Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g96 4/22 kur. 8-11
  • Ulimwengu Usio na Vita U Karibu

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Ulimwengu Usio na Vita U Karibu
  • Amkeni!—1996
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Kuwaita Wapendao Amani
  • “Siku za Mwisho”
  • Ulimwengu Usio na Vita
  • Siku za Mwisho—Ni Nini Kitakachofuata?
    Amkeni!—2008
  • Tafuta Sana Amani ya Kweli na Kuifuatia!
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1997
  • Amani Duniani—Itapatikanaje?
    Maswali ya Biblia Yajibiwa
  • Watu Wote Watakapopendana
    Amkeni!—1998
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1996
g96 4/22 kur. 8-11

Ulimwengu Usio na Vita U Karibu

TAZAMA tena unabii wa Biblia katika Isaya unaosema: “Watafua panga zao ziwe majembe, na mikuki yao iwe miundu; taifa halitainua upanga juu ya taifa lingine, wala hawatajifunza vita tena kamwe.” Ona kutokana na muktadha kwamba wale wanaofua panga zao ziwe majembe ni “mataifa mengi” ambayo hutembea katika njia za Mungu. (Isaya 2:2-4) Hili lamaanisha kwamba watu hawa humwabudu Yehova Mungu na kutii sheria zake. Wao ni nani?

Lazima wawe watu wa mataifa mengi ambao hawajakataa silaha za vita tu bali ambao wameondoa kabisa kutoka akilini mwao na mioyoni mwao mitazamo na mielekeo inayoongoza kwenye uadui na kupigana. (Warumi 12:2) Badala ya kumwua jirani yao, wao wanampenda. (Mathayo 22:36-39) Je, umesikia juu ya watu kama hao?

Labda umesikia kwamba Mashahidi wa Yehova hufurahia udugu wa kimataifa na wamekataa kuchukua silaha ili kuua wengine. Fikiria jambo hilo: Ikiwa kila mtu duniani angekuwa na mtazamo huo, je, sayari hii haingekuwa tayari mahali pa amani na usalama?

Bila shaka, si kila mtu ana mtazamo huo. Ni kama alivyoandika Mfalme Sulemani miaka 3,000 hivi iliyopita: “Nikarudi na kuona madhalimu yote yanayotendeka chini ya jua; na tazama, machozi yao waliodhulumiwa, ambao walikuwa hawana mfariji, na upande wa wale waliowadhulumu kulikuwa na uwezo.”—Mhubiri 4:1.

Kuwaita Wapendao Amani

Je, kutapata kuwako na ulimwengu usio na vita? Ndiyo. Je, utakuja kupitia jitihada za wanadamu? La. Je, utakuja kupitia kugeuzwa kwa watu wengi kuelekea dini ya kweli? La. Kitabu cha Biblia cha Zaburi hujibu hivi: “Njoni, nyinyi watu, tazameni matendo ya Yehova . . . Afanya vita vikome hadi mwisho wa dunia.”—Zaburi 46:8, 9, NW.

Yehova Mungu atafanyaje hivyo? Kitabu cha Mithali hujibu: “Wanyofu watakaa katika nchi, na wakamilifu watadumu ndani yake. Bali waovu [wale wasioheshimu sheria za Mungu] watatengwa na nchi, nao wafanyao hila watang’olewa.”—Mithali 2:21, 22.

Sababu kuu ambayo imefanya Mungu asitende kabla ya wakati huu ni hii: Yeye anawapa watu fursa ya kujifunza kuhusu njia zake ili watembee katika njia zake. Mtume Petro aliandika: “Bwana hakawii kuitimiza ahadi yake, kama wengine wanavyokudhani kukawia, bali huvumilia kwenu, maana hapendi mtu ye yote apotee, bali wote wafikilie toba.” (2 Petro 3:9) Hivyo, watu wa Mungu husaidia wengine bila ubinafsi wajifunze juu ya Yehova. Kama alivyoonyesha Isaya, wao waita: “Njoni, twende juu mlimani kwa BWANA, . . . naye atatufundisha njia zake.”—Isaya 2:3.

“Siku za Mwisho”

Andiko katika Isaya lilitabiri kwamba kuelimisha watu katika njia za amani kungetukia “katika siku za mwisho.” (Isaya 2:2) Twaishi katika wakati huo sasa hivi. Kwa kushangaza, vita vya karne hii huonyesha hivyo.

Wanafunzi wa Yesu walipomwuliza ni nini kingeonyesha mwisho wa mfumo huu wa mambo, yeye alitabiri “matetemeko makubwa ya nchi; na njaa na tauni mahali mahali.” (Luka 21:11; Mathayo 24:3) Yeye alisema pia: “Mtakaposikia habari za vita na fitina, msitishwe; maana, hayo hayana budi kutukia kwanza, lakini ule mwisho hauji upesi. Kisha aliwaambia, Taifa litaondoka kupigana na taifa, na ufalme kupigana na ufalme.”—Luka 21:9, 10.

Ingawa kumekuwa na vita kwa maelfu ya miaka, karne hii pekee imekuwa na vita viwili vya ulimwengu na, kulingana na makadirio fulani, kihalisi kumekuwa na mamia ya vita vidogo-vidogo. Uhakika wa kwamba makumi ya mamilioni ya watu ambao wameuawa katika vita katika karne hii ni wenye kuhuzunisha. Kulingana na gazeti World Watch, katika miaka 2,000 kabla ya karne ya 20, kwa wastani, ilichukua miaka 50 watu milioni moja kufa vitani. Katika karne hii, urefu wa wakati uliochukua, kwa wastani, watu milioni moja kufa vitani ulikuwa mwaka mmoja.

Ulimwengu Usio na Vita

Vita vibaya vya karne yetu, pamoja na mambo mengine mengi yaliyotabiriwa katika unabii wa Biblia, huonyesha kwamba tuko karibu na ulimwengu mpya utakaofanyizwa na Mungu. Ukosefu wa utaratibu wa ulimwengu huu utafagiliwa mbali na mahali pao pachukuliwe na “dunia mpya,” ambapo amani na uadilifu zitakaa. (2 Petro 3:13, NW) Neno la Mungu lasema: “Watenda mabaya wataharibiwa, bali wamngojao BWANA ndio watakaoirithi nchi. Bali wenye upole watairithi nchi, watajifurahisha kwa wingi wa amani.”—Zaburi 37:9, 11.

Kotekote duniani leo, mamilioni yasiyohesabika hutamani ulimwengu usio na vita. Akionyesha kwamba Mungu atatimiza kwa hakika ahadi yake ya kuumba ulimwengu huo, nabii wa Mungu kitambo sana aliandika hivi: “Njozi hii bado ni kwa wakati ulioamriwa, inafanya haraka ili kuufikilia mwisho wake, wala haitasema uongo, ijapokawia, ingojee; kwa kuwa haina budi kuja, haitakawia.”—Habakuki 2:3.

Kwa hivyo, kwa hekima mtumaini Mungu na ufurahie utimizo wa ahadi yake: “Naye Mungu mwenyewe atakuwa pamoja nao [watu wake]. Naye atafuta kila chozi katika macho yao, wala mauti haitakuwapo tena; wala maombolezo, wala kilio, wala maumivu hayatakuwapo tena; kwa kuwa mambo ya kwanza yamekwisha kupita.”—Ufunuo 21:3, 4.

[Sanduku/Picha katika ukurasa wa9, 10]

Kile Inachoahidi Biblia kwa Ulimwengu Huo Mpya:

Hakuna Uhalifu, Jeuri, au Uovu

“[Mungu] avikomesha vita hata mwisho wa dunia.”—Zaburi 46:9.

“Watenda mabaya wataharibiwa, . . . Maana bado kitambo kidogo asiye haki hatakuwapo.”—Zaburi 37:9, 10.

Jamii Yote ya Kibinadamu Yaishi kwa Amani

“Kwa ajili yetu mtoto amezaliwa, tumepewa mtoto mwanamume; na uweza wa kifalme utakuwa begani mwake; naye ataitwa jina lake, . . . Mfalme wa amani. Maongeo ya enzi yake na amani hayatakuwa na mwisho kamwe.” —Isaya 9:6, 7.

Dunia Yote Yawa Paradiso

Yesu alisema: “Utakuwa pamoja nami katika Paradiso.”—Luka 23:43, New World Translation

“Wenye haki watairithi nchi, nao watakaa humo milele.”—Zaburi 37:29.

Udugu Wenye Upendo wa Ulimwenguni Pote

“Mungu hana upendeleo; bali katika kila taifa mtu amchaye na kutenda haki hukubaliwa na yeye.”—Matendo 10:34, 35.

[Picha katika ukurasa wa10]

Ufufuo wa Wapendwa Waliokufa

“Saa yaja, ambayo watu wote waliomo makaburini wataisikia sauti yake [Yesu]. Nao watatoka.”—Yohana 5:28, 29.

Hakuna Ugonjwa, Uzee, au Kifo Tena

“Atafuta kila chozi katika macho yao, wala mauti haitakuwapo tena; wala maombolezo, wala kilio, wala maumivu hayatakuwapo tena; kwa kuwa mambo ya kwanza yamekwisha kupita.”—Ufunuo 21:4.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki