Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g96 9/22 uku. 25
  • Kutano Lenye Kushangaza Sana

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kutano Lenye Kushangaza Sana
  • Amkeni!—1996
  • Habari Zinazolingana
  • Kutafuta Pomboo Huko New Zealand
    Amkeni!—2002
  • Mambo ya Kurudia na Familia
    Amkeni!—2005
  • Shark Bay—Eneo la Ajabu la Baharini
    Amkeni!—2007
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
    Amkeni!—2002
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1996
g96 9/22 uku. 25

Kutano Lenye Kushangaza Sana

“JAMBO lenye kusisimua zaidi ambalo nimepata kufanya maishani mwangu!” Hivyo ndivyo Kristie alivyofafanua jinsi alivyokutana na dolfini kwa njia ya kushangaza. Je, ndivyo ungalihisi ikiwa ungaliweza kuogelea pamoja na dolfini katika Ghuba ya Mexico?

Kila mtu husisimuka akiwaona dolfini wakiogelea au wakifanya tamasha za majini, kama vile kutembea kinyume-nyume kwa mikia yao, kuruka juu sana kutoka majini, au kuruhusu wanadamu wawapande. Kutazama tu maonyesho hayo kwaweza kumfanya mtu ahisi kuingia majini na kucheza na hao dolfini.

Sikuzote Kristie alikuwa amehisi hivyo. Kisha siku moja, alipokuwa akiendesha boti na kuogelea katika Ghuba ya Mexico, kwa ghafula kichwa fulani kikajitokeza mbele yake. Upesi, ikaonekana kwamba dolfini watatu wadadisi walikuwa wanafikiri wamepata mwenzi wa mchezo. Mwanzoni, Kristie aliogopa kidogo, lakini woga wake ukageuka kuwa msisimko alipoanza kucheza na hao dolfini. Akatulia, akiwaacha watawale mchezo, akitaka kuona watafanya nini.

Kristie alisema: “Dolfini alijitokeza tu mbele yangu—na ghafula, tulikuwa tukitazamana. Nikajikuta nikimpapasa-papasa na kuzungumza naye—kama ambavyo ningefanya na mbwa wangu.”

Kwa sababu dolfini ni wenye akili, wao ni watumbuizaji wanaopendwa sana, na wakufunzi wao wengi husema kwamba kwa sababu ya urafiki wao kwa watu, si lazima dolfini wahongwe kwa chakula ndipo wafanye tamasha zao.

Alipoulizwa ni nini kitu chenye kufurahisha zaidi katika kushughulika na dolfini, Liz Morris, ambaye ni mtaalamu wa tabia ya wanyama katika Sea World katika Florida, Marekani, alisema: “Nafikiri ni maumbile yao. Kwa sababu wao ni wenye michezo na ni wadadisi sana kimaumbile, unaweza kusitawisha sana uhusiano wenye ukaribu nao . . . Wao huitikia vizuri sana wakiguswa na kuonyeshwa upendo.” Katika mfumo mpya wa Mungu ulioahidiwa, sote tutaweza kukutana nao kwa njia ya kushangaza sana kama alivyofanya Kristie.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki