliko yote liko katika Afrika na eneo la Asia-Pasifiki, ambapo wanawake wafanyao kazi, kwa wastani, hufanya kazi kwa muda wa saa zipatazo 12 zaidi kwa juma kuliko wanaume. “Katika nchi nyingi zinazositawi,” laonelea hilo gazeti, “wanawake sasa wanafanya kazi kwa muda wa saa 60-90 kwa juma ili kujaribu tu kudumisha viwango vyao vya kuishi vilivyo chini vya mwongo uliopita.” Wakati huohuo, katika ulimwengu uliositawi kiviwanda, ushiriki wa wanaume katika kazi za nyumbani unaongezeka. “Lakini,” laeleza Populi, ongezeko hili “halitokani na ugawanyaji sawa wa kupika kwa kawaida, kusafisha, na kuosha nguo. Badala ya hivyo, wanaume wanachukua muda mrefu zaidi kufanya kazi kama vile kununua vitu.”

Idadi ya Watu wa China Yafikia Bilioni 1.2

Mapema mwaka huu idadi ya watu wa China ilifikia bilioni 1.2, likaripoti China Today. Hiyo idadi ya watu ingefikia kiasi hiki miaka tisa mapema kama hakungekuwako programu ya kitaifa ya upangaji uzazi iliyoanzishwa katika miaka ya 1970. Hata hivyo, katika kiwango cha sasa cha ukuzi, idadi ya watu wa China itafikia bilioni 1.3 mapema katika karne ijayo. Ingawa iko miongoni mwa nchi zilizo kubwa zaidi kijiografia, utokezaji wa jumla wa nafaka, nyama, na mayai wa China ni wa chini zaidi kuliko utokezaji wa nchi nyinginezo zilizositawi zaidi. Zaidi ya hilo, jumla ya ardhi iliyolimwa yawa ndogo kwa sababu ya uchafuzi na ukaaji wa watu wengi barani, likasema China Today.

Konokono Wavamia

Kabla ya konokono wa kidhahabu walio hai wa Amerika Kusini kuingizwa Vietnam kuwa chakula miaka sita iliyopita, wanasanyansi walionya kwamba konokono hao wangetokeza taabu kubwa kama wangepata kutoroka. Yaonekana wakati umethibitisha kwamba wanasayansi walisema kweli. Baadhi ya konokono walitoroka na haraka wakaonyesha hamu ya kula mpunga. Kisha serikali ikapiga marufuku konokono, lakini vituo vingi vidogo viliendelea kuwakuza na kuwauza kuwa chakula. Shirika la habari la Associated Press laripoti kwamba kulingana na shirika rasmi la Vietnam News, wanane tu wa viumbe hawa wadogo mno wanaweza kunyafua meta mraba ya shamba la mpunga kwa siku! Hao konokono wameripotiwa kuharibu hektari 31,000 za mpunga tayari na wameenea katika eneo la ukuzaji mpunga lililo na mazao kuliko yote katika hiyo nchi. Konokono mmoja wa kike anaweza kutaga mayai milioni 40 katika mwaka mmoja.

Tukio Dogo Linalohusiana na Vita ya Ulimwengu 2

Zaidi ya miaka 50 iliyopita, wakati Vita ya Ulimwengu 2 ilipokuwa imepamba moto, mkulima mmoja katika Colorado ya mashambani, Marekani, huenda alijifikiria kuwa salama kwa kadiri fulani kutokana na shambulizi la adui. Lazima mkulima kama huyo alishangaa kama nini wakati trekta yake kwa ghafula ilitumbukia katika shimo lililosababishwa na mlipuko wa bomu! Ilidhihirika kwamba hilo bomu lilikuwa limetegwa upande ule mwingine wa Bahari ya Pasifiki—kwa njia ya puto. Tukio hilo lisilo la kawaida kwa vita ya duniani pote, Wajapani waliamua kulipiza mashambulizi ya Marekani ya hewani katika 1942 kwa kurusha puto za hidrojeni zaidi ya 9,000 zilizobeba bomu zenye kuchoma na za kushambulia wanajeshi. Wazo kuu, kulingana na Scripps Howard News Service, lilikuwa kuanzisha mioto ya porini na wasiwasi katika Marekani, umbali upatao kilometa 10,000 kutoka Japani. Huo uharibifu ulikuwa mdogo kwa kulinganishwa, ingawa watu kadhaa waliuawa. Kulikuwa na visa vilivyoripotiwa 285 vilivyohusiana na puto, na kwa amri ya serikali, vyombo vya habari havikutangaza habari hii ili kuepuka wasiwasi.

Kuna Yeyote Angependa Kucheza Tenisi?

Uhitaji wa dawa za kulevya zisizo halali katika magereza ya Australia umeleta namna za kiufundi za ulanguzi wa dawa za kulevya. “Watu wanajaza mipira ya tenisi kwa dawa za kulevya zisizo halali na kutumia ubao wa kuchezea tufe ili kuipiga hadi katika jela za Australia,” laripoti shirika la habari la Reuters. Msemaji wa gereza Keith Blyth asema hivi: “Hufunga dawa kisha kuifunika (katika ukanda wa plastiki).” Kisha wanaiweka katika mpira wa tenisi na kuutupa au kuupiga kihalisi kuvuka ua wa gereza. Mlanguzi mwingine mwenye bidii alitumia upinde kurusha madawa ya kulevya yaliyo ndani ya mpira wa tenisi kuvuka ukuta wa gereza. Katika jaribio la kukomesha upitishaji huo, serikali ya Australia Kusini imefikiria, miongoni mwa mambo mengine, kutumia “mbwa wa kunusa madawa ya kulevya” kushika doria nje ya jela za serikali kutafuta “watu wenye mipira ya tenisi yenye kushukiwa,” akaeleza Blyth. Hata hivyo, hiyo ripoti ilisema kwamba “ile njia ya kidesturi zaidi ya kuficha dawa za kulevya katika keki” na kuzipeleka gerezani bado inapendwa sana.

Mimea Iliyo na “Kumbukumbu”

Inaposhambuliwa, mimea mingi hutokeza kemikali za kufukuza washambuliaji wayo. Gazeti New Scientist laripoti kwamba mingine pia hufanyiza “kumbukumbu” la hilo shambulizi, ikiiruhusu kuanza kutokeza sumu za kufukuza haraka zaidi ikishambuliwa tena. Kiwavi anayetafuna jani la tumbaku huchochea ufanyizaji wa asidi jasmoni, ambayo husafiri hadi mizizini. Jambo hili huanzisha utokezaji wa nikotini, ambayo hurudi kwenye majani ili kuyafanya yasiyotamanika kwa mlaji. Mimea yenye mizizi ambayo iliwekewa hiyo asidi iliitikia haraka zaidi kwa shambulizi. “Hili ladokeza kwamba mimea kwa kweli ina kumbukumbu,” asema Ian Baldwin wa Chuo Kikuu cha Jimbo la New York huko Buffalo.

Makasisi wa Ziada

Kupungua kwa washiriki katika makanisa ya Kiprotestanti ya Kanada kumeongoza kwenye “ziada isiyo na kifani ya makasisi Waprotestanti,” laripoti The Globe and Mail. Kwa miaka kumi iliyopita, Kanisa la Kianglikana katika Montreal, Quebec, limeona idadi ya washiriki ikianguka kutoka 67,000 hadi 27,000, huku idadi ya makasisi ikibaki palepale. Ziada ya makasisi imetokeza uhitaji wa kupata kazi za nusu-wakati au kuomba kupata bima ya ukosefu wa kazi ya kuajiriwa ili kuendelea kuishi. Katika Toronto, Ontario, Kanisa la Kipresbiteri linakabili tatizo sawa na hilo. Jean Armstrong, katibu mshirika wa huduma na kazi ya kanisa, asema hivi: “Hatuna uhakika ni kwa muda gani zaidi makutaniko yanaweza kustahimili wahudumu wa wakati wote.”

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki