Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g 5/11 uku. 3
  • ‘Umeumbwa kwa Njia ya Ajabu’!

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • ‘Umeumbwa kwa Njia ya Ajabu’!
  • Amkeni!—2011
  • Habari Zinazolingana
  • Michezo ya Olimpiki ya Norway—Je, Ile Miradi Ilitosha?
    Amkeni!—1994
  • Mambo Unayopaswa Kujua Kuhusiana na Kuokoa Nishati
    Amkeni!—2017
  • Mkuu wa Mbio
    Amkeni!—1996
  • Malengo ya Olimpiki Yanazorota
    Amkeni!—2000
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—2011
g 5/11 uku. 3

‘Umeumbwa kwa Njia ya Ajabu’!

UNAPOFIKIRIA kuhusu uwezo wa ajabu wa wanyama mbalimbali, je, nyakati nyingine wewe huwaonea wivu? Labda wewe hutamani kwamba ungeweza kupaa kama albatrosi, kuogelea kama pomboo, kuona kama tai, au kukimbia kwa kasi kama duma.

Naam, wanyama wana uwezo fulani wa ajabu. Lakini sisi pia tuna uwezo wa ajabu! Kwa kweli, mwili wa mwanadamu umefafanuliwa kuwa mashini bora zaidi. Lakini sisi si mashini tu. Tuna uwezo wa kubuni, kudadisi, kufikiri, na kutumia akili—sifa ambazo zinatuwezesha kutengeneza mashini ambazo zinaweza kufanya chochote tunachotaka. Tunaweza kuruka kwa kasi hata kuliko mwendo wa sauti; tunaweza kusafiri ndani ya bahari kubwa sana, juu au chini ya maji; tunaweza kuona umbali wa miaka bilioni 14 hivi ya nuru ndani ya anga za juu; tunaweza kutazama ndani ya chembe iliyo hai; na tunaweza kutengeneza dawa, mbinu za matibabu, na vifaa vya kutusaidia kutambua na kutibu magonjwa.

Hata bila msaada wa mashini, wanadamu wenye afya na waliozoezwa vizuri wanaweza kufanya mambo ya ajabu. Kwa mfano, katika Michezo ya Olimpiki, wanasarakasi, watu wanaoruka kutoka juu sana hadi ndani ya kidimbwi, watu wanaoteleza kwenye barafu, na wengine hufanya mambo ya ajabu kwa wepesi, ustadi, ubunifu, na madaha yanayowashangaza watazamaji.

Je, unathamini zawadi za pekee ulizo nazo? Ni kweli kwamba huenda wewe si mwanamichezo wa Olimpiki, lakini una vipawa vingi ambavyo unapaswa kushukuru kwamba umepewa. Mwandikaji wa Biblia wa kale alimshukuru Mungu hivi katika wimbo: “Nitakusifu kwa sababu nimeumbwa kwa njia ya ajabu yenye kuogopesha.”a (Zaburi 139:14) Mbona usifikirie kuhusu maneno hayo unaposoma habari zifuatazo? Zitazungumzia kwa undani zaidi maajabu fulani ya mwili wa mwanadamu, kutia ndani sifa nyingine muhimu zaidi zinazotufanya tuwe watu wa pekee sana.

[Maelezo ya Chini]

a Wasomaji wanaopendezwa na masuala yanayohusu uumbaji au mageuzi wanaweza kusoma broshua Uhai—Ulitokana na Muumba? na Maswali Matano Muhimu Kuhusu Chanzo cha Uhai. Unaweza kupata broshua hizo kutoka kwa Mashahidi wa Yehova wanaoishi karibu nawe au kutoka kwa wachapishaji wa gazeti hili.

[Sanduku katika ukurasa wa 3]

TUMEUMBWA TUSIPOTEZE NISHATI

Uwezo wetu wa kusimama na kutembea tukiwa wima unasaidia tusipoteze nishati kwa kuwa mtu hutumia misuli kidogo tu kusimama wima. Kwa kweli, ‘kiwango cha nishati tunachotumia kusimama kinazidi nishati tunayotumia kulala kwa asilimia 7 tu,’ anasema mtafiti wa mfumo wa neva John R. Skoyles. Anaongezea kusema kwamba mbwa anaposimama (kwa miguu minne) yeye hutumia asilimia 70 zaidi ya nishati kuliko ile anayotumia anapolala.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki