Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g96 4/8 uku. 31
  • Kujitahidi Kufikia kwa Mikono Itoayo Ishara

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kujitahidi Kufikia kwa Mikono Itoayo Ishara
  • Amkeni!—1996
  • Habari Zinazolingana
  • Uwe Macho Kutafuta Viziwi Katika Eneo Lenu
    Huduma Yetu ya Ufalme—2001
  • ‘Yehova Ameufanya Uso Wake Ung’ae Kuwaelekea’
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2009
  • Yehova Alithawabisha Kazi ya Mikono Yangu
    Masimulizi ya Maisha ya Mashahidi wa Yehova
  • Jinsi Mungu Anavyowajali Viziwi
    Habari Zaidi
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1996
g96 4/8 uku. 31

Kujitahidi Kufikia kwa Mikono Itoayo Ishara

KUANZIA mwezi wa Juni 1995 na kuendelea katika kiangazi chote, Mashahidi wa Yehova chini ya eneo la tawi la Marekani, walikuwa na mikusanyiko ya wilaya 181 yenye kichwa “Wasifaji Wenye Shangwe.” Kwenye miwili kati yayo—mmoja upande wa mashariki na mwingine upande wa magharibi—programu nzima ilitolewa moja kwa moja katika Lugha ya Ishara ya Marekani. Hivyo, ueleweshaji wa programu ulizidishwa—kwa kuwa utoaji wa moja kwa moja kwa viziwi katika lugha ya ishara unaeleweka zaidi kuliko ufasili wa maneno ya kuongewa.

Wajumbe walikuwapo kutoka makutaniko 11 ya lugha ya ishara na vikundi 30 hivi vya lugha ya ishara katika Marekani. Lakini waliokuwapo pia ni wajumbe kutoka Denmark, Ekuado, Jamhuri ya Dominika, Japani, Kanada, Mexico, Norway, Puerto Riko, Uingereza, Ujerumani, na Urusi. Hivyo, kulikuwako na hali ya kimataifa.

Viwambo vya vidio viliwekwa ili programu iweze kuonyeshwa kupitia televisheni kadhaa zilizounganishwa. Hata hivyo, wajumbe kadhaa walikuwa viziwi na pia vipofu. Watu hawa wangenufaikaje na programu? Ilichochea kwelikweli kuona wajitoleaji zaidi ya mia moja wakitwaa duru ya kuwasilisha programu ya kila siku kwao kupitia ufasili wa kugusa.

Kwenye mikusanyiko hii miwili, 36 walionyesha wakfu wao kwa Yehova Mungu kupitia ubatizo. Jambo jingine kuu lilikuwa ile drama, Kuheshimu Wastahiki Katika Miaka Yao ya Uzee. Ilisisimua kama nini kuwa na utoaji wa drama hii nzima katika lugha ya ishara, ikiruhusu washiriki viziwi kuwa na sehemu kubwa katika utoaji huu!

Kisha kikaja kitolewaji cha msaada mpya wa kujifunza Biblia, kitabu Ujuzi Uongozao Kwenye Uhai Udumuo Milele. Wakusanyikaji walifurahi hasa kujua kwamba nakili ya lugha ya ishara ya kitabu hiki imefanywa ipatikane kwenye ukanda wa vidio! Sehemu ya 1, ilitolewa mkusanyikoni, ina sura nne za kwanza. Sehemu nyingine tano zitafuata. “Twashukuru sana kwa vidio hii mpya,” akasema mjumbe mmoja kutoka Ohio. “Itatusaidia kuharakisha kazi katika maeneo ya viziwi.”

Wale 2,621 waliohudhuria mikusanyiko hii miwili walirudi nyumbani wakiwa wameburudishwa kiroho. Kupita wakati mwingine wowote, waliazimia kufuatisha yale maneno ya mtunga-zaburi: “Kila mwenye pumzi na amsifu BWANA. Haleluya.”—Zaburi 150:6.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki