Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g96 8/8 kur. 9-10
  • Spishi Zilizo Hatarini mwa Kutoweka—Jinsi Unavyohusika

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Spishi Zilizo Hatarini mwa Kutoweka—Jinsi Unavyohusika
  • Amkeni!—1996
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Safina ya Kuokolewa
  • Wanyama Katika Ulimwengu Mpya
  • “Alitembea Pamoja na Mungu wa Kweli”
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2013
  • Mfano wa Unabii Uliofananisha Wokovu
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1975
  • Spishi Zilizo Hatarini mwa Kutoweka—Mweneo wa Hilo Tatizo
    Amkeni!—1996
  • “Alitembea Pamoja na Mungu wa Kweli”
    Igeni Imani Yao
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1996
g96 8/8 kur. 9-10

Spishi Zilizo Hatarini mwa Kutoweka—Jinsi Unavyohusika

SIMBAMARARA, kasa, vifaru, vipepeo—yaonekana orodha ya spishi zilizo hatarini haikomi! Bila shaka utakubali kwamba ni lazima mwanadamu alaumike zaidi. Lakini jambo hilo linakuhusuje?

Kwa kutazama hali mbaya ya kiuchumi ya ulimwengu, je, inapatana na akili kutazamia watu ambao wanahangaikia hali njema zao kutegemeza miradi ya hifadhi, hata miradi hiyo iwe mizuri kama nini? “Hakika si rahisi kuhangaikia mambo ya mazingira katika sehemu kubwa ya Afrika iliyoko kusini ya Sahara, ambako mamilioni ya watu wanakabiliwa na fujo za kisiasa, vita ya kikabila, njaa kuu na maradhi ya kuenea,” lasema Time. Na ndivyo hali ilivyo kwingineko.

Mabadiliko makubwa yanahitajika ikiwa tatizo la spishi zilizo hatarini mwa kutoweka litasuluhishwa. Kulingana na The Atlas of Endangered Species, mabadiliko hayo ni “makubwa sana hivi kwamba yanaweza kufanywa na serikali tu.” Kisha chapendekeza hivi: “Mahali ambapo serikali ni zenye kuchaguliwa kwa kura, ni daraka la kila mtu kuhakikisha kwamba kufikia mwaka wa 2000 ni wanasiasa tu ambao wanahangaikia mazingira ndio wanaochaguliwa kwa kura.”

Je, hilo ni tazamio liwezalo kutimizwa? Kwa kufikiria yaliyotokea katika historia, ni lazima tukate kauli kwamba “mwanadamu ametawala mwanadamu kwa umizo lake”—na wanyama wa pori vilevile. (Mhubiri 8:9, NW) Kwa kweli, wahifadhi wengi waamini kwamba mimea na wanyama ni ishara za mambo ya mazingira. Hao wanapokuwa hatarini mwa kutoweka, hata sisi wanadamu vilevile tumo katika hatari hiyo. Lakini hii si mara ya kwanza katika historia ya kibinadamu kwamba uhai wote katika dunia umetishwa na utoweko.

Kitabu cha kale zaidi kati ya vitabu vya historia kilirekodi maneno haya: “Nitaleta gharika ya maji juu ya nchi, niharibu kila kitu chenye mwili na pumzi ya uhai, kisiwepo chini ya mbingu; kila kilichoko duniani kitakufa.” (Mwanzo 6:17) Hata hivyo, si kila binadamu na si kila aina ya uhai mwingine uliokufa, kwa sababu Mungu alipanga kuwe na njia ya kuokolewa.

Safina ya Kuokolewa

Wanasayansi wanaamini kwamba suluhisho bora kwa tatizo la spishi zilizo hatarini mwa kutoweka leo lahusisha kuhifadhi makao yao. Kwa kupendeza, New Scientist laripoti juu ya hilo na kurejezea jinsi wahifadhi wanavyotumia maneno “Safina ya Noa ya mfano.” Safina ya Noa ilikuwa ndicho chombo ambacho kwacho wanadamu na wanyama waliokoka Gharika ya siku za Noa.

Mungu alimpa Noa muundo wa safina, sanduku kubwa sana la mbao, ambalo lilipaswa kuelea juu ya maji ya furiko. Hiyo ilihifadhi uhai wa Noa, mke wake, wana wao watatu, na wake za wana hao, pamoja na wawakilishi wa aina mbalimbali za wanyama, wa mwitu na vilevile wa kufugwa—hakika, “kila chenye mwili kilicho na pumzi ya uhai ndani yake.” (Mwanzo 7:15) Aina nyingi za uhai uliopo leo zathibitisha jinsi safina ilivyotumikia kusudi layo vizuri.

Lakini, ona kwamba kuokolewa hakukutegemea jitihada za binadamu pekee. Noa na familia yake walipaswa kumtii Mungu, aliyekuwa na uwezo wa kuwahifadhi wakiwa hai. Ni Mungu aliyemaliza mzozo, jeuri, na pupa iliyojaa katika ulimwengu huo wa kabla ya Gharika.—2 Petro 3:5, 6.

Wanyama Katika Ulimwengu Mpya

Yehova Mungu ameahidi kwamba utii wa sheria zake waweza kubadili wanadamu wasiwe kama wanyama wakali wawindaji na wawe kama wanyama wapole. (Isaya 11:6-9; 65:25) Hata sasa, uthibitisho wa hilo ni tele. Hudhuria mikutano kwenye Jumba la Ufalme la Mashahidi wa Yehova lililoko karibu na wewe, na ujionee mwenyewe. Ikiwa Yehova aweza kutimiza mabadiliko hayo makubwa miongoni mwa binadamu, je, yeye hawezi pia kupanga jamii ya wanyama kuishi pamoja kwa amani na usalama, hata kama hiyo inamaanisha kubadili tabia zao za sasa? Kwa hakika yeye aahidi hivi: “Nitafanya agano na wanyama wa mashamba . . . , tena na ndege wa angani, tena na wadudu wa nchi; . . . nami nitawalalisha salama salimini.”—Hosea 2:18.

Mtume Petro aliandika juu ya “siku ya hukumu [ya wakati ujao], na ya kuangamia kwao wanadamu wasiomcha Mungu.” (2 Petro 3:7) Mwingilio wa Mungu uliodhibitiwa utaangamiza wanadamu wasiomhofu pekee. Mungu ‘atawaharibu hao waiharibuo nchi.’—Ufunuo 11:18.

Ebu wazia jinsi itakavyokuwa shangwe kuishi katika ulimwengu ambamo viumbe hawamo hatarini tena. Kutakuwa na mengi ya kujifunza kama nini kutokana na wanyama wa pori ambao watakuwa wametuzingira wakati huo! Ndiyo, simbamarara, simba, tembo, wataenda huku na huku bila kusumbuliwa. Viumbe vya bahari vitasitawi, kama ilivyo na wanyama-watambazi, wadudu, na aina mbalimbali za ndege, kutia ndani kasuku-mkia—wote wakisawazishwa vizuri kiikolojia. Huku wanadamu watiifu wakiwa wamerudishwa kwenye ukamilifu wa kibinadamu chini ya Ufalme wa Kimesiya, makao yenye mazingira kamilifu ya kuishi yataenea.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki