Tumbako na Uchunguzi wa Kama Yafaa Kutumiwa
Sasa Uchunguzi na Ukome! Uhuru wa kunena—kutia na uhuru wa kutangaza—ni haki ambayo ni lazima tuihifadhi. Marufuku juu ya kutangaza sigareti haiungwi mkono na Waamerika walio wengi.”—Tangazo la karatasi-habari, Januari 1989, msingi walo ukiwa ni “maoni ya watu wazima 1500 walioombwa maoni katika simu.” Lakini je! watu 1,500 ndio huwakilisha “Waamerika walio wengi”?
WATANGAZAJI wa tumbako wabisha kwamba matangazo yao siyo huanzisha watu kuvuta sigareti. Hayo huamua tu kadiri ya uenezaji wa biashara miongoni mwa zile aina tofauti-tofauti. Hata hivyo, ongezeko la sasa miongoni mwa wavutaji wanawake hufanya dai hilo liwe la kubishanika. Lakini kuna uvutano mwingine wenye madhara ambao hutokana na nguvu nyingi za kunasa watu ambazo hutokezwa na watangazaji wa tumbako.
Katika miaka ya majuzi kampuni za tumbako United States zimejinunulia hali fulani ya kustahika (kuheshimika) kwa kununua kampuni za chakula na kuliondoa neno tumbako katika majina ya mashirika yao. Hivyo, Kampuni ya Tumbako Amerika ikawa Aina za Kiamerika; Kampuni ya Tumbako ya R. J. Reynolds hivi majuzi ikawa RJR/Nabisco; Shirika la Tumbako la Brown na Williamson likawa Shirika la Viwandani la Brown na Williamson. Lakini ni nini moja la matokeo ya mabadiliko haya? Hutokea mbano zaidi wa kufanya utangazaji. Jinsi gani hivyo?
Hata magazeti ambayo hayawi kamwe na matangazo ya tumbako hulazimika kuwa waangalifu yasichapishe makala zenye kuchambua uvutaji sigareti na bidhaa zilizofanyizwa kwa tumbako. Ni kweli kwamba huenda kusitokee hasara ya mapato ambayo hutokana na kutangaza tumbako. Lakini namna gani mashirika yale mengine ambayo sasa ni sehemu ya watengenezaji wakuu wa tumbako na ambayo hutangaza chakula au bidhaa nyinginezo? Na namna gani kuhusu zile makala au taarifa ambazo huenda zikaonyesha ubaya wa kuvuta sigareti? Huu ndio msingi ambao hufanya kila mhusika ajiamulie ni njia gani atakayotumia kutangaza sigareti bila kuonyesha wazi sana ubaya wazo.
Kielelezo kimoja chenye kupendeza ni lile toleo la Juni 6, 1983 la Newsweek. Matoleo yaliyotangulia na kufuata hilo la Juni 6 yalikuwa na kuanzia kurasa saba hadi kumi za matangazo ya sigareti. Lakini Newsweek ya Juni 6 ilikuwa na kurasa 4.3 kuhusu mfululizo wa makala zenye kupinga matumizi ya sigareti, zikiwa na kichwa “Uvutaji Sigareti Wapingwa Wazi.” Gazeti hilo lilikuwa na kurasa ngapi za matangazo ya sigareti katika toleo hilo? Hakuna. Mtungaji White ataarifu hivi: “Kampuni za sigareti zilipopata habari kuna mipango ya kuandika hadithi hiyo, ziliagiza kwamba matangazo yao yaondolewe. Huenda ikawa gazeti hilo lilipoteza dola milioni 1 za matangazo kwa sababu ya kuchapisha hadithi hiyo.”
Pesa ambazo hupatikana kutokana na matangazo ndizo hasa husaidia kuendeleza uchapishaji usiokoma wa magazeti na karatasi-habari hizo. Ushuhuda waonyesha kwamba wahariri hufikiri kwa uangalifu sana kuhusu habari watakazochapisha kwa kuchambua biashara ya tumbako, ikiwa kweli watachapisha hata moja. Mwandikaji mmoja wa afya alitaarifu hivi: “Kwa kielelezo, nikipanga uvutaji sigareti kati ya visababishi vya ugonjwa wa moyo mhariri wangu ataweka habari hiyo mwishoni mwa orodha au ataiondoa kabisa isiwepo.” Ni kama kusema, ‘Ulichokinunua kitumie utakavyo.’ Hali ya sasa imekuwa ya kwamba mhusika ndiye apaswa kujiamulia mwenyewe ni matangazo gani atakayochapisha.
Kwa kupendeza, The Wall Street Journal liliripoti kwamba kwa kipindi cha zaidi ya miaka sita ambapo magazeti mawili yenye kuelekezwa kwa weusi yalikuwa yakionyesha matangazo ya tumbako, hakuna lolote la hayo lililochapisha makala yoyote yenye kutaja moja kwa moja habari ya uvutaji sigareti na afya. Je! ilikuwa hivyo kwa sadfa tu? Ni wazi kwamba ni vigumu magazeti ambayo hutangaza bidhaa za tumbako yauume mkono ambao huyalisha. Kwa hiyo magazeti hayo hujiepusha kufichua wazi hatari za kuvuta sigareti.
Pitio hili la habari ya tumbako, kuvuta sigareti, na utangazaji latusaidia tuone kwamba kuna mengi ambayo huwa yapasa kufikiriwa sana. Kwa upande wa wakuzaji tumbako, huwa yawapasa wafikiri sana juu ya kupoteza riziki yao. Kwa upande wa watengenezaji wakuu na wauzaji wa tumbako, huwa yawapasa wafikiri sana juu ya kupoteza mapato yao manono. Kwa serikali, huwa yazipasa zifikiri sana juu ya kupoteza mapato ambayo hutokana na kodi. Na kwa yale mamilioni ya wavutaji sigareti, huwa yawapasa kufikiri sana juu ya kupoteza afya na maisha zao.
Kama wewe ni mvutaji wa sigareti au unafikiria kuanza kuvuta, chaguo ni lako. Kama vile mashirika tajiri ya tumbako katika United States yangependa kukukumbusha, kulingana na katiba wewe una haki ya kuvuta sigareti. Lakini kumbuka kwamba, kulingana na katiba wewe una haki pia ya kujasiria kuuawa na kansa ya mapafu au ya kooni, magonjwa ya moyo, kusakamwa na hewa mapafuni, ugonjwa wa Buerger (ona sanduku katika ukurasa 9), na maradhi mengine mengi. Kwa upande mwingine, ikiwa wewe wataka kuacha kuvuta sigareti, waweza kuacha jinsi gani? Ni nini chahitajiwa? Ni kichocheo!
[Picha katika ukurasa wa 12]
Koop mpasuaji mkuu wa United States amedumu katika kuonya dhidi ya hatari za utumizi wa tumbako
[Hisani]
Foto ya Utumishi wa Afya kwa Halaiki