Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g90 3/8 kur. 10-11
  • Je! Nchi Yako Ni Shabaha Kubwa ya Kuuziwa?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Je! Nchi Yako Ni Shabaha Kubwa ya Kuuziwa?
  • Amkeni!—1990
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Viwango Maradufu Katika Kueneza Magonjwa na Kifo
  • Baadhi Yao Hujitetea kwa Kujipigania
  • Maadili ya Tumbaku?
    Amkeni!—1992
  • Mamilioni ya Uhai Yakitokomea Moshini
    Amkeni!—1995
  • Tumbako na Uchunguzi wa Kama Yafaa Kutumiwa
    Amkeni!—1990
  • Makampuni ya Tumbaku Yamo Motoni
    Amkeni!—1996
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1990
g90 3/8 kur. 10-11

Je! Nchi Yako Ni Shabaha Kubwa ya Kuuziwa?

KWA sababu United States hununua tumbako ya bei rahisi zaidi katika Brazili na Zimbabwe, ina ziada ya tumbako. Kwa hiyo watengenezaji wakuu wa tumbako wangeweza kuiuza wapi? Kwenye nchi zilizo katika Afrika na Esia. Hivyo, gazeti Asiaweek laripoti hivi: “Nchi za Esia sasa zatumia karibu asilimia 50 ya tumbako ambayo Amerika huuza ng’ambo ya kwao, kwa njia hiyo zikichukua nafasi ya Uingereza na Ujeremani Magharibi katika kuwa masoko yenye kuongoza.”

Na wauzaji hao wa tumbako hupata malipo makubwa kama nini! Hupata soko lenye uwezekano wa kuwako watu karibu bilioni mbili katika muda wa miaka 20 ijayo. Idadi ya watu wa China na India tu kwa sasa ni kubwa ajabu—jumla iliyounganika ya watu karibu bilioni 1.8! Na kama vile World Health ilivyotaarifu: “Ingawa masoko ya tumbako yanapungua kule magharibi kwa kadiri ya asilimia moja kwa mwaka, katika nchi zinazositawi kuvuta sigareti kunaongezeka kwa wastani wa asilimia mbili kwa mwaka.” Na kumbuka kwamba lile soko lenye kupungua lina idadi ya watu wachache kuliko soko lililo wazi likingojea kutumiwa katika Mashariki. Biashara ya tumbako katika United States hutarajia kwamba mauzo katika Esia yataongezeka kwa asilimia 18 ufikapo mwaka 2000. Lakini kuna angalau kizuizi kimoja. Malipo ya forodhani.

Viwango Maradufu Katika Kueneza Magonjwa na Kifo

Kampuni za tumbako Amerika zaweza kufanyaje nchi zile nyingine zikubali sigareti zao za ziada? Zina mshirika ambaye ingawa kwa upande mmoja anaonya halaiki ya nchi yao wenyewe dhidi ya hatari za kuvuta sigareti, kwa upande ule mwingine yeye huendeleza moyo wa kuuza tumbako hatari katika nchi nyinginezo. Ni nani huyo? Ni serikali ya United States!

Asiaweek yaeleza hivi: “Ile jitihada kubwa ya kusafirisha tumbako nchi za nje imeungwa sana mkono na serikali ya United States. . . . Ofisi ya Mwakilishi wa Biashara Katika United States . . . imejitokeza kweli kweli kukandamiza vizuizi vya kibiashara na kujitahidi kupewa nafasi katika vyombo vya habari vya Esia ili itumiwe na kampuni za Kiamerika—hata ingawa matangazo ya sigareti yamepigwa marufuku kwa muda mrefu yasitangazwe katika mawimbi ya hewa katika United States.” Gazeti World Health laripoti hivi: “Kampuni za tumbako [za United States] zina uvutano mwingi sana wa kisiasa. Amri za lazima zimetokezwa ili kunyima au kutokeza tisho la kunyima Hong Kong, Taiwan, Japan na Korea idhini ya kufanyia biashara isipokuwa kama zitafungua masoko yao ili yatumiwe kwa mauzo na utangazaji wa bidhaa za tumbako ya Amerika.”

Jambo baya hata zaidi ni kwamba, kampuni za tumbako haziuzi bidhaa zazo katika Esia tu bali pia huinua sana mauzo yazo kwa kutumia utangazaji wa kubana sana watu. Nchi fulani-fulani, kama Taiwan na Korea Kusini, kwa kutiwa chini ya mbano, hata ziliondoa marufuku yazo kuhusu utangazaji wa tumbako! Sasa China iko katika nafasi zile za kwanza-kwanza katika orodha ya wenye kupelekewa kwa wingi zaidi sigareti za watengenezaji wa United States! Si ajabu kwamba mtekelezaji mmoja wa kampuni ya tumbako anukuliwa kuwa akisema: “Je! mwajua sisi twataka nini? Twaitaka Esia.” Lakini watu fulani wana maoni gani juu ya mbinu hizi za Kiamerika za kubana sana watu?

Kulingana na mwandikaji mmoja wa safu za New York Times, mwanabiashara mmoja Mkorea aliteta vikali “dhidi ya ukosefu wa maadili wa Kiamerika kwa sababu ya kulazimisha watu wa Korea wakubali sigareti za Kiamerika.” Naye hapo ana wazo halali. Ingawa Amerika hupiga vita vikali dhidi ya kuingia nchini kwa kokeni na heroini ambazo ni bidhaa za msingi kwa uchumi wa wengine, hiyo yataka kupakua mmea wayo yenyewe wenye sumu katika mataifa mengine. Kwa kuwa Amerika hudai kuwa ina viwango vya juu vya maadili, je! ni jambo lenye upatani idanganye mataifa mengine kwa kuyauzia ziada yayo ya bidhaa hatari za tumbako, na hali mengi ya mataifa hayo yana magumu makubwa ya kiuchumi?

Baadhi Yao Hujitetea kwa Kujipigania

Mataifa fulani ya Kiafrika, kama vile Gambia, Msumbiji, na Senegal, yamepiga marufuku utangazaji wa sigareti. Mwaka juzi waziri wa afya Naijeria alitaarifu kwamba serikali ya Naijeria ‘ingepiga marufuku utangazaji wote katika karatasi-habari, redio, na televisheni na mbao za matangazo. Tutapiga marufuku uvutaji sigareti katika mahali pote na vyombo vyote vya usafiri wa halaiki ya watu.” Amkeni! ilipashwa habari (Januari 1989) na ofisa wa habari katika Naijeria kwamba suala hili lingali likijadiliwa.

China ni taifa lenye wavutaji milioni 240. Kufikia mwaka 2025, wenye mamlaka wa tiba watarajia kupoteza watu milioni mbili kila mwaka kutokana na magonjwa yenye kuhusiana na uvutaji sigareti. China ina tatizo kubwa sana, kama vile yakiriwa na gazeti China Reconstructs: “Ijapokuwa serikali ya China ilipiga marufuku utangazaji wa sigareti, na kujapokuwako ripoti zenye kutokea mara nyingi katika karatasi-habari na magazeti zikionya juu ya athari zenye madhara kutokana na kuvuta sigareti, na bei ya sigareti ijapoongezeka daima, hesabu ya wavutaji katika China yaendelea kupanda.” Na tokeo moja ni nini? Ni kwamba “sasa kansa, magonjwa ya mishipa ya moyo na mapafu ndiyo yenye kuua zaidi katika China.”

Katika sehemu fulani za China, yaonwa kuwa ishara ya ukaribishaji mzuri kutolea wageni sigareti wakati wa kuwakaribisha. Lakini lo, ni bei iliyoje ambayo Wachina wanalipa! China Reconstructs laripoti hivi: “Wastadi wa tiba wameonya kwamba kutukia kwa kansa ya mapafu kunaongezeka kwa kadiri kubwa sana.” Kama vile mstadi mmoja Mchina alivyotaarifu: “Tayari sisi tunalipa bei ya juu mno.”

Hata hivyo, kuna hatari nyingine katika nguvu walizo nazo watangazaji wa tumbako—ule uvutano wao wenye ujanja usioonekana wazi katika vyombo vya habari.

[Picha katika ukurasa wa 10]

Tangazo la kukataza kuvuta sigareti katika Hong Kong

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki