Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g95 12/22 kur. 28-29
  • Kuutazama Ulimwengu

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kuutazama Ulimwengu
  • Amkeni!—1995
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Ulimwengu Wakabili “Msiba wa Kiafya”
  • Kupunguza Vifo vya Vitandani mwa Vitoto
  • Kukabiliana na Maumivu ya Mgongo
  • Michezo ya Vidio Yenye Jeuri
  • Viini Vyenye Kusumbua
  • Je, Ni Matokeo ya Mazingira Yenye Sumu?
  • Vijana Wana Maoni Hasi Kuhusu Wakati Ujao
  • Wenye Viini vya UKIMWI Hawaelezwi
  • Jambo Jipya Kwenye Soko la Ngamia
  • Viwango Vyenye Kuzorota vya China
  • Aina Mpya
  • Je, Nicheze Michezo ya Kompyuta au ya Vidio?
    Amkeni!—1996
  • Kuutazama Ulimwengu
    Amkeni!—1996
  • Je, Kuna Hatari kwa Wachezaji?
    Amkeni!—2002
  • Kuutazama Ulimwengu
    Amkeni!—1997
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1995
g95 12/22 kur. 28-29

Kuutazama Ulimwengu

Ulimwengu Wakabili “Msiba wa Kiafya”

“Muuaji mkubwa kuliko wote ulimwenguni na kisababishi kikuu kuliko vyote cha afya mbaya na kuteseka tufeni pote ni . . . umaskini wa kupindukia.” Ndivyo inavyotaarifu The World Health Report 1995, iliyochapishwa na WHO (Shirika la Afya Ulimwenguni). Nusu ya watu bilioni 5.6 ulimwenguni hawawezi kupata dawa zinazohitajika; karibu thuluthi ya watoto ulimwenguni hawapati lishe bora; na sehemu moja kwa tano ya idadi ya watu ulimwenguni huishi katika umaskini wa kupindukia, kulingana na hiyo ripoti. The Independent, gazeti la habari la London, Uingereza, lamnukuu mkurugenzi-msimamizi wa WHO akionya juu ya “msiba wa kiafya ambao katika huo mengi ya matimizo makubwa . . . katika miongo ya hivi majuzi yatashindwa vibaya mno.”

Kupunguza Vifo vya Vitandani mwa Vitoto

Katika jimbo la Ujerumani la North Rhine-Westphalia, programu fulani hupatia wazazi wote wa watoto waliozaliwa karibuni kijitabu kunachowafahamisha juu ya mambo ambayo huenda yakaongeza hatari ya kifo cha vitandani mwa vitoto. Baada ya kuanzishwa kwa hiyo programu, vifo vya vitandani mwa vitoto katika hilo jimbo vilishuka kwa asilimia 40, kulingana na gazeti la habari Süddeutsche Zeitung. Kufuatia programu kama hizo, Australia, Uingereza, Uholanzi, na Norway inasemekana zinapata mapunguo ya kufikia asilimia 60 katika vifo vya aina hiyo. Programu hii mpya ya kutambua kifo cha vitandani mwa vitoto huonya wazazi dhidi ya kulaza watoto kifudifudi, kutumia vifunikio vyenye manyoya mengi, au godoro laini, kuvuta sigareti wakati wa ujauzito, na kumfanya mtoto apumue moshi wa tumbaku.

Kukabiliana na Maumivu ya Mgongo

Yakitukia katika asilimia 90 ya watu ulimwenguni pote wakati fulani maishani mwao, maumivu ya sehemu ya chini ya mgongo ndiyo “hali ya mara kwa mara zaidi inayoathiri binadamu,” kulingana na The Medical Post la Kanada. Hata hivyo, katika visa vingi, matibabu ya kitiba ya bei ya juu huenda yasiwe ya lazima. Dakt. Garth Russell, daktari wa kiunzi, asema kwamba “asilimia 90 ya visa vya maumivu ya ghafula na makali yenye uvimbe ya mgongo (kwa kawaida yakifuatia utendaji wa kimwili) huhusisha mikaziko mibaya ya misuli ya mgongo, na yaondoshwa kwa siku mbili hadi tatu za kupumzika kitandani.” Baada ya hapo, Dakt. Russell apendekeza, “anza mazoezi yasiyo mazito na urudie utendaji wako wa kila siku.”

Michezo ya Vidio Yenye Jeuri

Michezo yenye jeuri ya vidio imeenea sana katika tamaduni za vijana, kulingana na ripoti moja katika The Vancouver Sun la Kanada. Gazeti hilo lataja uchunguzi unaoonyesha kwamba wachezaji wachanga husisimka kimwili wanapocheza michezo hiyo. Mpigo wao wa moyo huongezeka kwa kiasi kikubwa—katika visa fulani huwa zaidi ya mara mbili. Lililomhangaisha huyo mtafiti lilikuwa swali, “Je, michezo yenye jeuri ya vidio huwafanya wawe wajeuri katika maisha halisi”? Profesa wa elimu Charles Ungerleider wa Chuo Kikuu cha British Columbia aamini kwamba michezo hiyo hutoa ujumbe kwamba jeuri ndiyo njia ya kutatua matatizo. Yeye aonelea hivi: “Ni jambo linalotoa kielezi kwa jamii kwamba michezo yenye jeuri ya vidio ni aina ya kitumbuizo inayokubalika.”

Viini Vyenye Kusumbua

Maofisa wa afya katika CDC (Vitovu vya Kuzuia Magonjwa) katika Atlanta, Georgia, wana wasiwasi juu ya magonjwa ya kuambukiza katika Marekani. Kulingana na makala katika U.S.News & World Report, “tauni mpya na vilevile magonjwa ya zamani yanaenea sana.” Kwa nini? Idadi kadhaa ya visababishi imeongeza hali ya binadamu ya kuweza kupatwa na magonjwa kwa urahisi, laeleza gazeti la habari la Uswisi Neue Zürcher Zeitung. Hivyo visababishi hutia ndani ongezeko katika usafiri wa kimataifa, ambao hutokeza kuletwa kwa magonjwa katika idadi za watu wasio na kinga. Kwa kuongezea, “kinachotisha watu katika CDC,” laonelea U.S.News, “ni vijidudu vya kawaida, ambavyo wakati mmoja viliharibiwa kwa viuavijasumu, ambavyo vimeanza kushinda hata dawa mpya zaidi na zenye nguvu mno.”

Je, Ni Matokeo ya Mazingira Yenye Sumu?

Kulingana na gazeti la habari The Globe and Mail, kwa mara ya kwanza Kanada ilipata ongezeko katika kiwango cha kifo cha kitaifa cha juu zaidi kuliko ilivyotabiriwa. Badala ya ongezeko la asilimia 3 lililotabiriwa, vifo miongoni mwa Wakanada kutoka 1992 hadi 1993 viliongezeka kwa asilimia 4.3, ongezeko la juu kupita yote katika rekodi. Tarakimu zatia ndani kuongezeka kwa vifo vya vitoto, ongezeko la kwanza katika miaka 31. Maongezeko haya si ya kawaida na ni yenye kutia wasiwasi, kulingana na hiyo ripoti. Mtaalamu mmoja Mkanada alikumbushwa juu ya kifo cha ndege aina ya kanari—aliyetumiwa huko nyuma ili kuonya kuhusu gesi zenye sumu katika machimbo. “Je, hii yaweza kuwa ishara ya kwanza kwamba mazingira yanaendelea kuwa yenye sumu zaidi?” ndilo swali lililoulizwa.

Vijana Wana Maoni Hasi Kuhusu Wakati Ujao

Australia ilikuwa ikiitwa “nchi yenye bahati,” lakini idadi yenye kuongezeka ya vijana wa Australia huenda isikubali uchanganuzi huo leo. Gazeti la habari The Australian, likiripoti juu ya uchunguzi wa vijana kati ya umri wa miaka 15 na 19, lilipata kwamba vijana hao walipata “maono ‘mabaya’ ya wakati ujao wa uchumi wa Australia.” Wanafunzi katika kidato cha kwanza hadi cha tatu katika shule za serikali, za Kikatoliki, na za kibinafsi walihojiwa. “Kulingana na hiyo ripoti, matokeo yanadokeza ‘waziwazi sana’ kwamba kizazi cha wakati huu cha watu wenye umri wa miaka 15 na 16 ‘hakitazamii kwa hamu wakati ujao’—kwa kuwa wanaamini kwamba jamii inazidi kuwa yenye jeuri zaidi na ukosefu wa kazi ya kuajiriwa utabaki ukiwa juu,” gazeti hilo likasema. Walipoulizwa wafafanue jinsi maisha yao yatakavyokuwa miaka kumi ijayo, “wengi wa wenye kuhojiwa walitaja uchumi wenye kuzorota na jamii ambayo katika hiyo watu walikuwa wenye udhibiti mchache zaidi juu ya hali yao ya mbele ya kiuchumi.”

Wenye Viini vya UKIMWI Hawaelezwi

Katika Japani madaktari wanakosa kuwajulisha wenye viini vya UKIMWI kuhusu ambukizo lao, na wenzi wa ndoa wa wenye hivyo viini wameambukizwa. Baada ya kuchunguza hospitali na vituo vya kitiba 363 vya hiyo nchi, Wizara ya Afya na Huduma za Umma ilifunua kwamba ni asilimia 43 tu ya hivyo vituo hujulisha wagonjwa wote wenye viini vya UKIMWI juu ya hali yao. Asilimia 28 hivi hujulisha baadhi ya wagonjwa wao. Hospitali fulani zilikiri kukosa kuwajulisha wagonjwa kabisa, huku nyingine zikikataa kujibu swali la uchunguzi, likasema The Daily Yomiuri. Sababu moja kuu inayotolewa na madaktari ya kutofahamisha ilikuwa “hali isiyosawazika mno ya kiakili” ya wenye viini hivyo.

Jambo Jipya Kwenye Soko la Ngamia

Ingawa watalii hutafuta kuona vitu visivyo vya kawaida wanaposafiri, wao wenyewe huenda wakaonekana kuwa wasio wa kawaida kwa wakazi wenyeji. International Herald Tribune laripoti kwamba watalii kutoka nchi za Magharibi wamegundua kile ambacho huenda kiwe soko la ngamia lililo kubwa kuliko yote ulimwenguni katika jiji la Pushkar la jangwa la kaskazini, India. Huko, wafanya biashara wa ngamia huona wageni wao wa kutoka nje kuwa wenye kufurahisha. Tribune laeleza kwamba “wenye ngamia hushangazwa na jamii hii ambayo hugeuka kuwa nyekundu chini ya jua la jangwa, hutazama ulimwengu kupitia visanduku vyeusi mbele ya nyuso zao [kamera] na wako tayari kulipa dola mbili (zaidi ya mshahara wa siku mbili kwa wengi wa wakulima wa jangwani) kwa ajili ya kubebwa kwa saa moja juu ya ngamia anayejikokota.” Alipoulizwa ikiwa idadi inayoongezeka ya watalii ni nzuri au mbaya, mfanya biashara mmoja wa ngamia alijibu: “Ni nzuri. Tunapenda kuwatazama.”

Viwango Vyenye Kuzorota vya China

“Kushughulikia mno utajiri kunatisha msingi wa jamii ya Kichina, familia,” laripoti The Wall Street Journal. “Familia zinavunjika, zikitokeza ‘kizazi cha mimi kwanza’ chenye ubinafsi cha vijana. Uhalifu na ufisadi ziko katika kiwango kipitacho cha kawaida.” Watoto ambao mbeleni waliwastahi wazazi wao sasa wanawatumia kama watumwa na hawako tayari kuwatunza katika umri wao wa uzeeni, asema mtafiti mmoja. Ingawa wengi katika China bado wanashikilia viwango vya kidesturi, hivi viwango vinazorota huku mamilioni yakiacha makao yao ili kutafuta kazi mahali penginepo. “Kufuatia pesa kumekuwa mradi. Watu wako tayari kupuuza mambo mazuri, kupuuza maadili ya kijamii, kwa sababu ya pesa,” asema makamu wa waziri wa usalama wa umma Bai Jingfu.

Aina Mpya

Wakitafuta aina mpya za mimea, wanabotania Waingereza na Wabrazili wamekuwa wakivinjari mlima mmoja katika kaskazini-mashariki mwa Brazili kwa zaidi ya miaka 20. Kufikia sasa wamevumbua aina za mimea zenye kushangaza 131 ambazo hazikujulikana mbeleni, zote zikikua katika eneo la kilometa 171 za mraba tu. Hili “shamba la Edeni,” kama gazeti la habari Folha de São Paulo linavyoita mahali hapo, hukua kwenye mlima Pico das Almas wenye kimo cha meta 1,960 katika jimbo la Brazili la Bahia. Wanabotania walikagua mkusanyo wa mimea ipatayo 3,500 iliyokaushwa ili kuhakikisha kama mimea yote hii ilikuwa uvumbuzi mpya kikweli—na ndivyo ilivyokuwa. Simon Mayo wa Royal Botanic Gardens ya Uingereza aliambia hilo gazeti la habari hivi: “Inashangaza kuvumbua mimea mingi mno mwishoni mwa karne ya ishirini.”

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki