Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g96 10/8 kur. 28-29
  • Kuutazama Ulimwengu

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kuutazama Ulimwengu
  • Amkeni!—1996
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Utumizi wa Tumbaku
  • Vijana na Bunduki
  • Vitabia vya Ujiuaji-Kimakusudi
  • Kujifunza Jeuri
  • Uhaba wa Makasisi Katika Ufaransa Waongezeka
  • Saa Iliyo Sahihi Kuliko Zote Ulimwenguni
  • Sandwichi ya Hali ya Chini?
  • Biashara ya Asia ya Ngono ya Watoto
  • Uadui au Muungano?
  • Kuutazama Ulimwengu
    Amkeni!—1997
  • Kuutazama Ulimwengu
    Amkeni!—1995
  • Kujiua—Pigo la Vijana
    Amkeni!—1998
  • Kuutazama Ulimwengu
    Amkeni!—2000
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1996
g96 10/8 kur. 28-29

Kuutazama Ulimwengu

Utumizi wa Tumbaku

Ingawa utumizi wa tumbaku umepungua sana katika nchi fulani, mataifa mengi huonyesha ongezeko kwa miongo miwili iliyopita. Kwa kielelezo, China bado ndiyo mtumizi mkuu ulimwenguni na ilikuwa na ongezeko la asilimia 297. Marekani na India zilidumisha nambari mbili na tatu kwa utumizi nazo zilipata ongezeko la asilimia 27 na 50. Nchi nyinginezo zenye maongezeko makubwa ni Rwanda ikiwa na asilimia 388; Ugiriki, asilimia 331; Korea Kaskazini, asilimia 325; Tanzania, asilimia 227; Hong Kong, asilimia 214; Indonesia, asilimia 193; Singapore, asilimia 186; na Uturuki, asilimia 185. Tarakimu hizo, zilizochapwa katika Asiaweek, huonyesha badiliko la asilimia kati ya 1970 na 1993. Kati ya mataifa 138 yaliyoorodheshwa, ni 26 tu yaliyoonyesha upungufu katika utumizi wa tumbaku.

Vijana na Bunduki

Vifo visababishwavyo na milipuo ya bunduki vyaongezeka sana miongoni mwa vijana wa Marekani wenye umri wa miaka 10 hadi 19 kuliko kikundi kinginecho chote, yasema ripoti iliyotolewa na Hazina ya Ulinzi wa Watoto. Bunduki sasa ndizo kisababishi cha pili cha kifo. Aksidenti, hasa za magari, ndizo kisababishi kikuu. Kati ya vijana Wamarekani walio chini ya umri wa miaka 20, mmoja alikufa kila baada ya dakika 92 kutokana na mlipuo wa bunduki katika 1993—ongezeko la asilimia 7 kupita mwaka uliotangulia. Kwa kulinganisha, kwa marika yote, ongezeko lilikuwa asilimia 4.8 tu. Hazina ya ulinzi ilishtaki serikali kwa kutofanya mengi ili kuondosha bunduki kutoka kwa watoto na shule. Yaonekana tarakimu za Idara ya Sheria ya Marekani zakubaliana na hilo: Idadi ya vijana walio wauaji-kimakusudi imeongezeka mara tatu katika mwongo uliopita, ikipita 26,000 katika 1994. Idadi ya wale wanaotumia bunduki zikiwa silaha yao ya kuua imeongezeka mara nne katika kipindi hicho hicho, ingawa idadi ya wale wanaotumia silaha nyinginezo imebaki karibu vile vile. Tarakimu hizo hukazia uharibifu unaofanywa na kupatikana kwa bunduki.

Vitabia vya Ujiuaji-Kimakusudi

“Wamarekani wapatao 30,000 [hujiua] kila mwaka,” lataja gazeti Scientific American, na “kuna uwezekano mara nne kwa wanaume kujiua kuliko wanawake.” Kiwango cha ujiuaji-kimakusudi pia chaongezeka kulingana na kuzidi kwa umri, ikionyesha mikazo ya afya mbaya na mataraja yanayopungua. Kiwango cha ujiuaji-kimakusudi miongoni mwa wale wenye umri wa miaka 75 au zaidi ni mara nne kuliko ule wa matineja. Ni mambo gani ambayo huamua ikiwa mtu hasa atajiua kimakusudi? Sababu kuu ni ukosefu wa utegemezo wa familia na jumuiya na kutoshiriki sana katika dini. Vikilinganishwa na nchi nyinginezo viwango vya Marekani vya ujiuaji-kimakusudi viko katikati, kukiwa na kiwango cha ujiuaji-kimakusudi 11 hivi kwa kila watu 100,000.

Kujifunza Jeuri

◼ “Uchunguzi wa mwaka mmoja wa programu za televisheni, uliofanywa na watafiti katika vyuo vikuu vinne, hufikia mkataa kwamba jeuri ‘yenye kudhuru kiakili’ imeenea sana katika programu za televisheni,” lasema gazeti The Washington Post. Uchunguzi haukupata tu kwamba programu nyingi zilikuwa na jeuri bali pia kwamba namna ambavyo jeuri hiyo ilionyeshwa ingeweza kuwa na athari zenye madhara kwa watazamaji. Athari hizo “hutia ndani kujifunza kuenenda kwa jeuri, kutohisi chochote kutokana na matokeo yenye kudhuru ya jeuri na kuogopa sana kushambuliwa.” Sababu moja ilikuwa kwamba wakosaji katika asilimia 73 ya visa vya matendo yenye jeuri katika televisheni hukosa kuadhibiwa, ikitoa ujumbe kwamba “jeuri hufanikiwa.” Pia, maonyesho mengi hayaonyeshi matokeo kwa wahasiriwa, kama vile maumivu au madhara ya kihisia-moyo au ya kifedha. Na uchunguzi huo wasema kwamba utumizi wa mara kwa mara wa bastola katika visa vya jeuri kwenye televisheni waweza “kuanzisha mawazo na mienendo yenye ukatili.”

◼ Kufikia umri wa miaka 30, watu waliotazama jeuri nyingi ya televisheni walipokuwa wachanga “watakuwa na hatia nyingi zaidi za makosa ya jeuri, kukamatwa zaidi kwa sababu ya kuendesha gari wakiwa walevi, kuwa wakali zaidi wanapokuwa wamekunywa alkoholi na kutendea wenzi wao wa ndoa vibaya zaidi [na] pia kuwa na watoto wakali zaidi,” adai Len Eron, profesa wa saikolojia na utafiti kwenye Taasisi ya Utafiti wa Kijamii ya Chuo Kikuu cha Michigan. Michezo ya vidio husababisha matatizo sawa na hayo. Kama ilivyoripotiwa katika gazeti la habari The Toronto Star, Eron alisema kwamba hatari inayohusianishwa na mchezo wa vidio ni kwamba huo ni wenye kuhusisha anayecheza. Wachezaji “husogeza wenzo au kubofya kibonyezo na wao wenyewe wanatenda tendo hili baya la jeuri—kuua mtu fulani.” Profesa Eron ahisi kwamba usimamizi zaidi wa kimzazi wahitajiwa. Hata hivyo, yeye aomboleza kwamba “wazazi wengi hawajali kabisa.”

Uhaba wa Makasisi Katika Ufaransa Waongezeka

Uhaba wa makasisi Wakatoliki katika Ufaransa waongezeka. Gazeti la habari la Paris Le Monde laripoti kwamba katika 1995, kulikuwa na makasisi 96 tu waliotawazwa katika Ufaransa yote na 121 tu katika 1994. Wayesuiti walikuwa tu na wanafunzi 7 na Wadominika 25 katika 1995. Hali iko vivyo hivyo katika kuandikishwa kwa watawa wa kike Wakatoliki. Le Monde lasema kwamba “tangu miaka ya 1970, idadi ya watawa wa kike imeendelea kupungua sana, kutoka 92,326 katika 1977 hadi 51,164 tu mwaka jana.” Kupatana na umri wa kuzeeka wa wengi wa makasisi na ukosefu wa kanisa kuvutia wazoezwaji wapya, inatabiriwa kwamba kufikia mwaka 2005, kutakuwa na makasisi wa parokia 9,000 hivi katika Ufaransa. Le Monde hutaja “kupungua kwa makasisi katika kiwango cha kijamii, hofu za watu za uwajibikaji wa muda mrefu, maoni yasiyofaa kuelekea makasisi, na ukosefu wa kuwa na uhakika katika viongozi wa kanisa” kuwa sababu ya upungufu huo.

Saa Iliyo Sahihi Kuliko Zote Ulimwenguni

Saa ambayo ni sahihi mara elfu moja kuliko saa atomia zitumiwazo katika Uingereza ili kuamua kiwango cha wakati kikubalikacho kimataifa imetokezwa na wanasayansi katika Perth, Australia Magharibi. Ikiitwa saa-yakuti, hiyo hugharimu dola 200,000 hivi, na tayari kadhaa zimetengenezwa. Yaweza kupima femtosecond moja ipitayo kwa haraka, ambayo ni sehemu moja ya milioni ya sehemu ya bilioni ya sekunde! Kazi yayo ni nini? Kulingana na nadharia ya jumla ya Einstein ya nguvu za uvutano na mchapuko, wakati huenda mbio zaidi ikiwa mtu yuko juu zaidi ya dunia. “Lengo letu ni kupima tofauti ya kasi kati ya meta moja hivi—yaani kati ya nyayo zako na kichwa chako,” akasema mwanafizikia David Blair, ambaye alifanyia kazi kutengeneza saa hiyo. Hata hivyo, uthabiti wayo hudumu kwa dakika tano kwa wakati.

Sandwichi ya Hali ya Chini?

Katika 1762, Bwana Sandwich wa Uingereza, mwenye mazoea ya kucheza kamari, alikaa kwa muda wa saa 24 kwenye meza ya kuchezea kamari. Ili kutosheleza njaa yake, aliitisha silesi mbili za mkate pamoja na kipande cha nyama katikati yazo. Chakula hiki chepesi kipya—ile sandwichi—kikaitwa kwa jina lake. Waingereza sasa hutumia dola milioni 7.9 kila siku kwa sandwichi, ongezeko la asilimia 75 katika miaka mitano iliyopita. “Sandwichi huwa thuluthi ya biashara ya vyakula vitengenezwavyo haraka,” laripoti The Times la London, nazo hutolewa katika meza za kuuzia 8,000. Sandwichi zilizotengenezwa tayari zipatazo bilioni 1.3 huliwa Uingereza kila mwaka. Hata hivyo, sandwichi hizi mara nyingi ziko tofauti sana na vile vyakula sahili ambavyo familia hufunga wanapokwenda mandarini mashambani au ufuoni. Maduka fulani huandaa aina tofauti kabisa, kutia ndani sandwichi zilizotengenezwa kutokana nyama ya kangaruu au aligeta au mkate wa chokoleti uliotiwa zabibubua na krimu.

Biashara ya Asia ya Ngono ya Watoto

Wafanyakazi wa serikali na wa kijamii hukadiria kwamba zaidi ya wavulana na wasichana milioni moja, wenye umri wa miaka 17 na wachanga zaidi, wanahusika katika ukahaba katika Asia, lataarifu gazeti The New York Times. Ingawa tarakimu hususa hazijulikani, watoto ambao hata hawajafikia ubalehe wanaweza kupatikana katika madanguro ya nchi kama vile Kambodia, China, India, Filipino, Taiwan, na Thailand. Kwa nini watoto ambao ni wachanga sana wanatafutwa? Sababu moja ni hofu ya UKIMWI. “Wanaume kotekote Asia wanageukia watoto wadogo zaidi, sababu moja ikiwa ni kwamba hawaelekei sana kuambukizwa H.I.V., kirusi kisababishacho UKIMWI,” lasema Times. Hata hivyo, kirusi cha UKIMWI kinaenea kwa haraka sana miongoni mwa makahaba katika nchi hizo, sababu moja ikiwa ni kupitishwa kwa makahaba kuvuka mipaka na sababu nyingine ikiwa kwamba wateja, wengine wakiwa katika utalii wa kutafuta wenzi wa ngono, husafiri mahali pamoja hadi pengine. Ingawa watoto fulani hutoroshwa kwa ajili ya ukahaba, wengine wanauzwa na wazazi wao kwa ajili ya mapato ya kimwili.

Uadui au Muungano?

“Sherehe ya kukumbuka mwaka wa 2000 wa kuzaliwa kwa Kristo kwa haraka sana inakuwa suala nyetivu kati ya makanisa,” laripoti ENI (Habari za Kimataifa za Kikanisa) Bulletin. Konrad Raiser, katibu mkuu wa Baraza la Makanisa Ulimwenguni, ameomba makanisa yafikirie tukio hilo “kuwa pindi ya ushirikiano na muungano—badala ya mashindano na kutaka kuonekana.” Ingawa hivyo, alisema kwamba makanisa yalionekana yalikuwa na nia zaidi ya kuutumia mwaka huo kuwa “pindi ya kueneza evanjeli . . . ili kushinda kutengwa kwayo na umma.” Huku akimpongeza papa kwa ombi lake la kuwa na mwaka 2000 “ukiwa pindi ya uhakikisho imara wa muungano wa Kikristo,” Raiser aliongeza: “Kadiri ya kutimizwa kwa dhana hizi kufikia mwaka 2000 ni jambo linalobaki kuonwa—maono ya wakati uliopita hutokeza mashaka.”

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki