Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g96 2/8 kur. 3-4
  • Je, Kuna Yeyote Awezaye Kutumainiwa?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Je, Kuna Yeyote Awezaye Kutumainiwa?
  • Amkeni!—1996
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Tumaini Laharibiwa Kila Mahali
  • Kuwatumaini Wengine Ni Muhimu kwa Maisha Yenye Furaha
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2003
  • Je, Tunaweza Kumtumaini Yeyote?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2003
  • Unaweza Kuwatumaini Ndugu Zako
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova (Funzo)—2022
  • Ninaweza Kufanya Nini Ili Wazazi Wangu Waniamini?
    Vijana Huuliza
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1996
g96 2/8 kur. 3-4

Je, Kuna Yeyote Awezaye Kutumainiwa?

“ALIKUWA mmoja wa watu wachache nje ya familia ambao wazazi wangu walimtumaini kikamili. . . . Alijionyesha kuwa mtu mwema na mwenye kujali ambaye hangefanya lolote kamwe kutuumiza. . . . Alikuwa mmoja wa watu wachache maishani mwangu ambao nilikuja kutumaini kabisa.”

HIVYO ndivyo mwanamke mmoja kijana afafanuavyo tumaini alilokuwa nalo kwa daktari wa familia yao. Kwa kuhuzunisha, lilikuwa tumaini lililowekwa mahali pasipofaa kukiwa na matokeo hatari. Tangu alipokuwa na umri wa miaka 16, daktari huyo alimtenda vibaya kingono. “Yeye alinidanganya na kunihadaa,” akawaambia wenye mamlaka ya mahakama ambao walitekeleza haki hatimaye.—The Toronto Star.

Tumaini Laharibiwa Kila Mahali

Tumaini, kama ua lenye kuvutia lakini liharibikalo kwa urahisi, laweza kung’olewa na kukanyagwa-kanyagwa kwa miguu. Linavunjwa-vunjwa kila mahali! Michael Gaine, ambaye alikuwa katibu wa kadinali na askofu mkuu katika Uingereza alisema hivi: “Kulikuwa na wakati ambapo kila mtu alimtumaini kasisi. Wakati ambapo familia zilikuwa zikiacha watoto wao katika utunzi wake. Singetazamia hilo sasa. Tumetenganishwa na tumaini hilo milele.”—The Guardian Weekend.

Watu wa biashara hupunja washindani. Watangazaji wa bidhaa hupotosha na kutumia wateja kwa kujifaidi. Ofisa mmoja sugu aliibia kampuni yake mwenyewe fedha za malipo ya wakati wa uzeeni, akinyang’anya wafanyikazi wake akiba ya fedha. Wafanyikazi huibia waajiri wao kwa ukawaida. Kwa kielelezo, ripoti moja ilionelea kwamba “biashara za Kanada hupoteza kiasi kikadiriwacho cha dola bilioni 20 kwa mwaka kutokana na wizi wa ndani.”—Canadian Business.

Si wanasiasa wote wasiotumainika. Lakini ripoti kama hii ifuatayo haishangazi watu wengi: “Majuma mawili baada ya kuuawa kwa mmoja wa wanasiasa wanawake wabishani sana wa Ufaransa, polisi wanafunua hila za kisiasa na njama za kihalifu ambazo zimefunika kwa muda mrefu sehemu ya shughuli za serikali kwenye pwani ya Mediterania.”—The Sunday Times, London.

Mara nyingi, katika mahusiano ya karibu tumaini huvunjwa. Waume na wake hukosa kuwa waaminifu kingono kwa wenzio. Wazazi hutenda watoto vibaya. Watoto hudanganya wazazi. Habari zilizohifadhiwa za Stasi, polisi wa siri katika ile iliyokuwa Ujerumani Mashariki, zilipofunguliwa, zilifunua “mfumo wa hila ulioenea kila mahali” wa watu walioonwa kuwa marafiki. Katika mzingo wa usaliti, yasema ripoti moja, “Udhibiti wa kikatili wa Stasi ulienea hadi katika darasa la shule, jukwaa la kuhubiria, chumba cha kulala, hata katika chumba cha kuungama.”—Time.

Katika Ireland mwanasafu mmoja aliandika hivi: “Tumedanganywa, tumepotoshwa na tumetumiwa na kutumiwa vibaya na kudharauliwa na wale ambao tuliwaweka katika vyeo vya mamlaka.” (The Kerryman) Kwa sababu mara nyingi wao wamesalitiwa, watu wengi hawamtumaini mtu yeyote. Twaweza kufanya nini ili kuhakikisha kwamba tumaini letu halijawekwa mahali pasipofaa? Makala mbili zifuatazo zitachunguza swali hili.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki