Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g96 9/22 kur. 24-25
  • Kifungo Kilichopo Kati ya Mama na Watoto Wake

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kifungo Kilichopo Kati ya Mama na Watoto Wake
  • Amkeni!—1996
  • Habari Zinazolingana
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
    Amkeni!—1997
  • “Sijawahi Kamwe Kuhisi Upendo Kama Huu”
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2008
  • “Nimeshika Imani”
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1994
  • Binti Halisi wa Sara
    2016 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1996
g96 9/22 kur. 24-25

Kifungo Kilichopo Kati ya Mama na Watoto Wake

ALIKUWA tu paka asiye na makao wala jina, mwenye manyoya mafupi na watoto watano, aliyekuwa akijaribu kupata riziki katika mtaa wa hali ya chini wa East New York. Alikuwa anaishi katika gereji moja mbovu ambayo haikuwa inatumiwa na ambayo mara nyingi ilishika mioto yenye kutilika shaka. Alitafuta-tafuta katika ujirani takataka za chakula ambazo zingemwezesha kulisha watoto wake wanaokua.

Hayo yote yalikuwa karibu kubadilika saa 12:06 za asubuhi katika Machi 29, 1996. Moto wenye kutilika shaka ulifunika haraka gereji hiyo. Makao ya familia ya paka huyo yakashika moto. Kikosi cha zima-moto cha Ladder Company 175 kilikuja na upesi kikazima huo moto. David Giannelli, mmoja wa zima-moto, akasikia vilio vya watoto wa paka. Akapata watatu nje tu ya jengo, na mwingine umbali wa robo tatu kuvuka barabara, na wa tano kwenye kijia cha kando ya barabara. Watoto hao walikuwa wachanga mno kuweza kutoroka peke yao. Giannelli akagundua kwamba kuchomeka kwa kila mtoto kulikuwa kubaya kuliko kwa yule mwingine, wengine wakiwa walilazimika kungoja muda mrefu zaidi waokolewe huku mama yao akiwabeba mmoja-mmoja.

Hilo simulizi katika Daily News la New York la Aprili 7, 1996, lilitoa ripoti hii juu ya mahali alipokuwa mama na utunzaji wake wenye upendo: “Giannelli alimpata mama amelala kifudifudi akiwa na maumivu katika mahali palipo wazi, akahuzunika sana alipomwona. Kope za macho yake zilikuwa zimefura na kujifunika kwa sababu ya moshi. Nyayo zake zilikuwa zimechomeka vibaya. Kulikuwa na alama mbaya sana za kuchomeka usoni mwake, katika masikio na miguuni. Giannelli akapata katoni. Kwa uanana akamweka mama na watoto wake ndani. ‘Hata alishindwa kufumbua macho yake,’ akasema Giannelli. ‘Lakini akawagusa mmoja-mmoja kwa mguu wake, akiwahesabu.’”

Walipofika makao ya kutunza wanyama ya North Shore Animal League, walikuwa katika hali mbaya sana. Simulizi hilo likaendelea kusema: “Dawa za kupambana na mshtuko zilitumiwa. Neli iliyojazwa viuavijasumu iliunganishwa kwenye mwili wa paka huyo hodari. Dawa za kupaka za viuavijasumu zilipakwa katika sehemu ambazo alikuwa amechomeka. Kisha akawekwa kwenye kizimba cha tangi la oksijeni ili kumsaidia kupumua huku wafanyakazi wote wa makao hayo wakingoja kwa hamu kuona matokeo . . . Baada ya muda wa saa 48, huyo shujaa alikuwa akiketi. Macho yake yaliyofura yalifunguka na madaktari wakapata kwamba hayakupata madhara yoyote.”

Ebu tua na ufikiri. Chukua muda upige picha akilini mama huyo mwenye moyo mkuu, mwenye kuogopa moto kiasili, akiingia katika jengo lenye kujaa moshi na kuchomeka ili aokoe watoto wake wanaolia. Kwenda pindi moja kubeba watoto wake wadogo wasiojiweza ni jambo la kushangaza sana; lakini kufanya hivyo mara tano, kila pindi kwa maumivu ya kuchomeka zaidi kwa miguu na uso, ni ajabu sana! Mnyama huyo hodari alipewa jina Mwekundu kwa sababu kuchomeka kulionyesha kwamba ngozi yake ilikuwa na rangi nyekundu.

Simulizi hili lenye kugusa moyo la kifungo kilichopo kati ya mama na watoto wake lilipotangazwa ulimwenguni kote kutoka makao ya North Shore Animal League, simu zikaanza kulia daima. Zaidi ya watu 6,000 kutoka mbali kama Japani, Uholanzi, na Afrika Kusini walipiga simu kujua hali ya Mwekundu. Watu wapatao 1,500 wamejitolea kufuga Mwekundu na watoto wake. Mtoto mmoja alikufa baadaye.

Mwekundu aligusa mioyo ya watu ulimwenguni kote. Ni jambo linalofanya ujiulize ikiwa mamilioni ya akina mama leo ambayo huharibu mimba watoto wakiwa wangali tumboni au kuua watoto muda mfupi baada ya kuzaa, kwa kuwatenda vibaya, hayaguswi moyo na kielelezo cha Mwekundu cha kifungo kilichopo kati ya mama na watoto wake.

[Hisani ya Picha katika ukurasa wa 24]

North Shore Animal League

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki