Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g96 7/22 uku. 31
  • Mkuu wa Mbio

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Mkuu wa Mbio
  • Amkeni!—1996
  • Habari Zinazolingana
  • Duma—Paka Mwenye Mbio Zaidi
    Amkeni!—1997
  • ‘Umeumbwa kwa Njia ya Ajabu’!
    Amkeni!—2011
  • Kwa Nini Wamo Hatarini?
    Amkeni!—2004
  • Jinsi Wanyama Wanavyowalisha na Kuwatunza Watoto Wao
    Amkeni!—2005
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1996
g96 7/22 uku. 31

Mkuu wa Mbio

Na mleta-habari wa Amkeni! katika Afrika Kusini

NI NANI mwenye cheo hicho? Duma, mnyama mwenye mbio ya kasi zaidi ulimwenguni kwa mwendo mfupi. Kila duma ana kigezo chake mwenyewe cha madoadoa—ndiposa akapata jina duma, ambalo kwa Kisanskriti humaanisha “mwili wenye madoadoa.”

Wengine husema kwamba umwonapo kwa mara ya kwanza, paka huyo huonekana kana kwamba ana miguu mirefu sana. Wengine husema kwamba mgongo wake umeinama na kichwa chake ni kidogo mno. Lakini hali hizo hasa humfaidi duma. Miguu mirefu ya nyuma huandaa nguvu, ikimwezesha duma atembee kwa utaratibu na kukimbia kwa madaha. Na mnyama huyu aweza kutimua mbio kama nini! Kutoka hali ya kusimama, kwa sekunde chache duma aweza kufikia karibu mwendo wa kilometa 110 kwa saa.

Duma ameumbwa vizuri kwa ajili ya mwendo wa kasi zaidi. Mifupa yake iliyo myepesi yatia ndani uti wa mgongo upindao isivyo kawaida, ambao huweza kujikunja na kujikunjua kama springi. Duma pia amepewa kifua kikubwa, mapafu makubwa, moyo wenye nguvu, mkia unaompa usawaziko, na mianzi mikubwa ya pua ambayo humruhusu apumue haraka-haraka—yote yakichangia wepesi usio na kifani wa mnyama huyo. Hata hivyo, mbio ya kasi ya duma ni ya muda mfupi. Baada ya meta 400 tu ya mwendo wa kasi kabisa, ni lazima atue na kujituliza.

Mara nyingi duma si tisho kwa wanadamu. Ann van Dyk, ambaye amekuwa akilea duma kwa miaka mingi, aandika katika kitabu chake The Cheetahs of De Wildt: “Baada ya kuwalisha, nilipenda kutumia muda mchache kabla ya giza kuingia nikiwa pamoja na familia yangu ya paka hao. Hisia ya kutumainiana ilikuwa imekua kati yetu na ingawa hawakuwa wa kufugwa, nilijua hawangenidhuru.”

Hata hivyo, wanadamu hawajakuwa wenye fadhili sana kwa duma. Kwa kielelezo, wawindaji katika Afrika walipenda sana ngozi yake nzuri sana, na kutwaliwa kwa ardhi kumemwachia duma sehemu kidogo ya kukimbia. Hilo limepunguza sana idadi ya duma. Ingawa pindi moja walikuwa wamejaa sana India, duma walitokomea huko 1952. Pia hawapatikani tena katika nchi fulani zinazopakana na mashariki mwa Mediterenia.

Twaweza kufurahi kama nini kwamba katika ulimwengu mpya wa Mungu, wanyama hawatatishwa tena na wanadamu wenye pupa! (Isaya 11:6-9) Labda wakati huo utakuwa na pendeleo la kuona mkuu huyu wa mbio aliyeumbwa kwa njia nzuri ajabu, duma.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki